Please enable Javascript
Ruka uende katika maudhui ya msingi

Uwanja wa Ndege wa Berlin Tegel (TXL)

Iwe unasafiri unatoka Uwanja wa Ndege wa Berlin kwenda katikati ya jiji au kutoka jijini kwenda Uwanja wa Ndege wa Berlin, iamini Uber kukufikisha unakoenda.

13405
+49 30-60-91-11-50

search
Where from?
Navigate right up
search
Where to?

Omba safari kote ulimwenguni

Bofya kitufe sasa na upate usafiri wa uwanja wa ndege katika zaidi ya vituo vikuu 700.

Safiri kama mkazi

Acha programu na dereva wako washughulikie maelezo ya kina ili usisumbuke kutafuta maelekezo katika mji usiofahamu.

Safiri bila wasiwasi ukitumia Uber

Pata vipengele unavyovipenda, ikiwemo bei za wakati halisi na malipo ya kielektroniki, hata ukiwa ugenini.

Njia za kusafiri katika eneo husika

Chukua msafiri katika Uwanja wa Ndege wa Berlin Tegel (TXL)

Fungua programu yako ili uombe safari

Ukiwa tayari, fungua programu ya Uber ili uombe safari ya kuelekea mahali unakoenda. Chagua chaguo la usafiri wa uwanja wa ndege wa TXL linalokidhi mahitaji ya idadi ya wasafiri na mizigo yenu.

Fuata maelekezo kwenye programu

Utapata maelekezo kuhusu maeneo ya kuchukua wasafiri ya Tegel moja kwa moja kwenye programu. Maeneo ya kuchukua wasafiri yanaweza kutofautiana kulingana na kituo. Ishara za maeneo ya kuchukua wasafiri wanaosafiri pamoja zinaweza pia kupatikana katika Uwanja wa Ndege wa Berlin Tegel.

Kutana na dereva wako

Nenda kwenye eneo lako la kuchukuliwa la TXL kama ilivyobainishwa kwenye programu. Tafadhali kumbuka: eneo hili huenda lisiwe kwenye lango la kutoka lililo karibu zaidi nawe. Jina la dereva wako, nambari ya leseni na rangi ya gari itaonyeshwa kwenye programu. Thibitisha gari lako kabla ya kuingia. Ikiwa humpati dereva wako, wasiliana naye kupitia programu.

Maswali ambayo wasafiri wanauliza sana

  • Uber inapatikana katika Uwanja wa Ndege wa Berlin Tegel, kwa hivyo unaweza kufurahia usafiri wa starehe na uhakika popote unapotaka kwenda.

  • Ili kupata eneo la kuchukuliwa, angalia programu ya Uber baada ya kuitisha usafiri.

  • Hata kama safari si ndefu sana, ada za Uber kutoka na kwenda Uwanja wa Ndege wa Tegel zinaweza kuathiriwa na muda, foleni na masuala mengine. Angalia mfumo wa kukadiria nauli wa Uber ili ufahamu makadirio ya nauli ya safari.

  • Muda wa kuchukuliwa unaweza kuwa tofauti kulingana na wakati, idadi ya madereva wanaopatikana na masuala mengine.

Taarifa zaidi

  • Unaendesha gari ukitumia Uber?

    Kuanzia eneo la kuwachukua wasafiri hadi kufuata sheria na kanuni za mahali husika, fahamu jinsi ya kufanya safari zako za uwanja wa ndege ziwe bora zaidi.

  • Unaelekea uwanja tofauti wa ndege?

    Unaweza kushushwa na kuchukuliwa kutoka zaidi ya viwanja 700 vya ndege kote ulimwenguni.

1/2

Mambo unayofaa kufanya ukiwa katika vituo vya Berlin Tegel

Uber ni chaguo bora kwa wasafiri wanaowasili au kuondoka kwenye Uwanja wa Ndege wa Berlin. Berlin Tegel ni uwanja wa ndege wa 4 wenye shughuli nyingi zaidi nchini Ujerumani. Unahudumia zaidi ya wasafiri milioni 20 kila mwaka. Uwanja wa Ndege wa TXL uko umbali wa takribani kilomita 8 (maili 5) kutoka katikati mwa mji wa Berlin, upande wa kaskazini mwa mji. Hali hii inafanya wasafiri wanaowasili au kuondoka kutoka mji mkuu wa Ujerumani kufika TXL kwa urahisi. Uwanja huu wa ndege unahudumia miji mikuu mbalimbali barani Ulaya na maeneo mengine ya kimataifa.

