Ruka uende katika maudhui ya msingi
Uber
Uber

Uwanja wa Ndege wa London Stansted (STN)

Iwe unasafiri kuelekea London kutoka Uwanja wa Ndege wa Stansted au kutoka London kuelekea Uwanja wa Ndege wa Stansted, iamini Uber kukufikisha unakoenda.

Bassingbourn Road, Stansted CM24 1QW, United Kingdom
+44 808-169-7031

Njia bora zaidi ya kusafiri

Itisha usafiri kote ulimwenguni

Bonyeza tu kitufe ili upate usafiri wa angani katika zaidi ya viwanja vikuu 500.

Safiri kama mwenyeji

Acha App na dereva wako ashughulikie masuala ya kina ili usisumbuke kutafuta maelekezo katika jiji ambapo wewe ni mgeni.

Safiri bila wasiwasi kwa kutumia Uber

Pata vipengele unavyovipenda, ikiwa ni pamoja na bei zinazooneshwa moja kwa moja na uwezo wa kulipa bila pesa taslimu, hata ukiwa ugenini.

Mfumo wa Uber wa kukadiria nauli

Sampuli za bei za msafiri ni makadirio tu na hazioneshi mabadiliko yanayotokana na mapunguzo, kucheleweshwa kwenye foleni na mambo mengine. Tunaweza kutumia nauli isiyobadilika na bei za chini zaidi. Bei halisi zinaweza kubadilika.

Njia za kusafiri

 • UberX1-4

  Usafiri wa bei nafuu unaopatikana kila siku

 • Exec1-4

  Usafiri wa magari ya kifahari wa kila siku

Jinsi ya kupata usafiri wa Uber kutoka uwanja wa ndege

Fungua App yako ili uitishe usafiri

Ukiwa tayari kutoka nje, fungua programu yako kisha uitishe usafiri. Chagua usafiri unaotoshea idadi ya wasafiri na mizigo mliyo nayo.

Fuata maelekezo katika App

Utapata maelekezo kuhusu eneo la kuchukua wasafiri moja kwa moja katika programu. Pia kunaweza kuwa na alama katika uwanja wa ndege.

Kutana na dereva wako

Nenda katika eneo la kuchukuliwa jinsi ilivyobainishwa katika App. Tafadhali kumbuka, eneo hilo huenda halitakuwa karibu kabisa na lango unaloondokea. Ikiwa humpati dereva wako, wasiliana naye kupitia App.

Vidokezo vya kuzingatia katika Uwanja wa Ndege wa Stansted

WiFi katika Uwanja wa Ndege wa Stansted

Unaweza kupata WiFi bila malipo kwa saa 4 katika Uwanja wa Ndege wa Stansted kila siku kwa kila simu uliyoandikisha. Unaweza kununua kifurushi cha ziada cha saa 24 au vifurushi vya miezi 6 au 12 kwa wanaosafiri mara kwa mara.

Maegesho katika Uwanja wa Ndege wa Stansted

Kuna aina mbalimbali za maegesho katika Uwanja wa Ndege wa Stansted yakiwemo yale ya muda mfupi, muda kiasi na muda mrefu. JetParks za karibu ni chaguo mbadala nafuu la kuegesha magari.

Kubadilisha fedha katika Uwanja wa Ndege wa Stansted

Kuna mitambo ya ATM kabla na baada ya vituo vya usalama katika Uwanja wa Ndege wa London Stansted. Mitambo hii hutoa sarafu za Pauni ya Uingereza, Yuro na dola za Marekani. Kuna madawati 7 ya Moneycorp ya kubadilisha fedha katika sehemu za kuwasili na kuondoka kwenye Uwanja wa Ndege wa London Stansted.

Maswali ambayo wasafiri wanauliza sana

Uber inapatikana katika Uwanja wa Ndege wa STN, kwa hivyo unaweza kufurahia usafiri wa starehe na uhakika popote unapotaka kwenda.

Hata kama safari si ndefu sana, ada za Uber kutoka na kwenda Uwanja wa Ndege wa Stansted zinaweza kuathiriwa na muda, foleni na masuala mengine. Ada za uwanja wa ndege na maegesho pia zinaweza kuongezwa kwenye nauli yako kamili ya safari.

Ili kupata eneo la kuchukuliwa, angalia programu ya Uber baada ya kuitisha usafiri.

Muda wa kuchukuliwa unaweza kuwa tofauti kulingana na wakati, idadi ya madereva wanaopatikana na masuala mengine. Mara baada ya kuitisha usafiri, angalia programu ili uone kadirio la muda wa kusubiri.

Maelezo zaidi

Unatumia mfumo wa Uber kuendesha gari?

Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kurahisisha huduma unayopokea katika viwanja vya ndege, zikiwemo sheria na kanuni za nchi husika.

