Please enable Javascript
Ruka uende katika maudhui ya msingi

Uwanja wa Ndege wa Istanbul Sabiha Gökçen (SAW)

Je, unatafuta mbinu mbadala ya usafiri ambayo si basi la kawaida la Uwanja wa Ndege wa Sabiha Gökçen au teksi? Iwe unasafiri kutoka Uwanja wa Ndege wa SAW hadi Istanbul au kutoka Istanbul hadi Uwanja wa Ndege wa SAW, fika unakoenda ukitumia programu ya Uber unayoijua tayari. Omba gari la kukupeleka na kukurudisha kutoka SAW kwa kubofya kitufe.

Pendik/Istanbul, 34906
+90 216-588-88-88

search
Where from?
Navigate right up
search
Where to?

Request a ride around the world

Bofya kitufe sasa na upate usafiri wa uwanja wa ndege katika zaidi ya vituo vikuu 700.

Safiri kama mkazi

Acha programu na dereva wako washughulikie maelezo ya kina ili usisumbuke kutafuta maelekezo katika mji usiofahamu.

Safiri bila wasiwasi ukitumia Uber

Pata vipengele unavyovipenda, ikiwemo bei za wakati halisi na malipo ya kielektroniki, hata ukiwa ugenini.

Ways to ride in the area

Pickup at Uwanja wa Ndege wa Istanbul Sabiha Gökçen (SAW)

Fungua programu yako ili uombe safari

Ukiwa tayari, fungua programu ya Uber ili uombe safari ya kuelekea mahali unakoenda. Chagua chaguo la usafiri wa uwanja wa ndege wa SAW linalokidhi mahitaji ya idadi ya wasafiri na mizigo yenu.

Fuata maelekezo kwenye programu

Utapata maelekezo kuhusu maeneo ya kuchukua wasafiri ya Uwanja wa Ndege wa Sabiha Gökçen moja kwa moja kwenye programu. Maeneo ya kuchukua wasafiri yanaweza kutofautiana kulingana na kituo. Ishara za maeneo ya kuchukua wasafiri wanaosafiri pamoja zinaweza pia kupatikana katika Uwanja wa Ndege wa Istanbul Sabiha Gökçen.

Kutana na dereva wako

Nenda kwenye eneo lako la kuchukuliwa la SAW kama ilivyobainishwa kwenye programu. Tafadhali kumbuka: eneo hili huenda lisiwe kwenye lango la kutoka lililo karibu zaidi nawe. Jina la dereva wako, nambari ya leseni na rangi ya gari itaonyeshwa kwenye programu. Thibitisha gari lako kabla ya kuingia. Ikiwa humpati dereva wako, wasiliana naye kupitia programu.

Top questions from riders

  • Uber inapatikana katika Uwanja wa Ndege wa SAW, kwa hivyo unaweza kufurahia usafiri wa starehe na uhakika popote unapotaka kwenda.

  • Ili kupata eneo la kuchukuliwa, angalia programu ya Uber baada ya kuitisha usafiri.

  • Hata kama safari si ndefu sana, ada za Uber kutoka na kwenda Uwanja wa Ndege wa Sahiba Gökçen zinaweza kuathiriwa na muda, foleni na masuala mengine. Angalia mfumo wa kukadiria nauli wa Uber ili ufahamu makadirio ya nauli ya safari.

  • Muda wa kuchukuliwa unaweza kuwa tofauti kulingana na wakati, idadi ya madereva wanaopatikana na masuala mengine.

More information

  • Unaendesha gari ukitumia Uber?

    Kuanzia eneo la kuwachukua wasafiri hadi kufuata sheria na kanuni za mahali husika, fahamu jinsi ya kufanya safari zako za uwanja wa ndege ziwe bora zaidi.

  • Unaelekea uwanja tofauti wa ndege?

    Unaweza kushushwa na kuchukuliwa kutoka zaidi ya viwanja 700 vya ndege kote ulimwenguni.

1/2

Mambo ya kufanya katika kituo cha Uwanja wa Ndege wa Istanbul

Uber ni chaguo bora kwa wasafiri wanaowasili au kuondoka kwenye Uwanja wa Ndege wa SAW. Uwanja wa Ndege wa Sabiha Gökçen ni moja ya nyanja za shughuli nyingi mjini Istanbul. Unahudumia wasafiri katika upande wa mashariki mwa mji huu na huwahudumia zaidi ya wasafiri milioni 25 kila mwaka. Uwanja wa ndege wa Sabiha Gökçen unapatikana upande wa Asia wa Istanbul, takribani kilomita 50 (maili 31) kutoka katikati mwa mji. Kwa mtu yeyote anayesafiri kuelekea upande wa Asia wa mji, na pia mji wa Darika, uwanja huu ni chaguo bora lenye vifaa vya kisasa kwa wasafiri. Lina ukubwa wa mita 320,000 mraba (fiti 3.4 mraba).

