Ruka uende katika maudhui ya msingi

Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Philadelphia (PHL)

Tumia Uber kwenda popote, iwe unasafiri kutoka Uwanja wa Ndege wa Philadelphia kwenda Liberty Bell au kutoka Reading Terminal Market hadi PHL.

8000 Essington Avenue, Philadelphia, PA 19153
+1 215-937-6937

Njia bora zaidi ya kusafiri

Itisha usafiri kote ulimwenguni

Bonyeza tu kitufe ili upate usafiri wa angani katika zaidi ya viwanja vikuu 500.

Safiri kama mwenyeji

Acha App na dereva wako ashughulikie masuala ya kina ili usisumbuke kutafuta maelekezo katika jiji ambapo wewe ni mgeni.

Safiri bila wasiwasi kwa kutumia Uber

Pata vipengele unavyovipenda, ikiwa ni pamoja na bei zinazooneshwa moja kwa moja na uwezo wa kulipa bila pesa taslimu, hata ukiwa ugenini.

Punguzo la hadi $15

Pata punguzo la $5 kwenye safari zako tatu za kwanza. Tumia kuponi ya ofa NEWRIDER15. Muda wa kuitumia unakwisha siku 30 baada ya kuweka kuponi ya ofa kwenye akaunti yako ya Uber.

Aina za usafiri ukiwa eneo husika

 • UberX

  1-3

  Affordable everyday trips

 • Comfort

  1-3

  Newer cars with extra legroom

 • UberXL

  1-5

  Affordable rides for groups up to 5

 • Uber Pet

  1-4

  Affordable rides for you and your pet

 • Pool - Unavailable

  1-2

  Temporarily unavailable

1/5

Kupata usafiri kwenye Uwanja wa Ndege wa Philadelphia

Ita gari ukiwa tayari kutoka nje

Chagua aina ya gari linalotosha idadi ya wasafiri na mizigo mliyo nayo.

Ondoka kwenye sehemu ya kuchukua mizigo

Wasafiri wanaoitisha UberX, UberXL au UberPool wanaweza kukutana na madereva wao katika eneo la kuchukuliwa nje ya sehemu ya kuchukua mizigo. Fuata mabango ya Usafiri wa Pamoja.

Kwa wasafiri walioitisha Uber Black au SUV, kutana na dereva wako kwenye Eneo la 6 la kuchukua wasafiri ya limozini. Fuata maelekezo ya Limo.

Kutana na dereva wako

Ikiwa humpati dereva wako, wasiliana naye kupitia programu.

Ada za maegesho katika Uwanja wa Ndege wa Philadelphia

Ikiwa unapanga safari ya kwenda Uwanja wa Ndege wa Philadelphia na unatarajia kuendesha gari, unaweza kupata ada za maegesho hapa.
Ada za maegesho katika Uwanja wa Ndege wa Philadelphia

Ada

$44 kila siku
$24 kila siku
$11 kila siku
Huenda ada za maegesho zikawa zimebadilika; taarifa hii iliwekwa Tarehe 20 Novemba, 2018.

Ramani ya Uwanja wa Ndege wa Philadelphia

Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Philadelphia una jumla ya malango 124, yaliyogawanywa kati ya vituo 7. Vituo vya A Mashariki na A Magharibi hushughulikia safari zote za ndege za kimataifa.

Maswali ambayo wasafiri wanauliza sana

 • Ndiyo. Bonyeza hapa ili uone orodha ya viwanja vya ndege kote duniani unakoweza kuitisha usafiri wa Uber.

 • Nauli ya usafiri wa Uber kuenda (au kutoka) Uwanja wa Ndege wa PHL inategemea hali kama vile aina ya usafiri, kadirio ya umbali na muda wa safari, ada ya vibali barabarani na idadi ya maombi ya usafiri.

  Unaweza kuona kadirio la bei kabla ya kuitisha usafiri kwa kuweka eneo la kuchukuliwa na mahali unakoenda katika zana ya kukadiria nauli katika Uber hapo juu. Kisha, unapoitisha usafiri utaona nauli yako halisi kwenye app kwa kutegemea hali za wakati huo.

 • Maeneo ya kuchukuliwa yanategemea aina ya usafiri unaoitisha na ukubwa wa uwanja wa ndege. Fuata maagizo kwenye App kuhusu eneo utakakomkuta dereva wako. Unaweza pia kuangalia mabango yanayoashiria maeneo ya usafiri wa pamoja yaliyobainishwa kwenye uwanja wa ndege.

  Ikiwa humpati dereva wako, wasiliana naye kupitia programu.

Maelezo zaidi

Unatumia mfumo wa Uber kuendesha gari?

Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kurahisisha huduma unayopokea katika viwanja vya ndege, zikiwemo sheria na kanuni za nchi husika.

Je, unaelekea uwanja tofauti wa ndege?

Unaweza kupelekwa na kuchukuliwa kutoka zaidi ya viwanja 600 vya ndege kote duniani.

Maelezo kwa wageni katika Uwanja wa Ndege wa Philadelphia

Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Philadelphia ndio mkubwa zaidi katika jimbo la Pennsylvania, huku ukiwahudumia takribani watu milioni 30 kila mwaka. Upo umbali wa takribani maili 11 (kilomita 18) kutoka katikati ya jiji la Philadelphia, mwendo wa dakika 17 kwa gari wakati hakuna foleni au vikwazo vingine barabarani.

