Please enable Javascript
Ruka uende katika maudhui ya msingi

Uwanja wa Ndege wa London Stansted (STN)

Looking for an alternative to the traditional Uwanja wa Ndege wa Stansted shuttle or taxi? Whether you’re heading from Stansted Airport to London or London to Stansted Airport, get where you’re going with the Uber app you already know. Request a trip to and from STN at the tap of a button.

Stansted, CM24 1QW
+44 808-169-7031

search
Where from?
Navigate right up
search
Where to?

Request a ride around the world

Bofya kitufe sasa na upate usafiri wa uwanja wa ndege katika zaidi ya vituo vikuu 700.

Safiri kama mkazi

Acha programu na dereva wako washughulikie maelezo ya kina ili usisumbuke kutafuta maelekezo katika mji usiofahamu.

Safiri bila wasiwasi ukitumia Uber

Pata vipengele unavyovipenda, ikiwemo bei za wakati halisi na malipo ya kielektroniki, hata ukiwa ugenini.

Ways to ride in the area

Pickup at Uwanja wa Ndege wa London Stansted (STN)

Fungua programu yako ili uombe safari

Ukiwa tayari, fungua programu ya Uber ili uombe safari ya kuelekea mahali unakoenda. Chagua chaguo la usafiri wa uwanja wa ndege wa STN linalokidhi mahitaji ya idadi ya wasafiri na mizigo yenu.

Fuata maelekezo kwenye programu

Utapata maelekezo kuhusu maeneo ya kuchukua wasafiri ya Uwanja wa Ndege wa Stansted moja kwa moja kwenye programu. Maeneo ya kuchukua wasafiri yanaweza kutofautiana kulingana na kituo. Ishara za maeneo ya kuchukua wasafiri wanaosafiri pamoja zinaweza pia kupatikana katika Uwanja wa Ndege wa London Stansted.

Kutana na dereva wako

Nenda kwenye eneo lako la kuchukuliwa la STN kama ilivyobainishwa kwenye programu. Tafadhali kumbuka: eneo hili huenda lisiwe kwenye lango la kutoka lililo karibu zaidi nawe. Jina la dereva wako, nambari ya leseni na rangi ya gari itaonyeshwa kwenye programu. Thibitisha gari lako kabla ya kuingia. Ikiwa humpati dereva wako, wasiliana naye kupitia programu.

Top questions from riders

  • Uber inapatikana katika Uwanja wa Ndege wa STN, kwa hivyo unaweza kufurahia usafiri wa starehe na uhakika popote unapotaka kwenda.

  • Hata kama safari si ndefu sana, ada za Uber kutoka na kwenda Uwanja wa Ndege wa Stansted zinaweza kuathiriwa na muda, foleni na masuala mengine. Ada za uwanja wa ndege na maegesho pia zinaweza kuongezwa kwenye nauli yako kamili ya safari.

  • Ili kupata eneo la kuchukuliwa, angalia programu ya Uber baada ya kuitisha usafiri.

  • Muda wa kuchukuliwa unaweza kuwa tofauti kulingana na wakati, idadi ya madereva wanaopatikana na masuala mengine. Mara baada ya kuitisha usafiri, angalia programu ili uone kadirio la muda wa kusubiri.

More information

  • Unaendesha gari ukitumia Uber?

    Kuanzia eneo la kuwachukua wasafiri hadi kufuata sheria na kanuni za mahali husika, fahamu jinsi ya kufanya safari zako za uwanja wa ndege ziwe bora zaidi.

  • Unaelekea uwanja tofauti wa ndege?

    Unaweza kushushwa na kuchukuliwa kutoka zaidi ya viwanja 700 vya ndege kote ulimwenguni.

1/2

Mambo ya kufanya ukiwa katika kituo cha Uwanja wa Ndege wa Stansted London

Uber ni chaguo bora kwa watu wanaowasili au kuondoka kwenye Uwanja wa Ndege wa STN. Uwanja wa Ndege wa London Stansted unahudumia zaidi ya wasafiri milioni 27 kila mwaka na ndio Kituo kikuu cha kusafiri kuenda na kutoka barani Ulaya. Ni uwanja wa ndege wa 3 wenye shughuli nyingi mjini London na wa 4 Uingereza. London Stansted inapatikana Stansted Mountfitchet, Essex, takribani kilomita 55 (maili 34) kaskazini mashariki mwa London—safari ya takriban saa 1.5 kwa gari, kutegemea hali ya foleni barabarani. Mji wenye chuo kikuu cha Cambridge pia uko karibu, umbali wa kilomita 45 (maili 28) kaskazini mwa Stansted.