Kituo cha Uwanja wa Ndege wa Istanbul

Uwanja wa Sabiha Gökçen una jengo moja la kituo kinachohudumia safari za kimataifa na za nchini na kina vibanda 112 ya kuripoti. Katika uwanja wa ndege na majengo ya karibu, kuna ukumbi wa mikutano na jengo la VIP, pamoja na maegesho ya magari, hoteli na eneo la vyakula. Mashirika ya ndege yanayohudumu kwenye Uwanja wa Ndege wa Sabiha yanajumuisha:

  • Emirates
  • flydubai
  • Qatar
  • SunExpress
  • Turkish Airlines

Kusafiri kwenye Uwanja wa Ndege wa SAW

kwa vile Uwanja wa Ndege wa SAW una jengo moja la kituo, hamna haja kutumia gari kusafiri kutoka kituo kimoja hadi kingine. Usafiri mbalimbali unapatikana kuwapeleka na kuwaondoa watu kwenye uwanja wa ndege, zikiwemo teksi, mabasi, treni na Uber. Kuna pia kuna njia moja kwa moja ya kwenda kwenye barabara kuu ya TEM, hivyo kuwezesha watu wanaokodisha magari kwenye uwanja wa Ndege wa Istanbul Sabiha Gökçen kufikia mji wa Istanbul kwa urahisi. Maegesho yana ghorofa 4 na yanawafaa wasafiri wanaowasili kwenye uwanja wa ndege kwa kutumia magari yao.

Mambo ya kufanya kwenye Uwanja wa Ndege wa Sabiha Gökçen

Uwanja wa Ndege wa SAW una maduka mengi yanayofunguliwa kila wakati, kwa hivyo iwe unataka kununua vitu unavyohitaji safarini kabla ya safari au unataka kununulia marafiki na ndugu zako zawadi, kuna chaguo za kutosha. Bidhaa hizi hazitozwi kodi na kuna huduma nyingi. Una ukubwa wa mita 4,500 mraba (fiti 48,400 mraba).

Sebule katika Uwanja wa Ndege wa Istanbul Sabiha Gökçen

Kuna sebule mbalimbali kwenye Uwanja wa Ndege wa SAW, kwenye kumbi zote mbili za Nchini na za kimataifa, zinazokupa nafasi ya kupumzika baada ya shughuli kwenye uwanja wa ndege.

Hoteli karibu na Uwanja wa Ndege wa Sabiha Gökçen

Hoteli moja iko kwenye Uwanja wa Ndege wa Sabiha. Ni chaguo bora kwa yeyote anayesubiri ndege nyingine au anayewasili Istanbul alfajiri. Hoteli hii ina ghorofa 3 na vyumba 128. Inatosha kukidhi mahitaji ya wasafiri na inaweza kufikiwa katika pande zote za uwanja. Katika umbali wa dakika 30 kutoka uwanja wa ndege, wasafiri wanaweza kupata malazi mengi ya bei nafuu na pia hoteli za kifahari. Vyumba vya mikutano pia vinapatikana katika hoteli nyingi. Pia kuna vituo vya biashara, hivyo basi kumwezesha mfanyabiashara aendelee na kazi popote alipo.

Sehemu za kuvutia karibu na Uwanja wa Ndege wa SAW

Ikiwa unasubiri ndege nyingine kwa mrefu katika Uwanja wa Ndege wa Sabiha, una vivutio na maeneo mengi ya kuzuru, haswa ikiwa una muda wa kuelekea katikati mwa mji wa kihistoria wa Istanbul, yakiwemo:

  • The Blue Mosque
  • Mnara wa Galata
  • Grand Bazaar
  • Hagia Sophia
  • Kasri ya Topkapi

Pata maelezo zaidi kuhusu Uwanja wa Ndege wa Istanbul SAWhapa.

Facebook
Instagram
Twitter

This page contains information from third-party websites that are not under the control of Uber and that may be periodically changed or updated. Any information included on this page that is not directly related to Uber or its operations is for informational purposes only and in no way shall be relied upon, or interpreted or construed to create any warranties of any kind, either express or implied, regarding the information contained herein. Certain requirements and features vary by country, region, and city.