Ruka uende katika maudhui ya msingi

Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa O'Hare (ORD)

Tumia Uber kwenda popote, iwe unasafiri kutoka Uwanja wa Ndege wa O’Hare hadi Navy Pier au kutoka Cloud Gate hadi kwenye uwanja wa ndege.

10000 W. O'Hare Avenue, Chicago, IL 60666
+1 800-832-6352

Njia bora zaidi ya kusafiri

Itisha usafiri kote ulimwenguni

Bonyeza tu kitufe ili upate usafiri wa angani katika zaidi ya viwanja vikuu 500.

Safiri kama mwenyeji

Acha App na dereva wako ashughulikie masuala ya kina ili usisumbuke kutafuta maelekezo katika jiji ambapo wewe ni mgeni.

Safiri bila wasiwasi kwa kutumia Uber

Pata vipengele unavyovipenda, ikiwa ni pamoja na bei zinazooneshwa moja kwa moja na uwezo wa kulipa bila pesa taslimu, hata ukiwa ugenini.

Punguzo la hadi $15

Pata punguzo la $5 kwenye safari zako tatu za kwanza. Tumia kuponi ya ofa NEWRIDER15. Muda wa kuitumia unakwisha siku 30 baada ya kuweka kuponi ya ofa kwenye akaunti yako ya Uber.

Aina za usafiri ukiwa eneo husika

 • UberX

  1-3

  Affordable rides, all to yourself

 • Comfort

  1-3

  Newer cars with extra legroom

 • UberXL

  1-5

  Affordable rides for groups up to 5

 • Uber Green

  1-3

  Low-emission rides

 • Connect

  1-4

  Send packages to friends & family

 • UberCab

  1-4

  Local taxi-cabs at the tap of a button

 • Pool - Unavailable

  1-2

  Temporarily unavailable

1/7

Kupata gari kwenye Uwanja wa Ndege wa O'Hare

Chagua jinsi ungependa gari lako kuwa

Fuata maelekezo kwenye programu baada ya kuchagua bidhaa inayokufaa zaidi.

Ondoka kupitia ghorofa inayofaa

Katika maombi mengi ya usafiri, utamkuta dereva wako kwenye ghorofa ya juu katika kituo cha Wanaoondoka.

Kwa wasafiri wanaoitisha usafiri wa UberBLACK au SUV na walio kwenye Kituo cha Kimataifa, tafadhali kutana na dereva wako kwenye ghorofa ya chini katika kituo cha Wanaowasili.

Thibitisha eneo utakakochukuliwa

Ikiwa humpati dereva wako, wasiliana naye kwenye programu ya Uber.

Ada za maegesho katika Uwanja wa Ndege wa ORD

Ikiwa unapanga safari ya kwenda Uwanja wa Ndege wa ORD na unatarajia kuendesha gari, unaweza kupata ada za maegesho hapa.
Ada za maegesho katika Uwanja wa Ndege wa ORD

Ada

$74 kila siku
$74 kila siku
$61 kila siku
$40 kila siku
$17 kila siku
$17 kila siku
$10 kila siku
Huenda ada za maegesho zikawa zimebadilika; taarifa hii iliwekwa Tarehe 20 Novemba, 2018.

Ramani ya Uwanja wa Ndege wa ORD

Uwanja wa Ndege wa ORD una vituo 4 vya wasafiri—Vituo vya 1, 2, 3 na 5—vilivyo na jumla ya malango 191. Kituo cha 5 kinashughulikia wanaowasili kutoka mataifa mengine.

Maswali ambayo wasafiri wanauliza sana

 • Ndiyo. Bonyeza hapa ili uone orodha ya viwanja vya ndege kote duniani unakoweza kuitisha usafiri wa Uber.

 • Nauli ya usafiri wa Uber kuenda (au kutoka) ORD inategemea hali kama vile aina ya usafiri, kadirio ya umbali na muda wa safari, ada ya vibali barabarani na idadi maombi ya usafiri.

  Unaweza kuona kadirio la bei kabla ya kuitisha usafiri kwa kuweka eneo la kuchukuliwa na mahali unakoenda katika zana ya kukadiria nauli katika Uber hapo juu. Kisha, unapoitisha usafiri utaona nauli yako halisi kwenye app kwa kutegemea hali za wakati huo.