Kituo cha Stansted

Kuna kituo kimoja tu kwenye Uwanja wa Ndege wa London Stansted, kilicho na jumla ya milango 88 ya wanaoondoka. Stansted inahudumia zaidi ya ndege 30, zikiwemo:

  • Air Corsica
  • Air Moldova
  • Aurigny
  • British Airways
  • easyJet
  • Emirates
  • Eurowings
  • Flybe
  • Jet2.com
  • Pegasus
  • Ryanair
  • Thomas Cook
  • TUI

Migahawa kwenye Uwanaja wa ndege wa Stansted

Kuna aina nyingi za vyakula na vinywaji kwenye Uwanja wa Ndege wa London Stansted. Kwenye eneo la wasafiri wa ndege na wa barabarani, utapata vyakula vitamu vya aina zote kama vile vitafunio, vyakula vya kubeba na vyakula vya kienyeji.

Kusafiri kwenye Uwanja wa Ndege wa London Stansted

STN ni uwanja mdogo na unaweza kutembea humo kwa urahisi. Kwa hivyo, hamna haja ya kutafuta mabasi au treni za kukupeleka kwenye lango lako.

Mambo ya kufanya kwenye Uwanja wa Ndege wa Stansted

Unaweza kupata aina mbalimbali za mavazi, vipodozi, mapambo, mitambo, pombe na bidhaa nyingine kwenye maduka mengi katika Uwanja wa Ndege wa Stansted. Utaweza kuingia katika maduka baada ya kukaguliwa kwenye sehemu ya wanaoondoka. Eneo la wanaowasili pia lina duka linalouza bidhaa zisizotozwa ushuru baada ya sehemu ya kuchukua mizigo na kuna maduka yanayokufaa kwenye kituo kikuu. Uwanja wa Ndege wa Stansted una chaguo la kuagiza bidhaa mapema, ambapo unaweza kuagiza bidhaa kabla hata ufike kwenye uwanja wa ndege na zitakuwa tayari kuchukuliwa unapowasili.

Maeneo ya maombi na ibada kwenye Uwanja wa Ndege wa Stansted

Utapata chumba cha maombi mkabala wa Check-In Zone A na kingine baada ya kukaguliwa na walinzi, kwenye eneo karibu na Escape Lounge katika eneo la wanaoondoka. Vyumba vya maombi hufunguliwa wakati wowote kwa waumini wa dini yoyote.

Migahawa Karibu na Uwanja wa Ndege wa London Stansted

Kuna migahawa mingi karibu na Uwanja wa Ndege wa London Stansted, kwa hivyo unaweza kutilia humo kabla ya safari. Labda una safari ya alfajiri na ungependa kukaribia uwanja wa ndege ili ulale au pengine unasubiri ndege nyingine usiku na hutaki kuenda mbali zaidi na uwanja wa ndege. Stansted ina aina mbalimbali za migahawa inayokidhi mahitaji yako na ikiwa utaweka nafasi ya hoteli moja kwa moja kwenye uwanja wa ndege, utaokoa hadi zaidi ya 40%. Migahawa mingi iliyo karibu pia ina vyumba vya mikutano, kama ilivyo United Business Centre ambako unaweza kufikia haraka kwa gari kutoka kwenye uwanja wa ndege. Bila shaka, kutokana na Stanstend kuwa karibu na mji wa London, utapata aina nyingi za vyumba kwa kusafiri kwa saa chache kutoka kwenye uwanja wa ndege.

Sehemu za kuzuru karibu na Stansted

  • Hatfield Forest
  • House on the Hill Toy Museum
  • Mountfitchet Castle

Pata maelezo zaidi kuhusu STN hapa.

Facebook
Instagram
Twitter

This page contains information from third-party websites that are not under the control of Uber and that may be periodically changed or updated. Any information included on this page that is not directly related to Uber or its operations is for informational purposes only and in no way shall be relied upon, or interpreted or construed to create any warranties of any kind, either express or implied, regarding the information contained herein. Certain requirements and features vary by country, region, and city.