Vituo vya Uwanja wa Ndege wa Berlin Tegel

Uwanja wa Ndege wa Berlin Tegel una vituo 3 vya wasafiri: Kituo cha A/B, C na D. Ingawa ghorofa ya chini ya eneo la wanaowasili katika kituo cha D inaitwa Kituo cha E, hakichukuliwi kuwa kituo tofauti. Huduma mbalimbali kwenye vituo katika Uwanja wa Ndege wa Berlin Tegel zinajumuisha vyumba vya kulala, kuhifadhi mizigo na posta. Mashirika mengi ya ndege yanayosafirisha wasafiri kutoka TXL yanajumuisha:

  • Aer Lingus
  • Croatian Airlines
  • easyJet
  • Turkish Airlines

Migahawa kwenye Uwanja wa Ndege wa Tegel

Iwe unahitaji kahawa kwa haraka kabla ya safari ya alfajiri au unatafuta chakula halisi cha Kijerumani, kuna migahawa mingi kwenye Uwanja wa Ndege wa Berlin Tegel ya kugundua.

Kusafiri kwenye Uwanja wa Ndege wa Berlin Tegel

Mabasi na treni mbalimbali zinawaunganisha wasafiri kwenye Uwanja wa Ndege wa Tegel haraka na kwa urahisi. Kwa mfano, vituo 4 vya BVG vinapatikana nje ya Kituo cha A/B, ilhali basi la kuelekea Dresden husimama karibu na Kituo cha E. Isitoshe kampuni nyingi za kukodisha magari zinapatikana kwenye Uwanja wa Ndege wa Berlin Tegel. Zinapatikana kwenye kituo cha kukodisha magari, kwenye ghorofa ya chini, karibu na Kituo cha E.

Mambo unayoweza kufanya katika TXL

Maduka kwenye Uwanja wa Ndege wa Berlin Tegel yana aina mbalimbali za bidhaa unazohitaji, kama vile mavazi, vifaa na vitabu. Maduka ya bidhaa zisizotozwa ushuru katika Tegel ni sehemu bora ya kununulia marafiki na familia zawadi. Maduka haya mengi haya bidhaa za msingi unazohitaji katika safari za ndege za mbali.

Sebule kwenye Uwanja wa Ndege wa Tegel

Uwanja wa Ndege wa Berlin Tegel una sebule mbalimbali, zinazokufaa kwa ajili ya kazi na mapumziko. Unaweza kutulia katika sebule ya Lufthansa baada ya uchovu wa safari. Sebule ya C-Lounge inakupa fursa ya kupata vinywaji, magazeti na muunganisho kwenye WiFi. Sebule katika Uwanja wa Ndege wa Berlin Tegel ni bora kwa mtu yeyote anayetaka kufanya kazi kabla ya safari.

Hoteli karibu na Uwanja wa Ndege wa Berlin

Iwe unatafuta mahali pa kupumzika muda mfupi au muda mrefu, hoteli nyingi karibu na Uwanja wa Ndege wa Tegel mjini Berlin zinajumuisha vyumba vya bei nafuu na vingine ya kifahari. Kwa hivyo unaweza kupata sehemu nzuri ya kupumzika baada ya safari yako au kufanya ziara fupi kwenye katikati mwa mji wa Berlin, mahali ambapo hoteli nyingi hupatikana.

Maeneo ya kuvutia karibu na Uwanja wa Ndege wa Berlin Tegel

Ikiwa unasubiri ndege nyingine ya baadaye katika Uwanja wa Ndege wa Berlin TXL kuna vitu mbalimbali unavyoweza kuona au kufanya katika maeneo ya karibu. Unaweza kwenda kwa urahisi katikati mwa mji wa Berlin kwa kutumia Uber. Kwa hivyo unaweza kuchagua kuzuru mji huu, pengine pamoja na maeneo haya ya kihistoria yaliyo maarufu kote ulimwenguni:

  • Brandenburg Gate
  • Charlottenburg Palace
  • Checkpoint Charlie
  • Reichstag

Pata maelezo zaidi kuhusu Uwanja wa Ndege wa TXLhapa.

Facebook
Instagram
Twitter

Ukurasa huu una taarifa kutoka kwenye tovuti za wahusika wengine ambazo hazidhibitiwi na Uber na zinazoweza kubadilishwa au kusasishwa kila baada ya kipindi fulani. Taarifa yoyote iliyojumuishwa kwenye ukurasa huu ambayo haihusiani moja kwa moja na Uber au uendeshaji wake ni kwa madhumuni ya kuarifu pekee na haifai kutegemewa au kufasiriwa au kuchambuliwa kwa namna inayoweka dhamana za aina yoyote, iwe zimeelezewa au kudokezewa, kuhusu taarifa iliyomo. Matakwa na vipengele fulani hutofautiana kulingana na nchi, eneo na mji.