Je, kusafiri kwa Uber kunagharimu pesa ngapi?
Panga safari itakayofuata kupitia mfumo wa kukadiria nauli.
Jinsi bei hukadiriwa
Katika miji mingi, nauli unayolipa huhesabiwa mapema, kabla hujathibitisha safari. Katika miji mingine, utaona makadirio ya bei.* Hizi ni baadhi ya ada na mambo yanayoweza kuathiri bei yako:
Ada ya kawaida
Ada ya kawaida inategemea wakati na umbali wa safari.
Ada ya uendeshaji
Katika jiji lako, huenda ukatozwa ada isiyobadilika kwa kila safari. Inasaidia kulipia gharama za uendeshaji, udhibiti na usalama.
Nyakati na maeneo yenye wateja wengi
Wakati kuna wasafiri wengi kuliko madereva wanaopatikana, bei zinaweza kuongezeka kwa muda hadi idadi ya madereva na wasafiri ilingane.
Aina za usafiri ukiwa eneo husika
Kupata pesa kwa kuendesha gari kwa kutumia App ya Uber
Unapoendesha gari
Endesha gari ukitumia Uber unapotaka na upate pesa kulingana na ratiba yako.
Njia nyingine
Gundua nyenzo na ofa zilizo kwenye programu ambazo zinaweza kukusaidia upate mapato zaidi.
Maswali yanayoulizwa sana
- Ni wakati gani nitatozwa ada ya safari?
Nauli utakayolipa itahesabiwa na kuwekwa kwenye njia ya malipo uliyoweka moja kwa moja baada ya kuwasili katika eneo unakoenda.
- Ninaweza kupata usafiri wa Uber kutoka uwanja wa ndege?
Down Small Ndiyo, unaweza kuitisha usafiri kwenda na kuondoka kwenye viwanja vingi vikuu vya ndege kote ulimwenguni. Nenda kwenye ukurasa wetu wa viwanja vya ndege ili uone maeneo ambayo Uber inapatikana.
- Ninaweza kulipia safari kwa Uber kwa pesa taslimu?
Down Small Katika miji mingi, malipo ya huduma za Uber hufanyika kielektroniki. Katika miji ambako malipo hufanyika kwa pesa taslimu, ni lazima uteue chaguo hili kabla ya kuitisha usafiri.
- Ninapataje kadirio la nauli kwenye programu?
Down Small Fungua programu na uweke mahali unakoenda katika kisanduku cha “Unaenda wapi?”. Utaona kadirio la bei kwa kila chaguo la safari; sogeza ili uone linalopatikana katika eneo lako.
Fanya mambo zaidi ndani ya App
Fanya mambo zaidi ndani ya App
Kuhusu