Vituo katika Uwanja wa Ndege wa Philadelphia

Uwanja wa Ndege wa PHL una majengo 7 ya vituo: Kituo cha A East, Kituo cha A West, Kituo cha B, Kituo cha C, Kituo cha D, Kituo cha E na Kituo cha F, vyote kwa jumla vina malango 124. Kumbi katika Uwanja wa Ndege wa Philadelphia zipo katika vituo mbalimbali katika uwanja wa ndege. Unaweza kupanga safari yako ukitumia taarifa zilizo hapa chini.

Kituo cha A East katika PHL

 • Aer Lingus
 • American
 • American Airlines Admirals Club
 • Ukumbi wa American Express Centurion

Kituo cha A West katika PHL

 • American
 • British Airways
 • Icelandair
 • Lufthansa
 • British Airways Galleries Lounge

Kituo cha B katika PHL

 • American

Kituo cha C katika PHL

 • American

Kituo cha D katika PHL

 • Air Canada
 • Alaska
 • Delta
 • United
 • Delta Sky Club
 • United Club

Kituo cha E katika PHL

 • Frontier
 • JetBlue
 • Kusini magharibi
 • Spirit

Kituo cha F katika PHL

 • American Eagle

Kituo cha kimataifa katika PHL

Ndege za safari za kimataifa katika Uwanja wa Ndege wa Philadelphia zinapatikana katika Kituo cha A East na Kituo cha A West. PHL una safari 36 za moja kwa moja za kimataifa.

Kupata mlo katika Uwanja wa Ndege wa Philadelphia

Kuna zaidi ya maeneo 50 ya kupata chakula yakiwemo baa, maduka ya kahawa na migahawa iliyo na huduma ya kulia mezani katika sehemu mbalimbali za uwanja wa ndege. Kuna ukumbi wa maakuli kati ya Kituo cha B, Kituo cha C na katika Kituo cha F. Wasafiri wanaweza kuchagua maduka ya kahawa na migahawa inayouza vyakula vya kufungashiwa pamoja na migahawa ya kujitegemea katika Uwanja wa Ndege wa Philadelphia inayouza vyakula kama vile mapishi ya Kimediterenia, sushi na vyakula mseto vya kisasa.

Kusafiri katika Uwanja wa ndege wa Philadelphia

Abiria katika Uwanja wa Ndege wa Philadelphia wanaweza kutumia usafiri wa mabasi bila malipo, unaopatikana katika Kituo cha F (Lango la F14) kwenda Lango la C16 (ili kufikia Kituo cha B, C na D) na Lango la A1 (ili kufikia Kituo cha A East na A West).

Mambo ya kufanya katika Uwanja wa Ndege wa Philadelphia

PHL una mradi wa sanaa, unaoonesha kazi za sanaa za wasanii kutoka eneo lote la Philadelphia katika maeneo mbalimbali ya ndege. Vilevile, PHL huandaa tamasha za wanamuziki na watumbuizaji katika ukumbi wa maakuli kati ya Kituo cha B na C, na ukumbi wa maakuli ulio katika Kituo cha F. Kuna sehemu ya watoto kuchezea inayoitwa Ready for Takeoff karibu na Kituo cha A East na ina mfano wa ndege kubwa na mnara wa kuelekeza safari. Uwanja wa Ndege wa Philadelphia una rafu za kuuza majarida na maduka ya nguo za mitindo.

Kubadilisha sarafu katika Uwanja wa Ndege wa Philadelphia

Ofisi za kubadilisha fedha katika Uwanja wa Ndege wa Philadelphia zipo katika maeneo yafuatayo:

 • Kituo cha Wanaowasili kutoka Safari za Kimataifa
 • Kituo cha A East: karibu na Lango la 2
 • Kituo cha A West: karibu na Lango la A14 na karibu na Lango la A18
 • Kituo cha B
 • Kituo cha D: Lango la D7

Hoteli zilizo karibu na Philadelphia

Iwe unasubiri ndege nyingine au ndege imechelewa usiku kucha, au kama unahitaji mahali pa kukaa karibu na PHL, kuna zaidi ya hoteli 25 na maeneo ya kulala karibu.

Sehemu za kuvutia karibu na Uwanja wa Ndege wa Philadelphia

 • Ukumbi wa Independence
 • Bustani ya Kitaifa ya Historia ya Uhuru
 • Liberty Bell
 • Kituo cha Kitaifa cha Katiba

Pata maelezo zaidi kuhusu Uwanja wa Ndege wa Philadelphia hapa.

Facebook
Instagram
Twitter

Ukurasa huu una taarifa kutoka kwenye tovuti za washirika wengine ambazo hazisimamiwi na Uber na zinaweza kugeuzwa au kubadilishwa mara kwa mara. Maelezo yoyote yaliyojumuishwa kwenye ukurasa huu ambayo hayahusiani moja kwa moja na Uber au kazi zake yanatumika kuarifu tu na hayafai kutegemewa, au kuchukuliwa au kufasiliwa kwa namna inayoweka dhamana ya aina yoyote, iwe ya moja kwa moja au inayokisiwa, kuhusu maelezo yaliyo hapa. Baadhi ya masharti na vipengele hutofautiana kutegemea nchi, eneo na jiji. Ofa ya punguzo inawalenga watumiaji wapya pekee. Huwezi kutumia ofa hii pamoja na ofa nyinginezo na haiwezi kutumiwa katika bakshishi. Inapatikana kwa muda mfupi. Vigezo na masharti ya ofa vinaweza kubadilika.