Ruka uende katika maudhui ya msingi

Uwanja wa Ndege wa Berlin Tegel (TXL)

Iwe unasafiri unatoka Uwanja wa Ndege wa Berlin kwenda katikati ya jiji au kutoka jijini kwenda Uwanja wa Ndege wa Berlin, iamini Uber kukufikisha unakoenda.

Zufahrt zum Flughafen Tegel, 13405 Berlin, Germany
+49 30-60-91-11-50

Njia bora zaidi ya kusafiri

Itisha usafiri kote ulimwenguni

Bonyeza tu kitufe ili upate usafiri wa angani katika zaidi ya viwanja vikuu 500.

Safiri kama mwenyeji

Acha App na dereva wako ashughulikie masuala ya kina ili usisumbuke kutafuta maelekezo katika jiji ambapo wewe ni mgeni.

Safiri bila wasiwasi kwa kutumia Uber

Pata vipengele unavyovipenda, ikiwa ni pamoja na bei zinazooneshwa moja kwa moja na uwezo wa kulipa bila pesa taslimu, hata ukiwa ugenini.

Aina za usafiri ukiwa eneo husika

 • Comfort

  1-3

  Extra legroom and top rated drivers

 • UberX

  1-3

  Affordable everyday trips

 • Premium

  1-3

  High-end trips with professional drivers

 • UberXL

  1-5

  Fits 5 riders or 3 riders with luggage

 • Green

  1-3

  Emission-free, affordable, everyday rides

 • Taxi

  1-3

  Local taxi-cabs at the tap of a button

1/6

Jinsi ya kupata usafiri wa Uber kutoka uwanja wa ndege

Fungua App yako ili uitishe usafiri

Ukiwa tayari kutoka nje, fungua programu yako kisha uitishe usafiri. Chagua usafiri unaotoshea idadi ya wasafiri na mizigo mliyo nayo.

Fuata maelekezo katika App

Utapata maelekezo kuhusu eneo la kuchukua wasafiri moja kwa moja katika programu. Pia kunaweza kuwa na alama katika uwanja wa ndege.

Kutana na dereva wako

Nenda katika eneo la kuchukuliwa jinsi ilivyobainishwa katika App. Tafadhali kumbuka, eneo hilo huenda halitakuwa karibu kabisa na lango unaloondokea. Ikiwa humpati dereva wako, wasiliana naye kupitia App.

Vidokezo vya kuzingatia katika Uwanja wa Ndege wa TXL

WiFi katika Uwanja wa Ndege wa Tegel

Free wifi is available 24/7 at TXL Airport, so connecting from your laptop, tablet, or mobile device is easy. Just access the hotspot and accept the terms and conditions, and you’ll be online in no time.

Maegesho katika uwanja wa ndege wa Berlin Tegel

Uwanja wa Ndege wa Berlin Tegel una zaidi ya nafasi 2,500 za maegesho. Mbali na maegesho ya ghorofa kwa ajili ya kuegesha gari kwa muda mrefu, kuna maegesho ya muda mfupi kwa ajili ya kushukisha na kuchukua wasafiri.

Kuhifadhi mizigo katika Uwanja wa Ndege wa Tegel

Uwanja wa Ndege wa Berlin una sehemu za kuhifadhi mizigo zinazokuruhusu kuweka mikoba yako kwa saa au siku, iwe unasubiri ndege au kama unataka kuzuru jiji. Isitoshe, unaweza kupata huduma za posta na kufungasha mizigo katika sehemu ya huduma katika Kituo cha A.

Maswali ambayo wasafiri wanauliza sana

 • Uber inapatikana katika Uwanja wa Ndege wa Berlin Tegel, kwa hivyo unaweza kufurahia usafiri wa starehe na uhakika popote unapotaka kwenda.

 • Ili kupata eneo la kuchukuliwa, angalia programu ya Uber baada ya kuitisha usafiri.

 • Hata kama safari si ndefu sana, ada za Uber kutoka na kwenda Uwanja wa Ndege wa Tegel zinaweza kuathiriwa na muda, foleni na masuala mengine. Angalia mfumo wa kukadiria nauli za Uber ili ufahamu makadirio ya nauli ya safari.

 • Muda wa kuchukuliwa unaweza kuwa tofauti kulingana na wakati, idadi ya madereva wanaopatikana na masuala mengine.

Maelezo zaidi

Je, unaelekea uwanja tofauti wa ndege?

Unaweza kupelekwa na kuchukuliwa kutoka zaidi ya viwanja 600 vya ndege kote duniani.

Mambo unayofaa kufanya ukiwa katika vituo vya Berlin Tegel

Uber ni chaguo bora kwa wasafiri wanaowasili au kuondoka kwenye Uwanja wa Ndege wa Berlin. Berlin Tegel ni uwanja wa ndege wa 4 wenye shughuli nyingi zaidi nchini Ujerumani. Unahudumia zaidi ya wasafiri milioni 20 kila mwaka. Uwanja wa Ndege wa TXL uko umbali wa takribani kilomita 8 (maili 5) kutoka katikati mwa mji wa Berlin, upande wa kaskazini mwa mji. Hali hii inafanya wasafiri wanaowasili au kuondoka kutoka mji mkuu wa Ujerumani kufika TXL kwa urahisi. Uwanja huu wa ndege unahudumia miji mikuu mbalimbali barani Ulaya na maeneo mengine ya kimataifa.