Je, unaelekea uwanja tofauti wa ndege?

Unaweza kupelekwa na kuchukuliwa kutoka zaidi ya viwanja 500 vya ndege kote duniani.

Mambo ya kufanya ukiwa katika kituo cha Uwanja wa Ndege wa Stansted London

Uber ni chaguo bora kwa watu wanaowasili au kuondoka kwenye Uwanja wa Ndege wa STN. Uwanja wa Ndege wa London Stansted unahudumia zaidi ya wasafiri milioni 27 kila mwaka na ndio Kituo kikuu cha kusafiri kuenda na kutoka barani Ulaya. Ni uwanja wa ndege wa 3 wenye shughuli nyingi mjini London na wa 4 Uingereza. London Stansted inapatikana Stansted Mountfitchet, Essex, takribani kilomita 55 (maili 34) kaskazini mashariki mwa London—safari ya takriban saa 1.5 kwa gari, kutegemea hali ya foleni barabarani. Mji wenye chuo kikuu cha Cambridge pia uko karibu, umbali wa kilomita 45 (maili 28) kaskazini mwa Stansted.

Kituo cha Stansted

Kuna kituo kimoja tu kwenye Uwanja wa Ndege wa London Stansted, kilicho na jumla ya milango 88 ya wanaoondoka. Stansted inahudumia zaidi ya ndege 30, zikiwemo:

 • Air Corsica
 • Air Moldova
 • Aurigny
 • British Airways
 • easyJet
 • Emirates
 • Eurowings
 • Flybe
 • Jet2.com
 • Pegasus
 • Ryanair
 • Thomas Cook
 • TUI

Migahawa kwenye Uwanaja wa ndege wa Stansted

Kuna aina nyingi za vyakula na vinywaji kwenye Uwanja wa Ndege wa London Stansted. Kwenye eneo la wasafiri wa ndege na wa barabarani, utapata vyakula vitamu vya aina zote kama vile vitafunio, vyakula vya kubeba na vyakula vya kienyeji.

Kusafiri kwenye Uwanja wa Ndege wa London Stansted

STN ni uwanja mdogo na unaweza kutembea humo kwa urahisi. Kwa hivyo, hamna haja ya kutafuta mabasi au treni za kukupeleka kwenye lango lako.

Mambo ya kufanya kwenye Uwanja wa Ndege wa Stansted

Unaweza kupata aina mbalimbali za mavazi, vipodozi, mapambo, mitambo, pombe na bidhaa nyingine kwenye maduka mengi katika Uwanja wa Ndege wa Stansted. Utaweza kuingia katika maduka baada ya kukaguliwa kwenye sehemu ya wanaoondoka. Eneo la wanaowasili pia lina duka linalouza bidhaa zisizotozwa ushuru baada ya sehemu ya kuchukua mizigo na kuna maduka yanayokufaa kwenye kituo kikuu. Uwanja wa Ndege wa Stansted una chaguo la kuagiza bidhaa mapema, ambapo unaweza kuagiza bidhaa kabla hata ufike kwenye uwanja wa ndege na zitakuwa tayari kuchukuliwa unapowasili.

Maeneo ya maombi na ibada kwenye Uwanja wa Ndege wa Stansted

Utapata chumba cha maombi mkabala wa Check-In Zone A na kingine baada ya kukaguliwa na walinzi, kwenye eneo karibu na Escape Lounge katika eneo la wanaoondoka. Vyumba vya maombi hufunguliwa wakati wowote kwa waumini wa dini yoyote.

Migahawa Karibu na Uwanja wa Ndege wa London Stansted

Kuna migahawa mingi karibu na Uwanja wa Ndege wa London Stansted, kwa hivyo unaweza kutilia humo kabla ya safari. Labda una safari ya alfajiri na ungependa kukaribia uwanja wa ndege ili ulale au pengine unasubiri ndege nyingine usiku na hutaki kuenda mbali zaidi na uwanja wa ndege. Stansted ina aina mbalimbali za migahawa inayokidhi mahitaji yako na ikiwa utaweka nafasi ya hoteli moja kwa moja kwenye uwanja wa ndege, utaokoa hadi zaidi ya 40%. Migahawa mingi iliyo karibu pia ina vyumba vya mikutano, kama ilivyo United Business Centre ambako unaweza kufikia haraka kwa gari kutoka kwenye uwanja wa ndege. Bila shaka, kutokana na Stanstend kuwa karibu na mji wa London, utapata aina nyingi za vyumba kwa kusafiri kwa saa chache kutoka kwenye uwanja wa ndege.

Sehemu za kuzuru karibu na Stansted

 • Hatfield Forest
 • House on the Hill Toy Museum
 • Mountfitchet Castle

Pata maelezo zaidi kuhusu STN hapa.

Facebook
Instagram
Twitter