Vituo vya Uwanja wa Ndege wa Berlin Tegel

Uwanja wa Ndege wa Berlin Tegel una vituo 3 vya wasafiri: Kituo cha A/B, C na D. Ingawa ghorofa ya chini ya eneo la wanaowasili katika kituo cha D inaitwa Kituo cha E, hakichukuliwi kuwa kituo tofauti. Huduma mbalimbali kwenye vituo katika Uwanja wa Ndege wa Berlin Tegel zinajumuisha vyumba vya kulala, kuhifadhi mizigo na posta. Mashirika mengi ya ndege yanayosafirisha wasafiri kutoka TXL yanajumuisha:

 • Aer Lingus
 • Croatian Airlines
 • easyJet
 • Turkish Airlines

Migahawa kwenye Uwanja wa Ndege wa Tegel

Iwe unahitaji kahawa kwa haraka kabla ya safari ya alfajiri au unatafuta chakula halisi cha Kijerumani, kuna migahawa mingi kwenye Uwanja wa Ndege wa Berlin Tegel ya kugundua.

Kusafiri kwenye Uwanja wa Ndege wa Berlin Tegel

Mabasi na treni mbalimbali zinawaunganisha wasafiri kwenye Uwanja wa Ndege wa Tegel haraka na kwa urahisi. Kwa mfano, vituo 4 vya BVG vinapatikana nje ya Kituo cha A/B, ilhali basi la kuelekea Dresden husimama karibu na Kituo cha E. Isitoshe kampuni nyingi za kukodisha magari zinapatikana kwenye Uwanja wa Ndege wa Berlin Tegel. Zinapatikana kwenye kituo cha kukodisha magari, kwenye ghorofa ya chini, karibu na Kituo cha E.

Mambo unayoweza kufanya katika TXL

Maduka kwenye Uwanja wa Ndege wa Berlin Tegel yana aina mbalimbali za bidhaa unazohitaji, kama vile mavazi, vifaa na vitabu. Maduka ya bidhaa zisizotozwa ushuru katika Tegel ni sehemu bora ya kununulia marafiki na familia zawadi. Maduka haya mengi haya bidhaa za msingi unazohitaji katika safari za ndege za mbali.

Sebule kwenye Uwanja wa Ndege wa Tegel

Uwanja wa Ndege wa Berlin Tegel una sebule mbalimbali, zinazokufaa kwa ajili ya kazi na mapumziko. Unaweza kutulia katika sebule ya Lufthansa baada ya uchovu wa safari. Sebule ya C-Lounge inakupa fursa ya kupata vinywaji, magazeti na muunganisho kwenye WiFi. Sebule katika Uwanja wa Ndege wa Berlin Tegel ni bora kwa mtu yeyote anayetaka kufanya kazi kabla ya safari.

Hoteli karibu na Uwanja wa Ndege wa Berlin

Iwe unatafuta mahali pa kupumzika muda mfupi au muda mrefu, hoteli nyingi karibu na Uwanja wa Ndege wa Tegel mjini Berlin zinajumuisha vyumba vya bei nafuu na vingine ya kifahari. Kwa hivyo unaweza kupata sehemu nzuri ya kupumzika baada ya safari yako au kufanya ziara fupi kwenye katikati mwa mji wa Berlin, mahali ambapo hoteli nyingi hupatikana.

Maeneo ya kuvutia karibu na Uwanja wa Ndege wa Berlin Tegel

Ikiwa unasubiri ndege nyingine ya baadaye katika Uwanja wa Ndege wa Berlin TXL kuna vitu mbalimbali unavyoweza kuona au kufanya katika maeneo ya karibu. Unaweza kwenda kwa urahisi katikati mwa mji wa Berlin kwa kutumia Uber. Kwa hivyo unaweza kuchagua kuzuru mji huu, pengine pamoja na maeneo haya ya kihistoria yaliyo maarufu kote ulimwenguni:

 • Brandenburg Gate
 • Charlottenburg Palace
 • Checkpoint Charlie
 • Reichstag

Pata maelezo zaidi kuhusu Uwanja wa Ndege wa TXLhapa.

Facebook
Instagram
Twitter

Ukurasa huu una taarifa kutoka kwenye tovuti za washirika wengine ambazo hazisimamiwi na Uber na zinaweza kugeuzwa au kubadilishwa mara kwa mara. Maelezo yoyote yaliyojumuishwa kwenye ukurasa huu ambayo hayahusiani moja kwa moja na Uber au kazi zake yanatumika kuarifu tu na hayafai kutegemewa, au kuchukuliwa au kufasiliwa kwa namna inayoweka dhamana ya aina yoyote, iwe ya moja kwa moja au inayokisiwa, kuhusu maelezo yaliyo hapa. Baadhi ya masharti na vipengele hutofautiana kutegemea nchi, eneo na jiji. Ofa ya punguzo inawalenga watumiaji wapya pekee. Huwezi kutumia ofa hii pamoja na ofa nyinginezo na haiwezi kutumiwa katika bakshishi. Inapatikana kwa muda mfupi. Vigezo na masharti ya ofa vinaweza kubadilika.