 • Maeneo ya kuchukuliwa yanategemea aina ya usafiri unaoitisha na ukubwa wa uwanja wa ndege. Fuata maagizo kwenye App kuhusu eneo utakakomkuta dereva wako. Unaweza pia kuangalia mabango yanayoashiria maeneo ya usafiri wa pamoja yaliyobainishwa kwenye uwanja wa ndege.

  Ikiwa humpati dereva wako, wasiliana naye kupitia programu.

 • Hapo awali Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa O’Hare Chicago ulikuwa kiwanda cha ndege kilichoitwa Orchard Place, hii ndiyo asili ya jina fupi la uwanja huo, ORD.

Maelezo zaidi

Unatumia mfumo wa Uber kuendesha gari?

Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kurahisisha huduma unayopokea katika viwanja vya ndege, zikiwemo sheria na kanuni za nchi husika.

Je, unaelekea uwanja tofauti wa ndege?

Unaweza kupelekwa na kuchukuliwa kutoka zaidi ya viwanja 600 vya ndege kote duniani.

Maelezo kwa wageni kwenye Uwanja wa Ndege wa O’Hare

Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa O’Hare (ORD) ndio uwanja wa ndege wa 6 wenye shughuli nyingi duniani, unawahudumia zaidi ya abiria milioni 80 kila mwaka. O’Hare upo maili 16 (kilomita 26)—mwendo wa dakika 35 kwa gari wakati hakuna foleni au vikwazo vingine barabarani—kutoka katikati ya jiji la Chicago na fukwe za Ziwa Michigan.

Vituo katika Uwanja wa Ndege wa ORD

ORD ina vituo 4: Kituo cha 1, Kituo cha 2, Kituo cha 3 na Kituo cha 5, zote zikiwa na jumla ya malango 191 katika uwanja wote wa ndege. Kumbi za Uwanja wa Ndege wa Chicago zimetapakaa katika vituo vyote. Unaweza kupanga safari yako ukitumia taarifa zilizo hapa chini.

Kituo cha 1 ORD

 • All Nippon
 • Ethiopian
 • Lufthansa
 • United
 • United Club
 • Ukumbi wa United Polaris

Kituo cha 2 katika ORD

 • Air Canada
 • Delta
 • Delta Sky Club
 • United Club

Kituo cha 3 katika ORD

 • Air Choice One
 • Alaska
 • American
 • Cape Air
 • Iberian
 • Japan
 • JetBlue
 • Spirit
 • American Airlines Admirals Club
 • Ukumbi wa American Airlines Flagship

Kituo cha 5 katika ORD

 • Aer Lingus
 • Aeroméxico
 • Air France
 • Air India
 • Air New Zealand
 • Alitalia
 • All Nippon
 • Asiana
 • Austrian
 • Avianca
 • British Airways
 • Cathay Pacific
 • Cayman
 • China Eastern
 • Copa
 • Emirates
 • Etihad
 • EVA Air
 • Finnair
 • Frontier
 • Hainan
 • Icelandair
 • Interjet
 • KLM Royal Dutch
 • Korean Air
 • LOT Polish
 • Norwegian
 • Qatar
 • Royal Jordanian
 • Scandinavian
 • Spirit
 • SWISS
 • Turkish
 • Volaris
 • WestJet
 • WOW
 • Air France–KLM Lounge
 • Ukumbi wa British Airways First
 • Ukumbi wa British Airways Terraces
 • Ukumbi wa SAS
 • Ukumbi wa SWISS
 • Ukumbi wa Swissport

Kituo cha kimataifa katika ORD

Kuabiri na kuwasili kutoka safari za kimataifa katika Uwanja wa Ndege wa O’Hare aghalabu hufanyika katika Kituo cha 5, hata hivyo kuna baadhi ya safari za kimataifa ambazo hutokea Kituo cha 1 na cha 3. O’Hare una safari za moja kwa moja kuelekea maeneo 63 ya kimataifa.

Kupata mlo katika Uwanja wa Ndege wa ORD

Kuna zaidi ya maeneo 135 ya kupata chakula katika Uwanja wa Ndege wa Chicago, ikiwemo maduka ya kahawa, baa, migahawa inayouza vyakula vya kufungashiwa na iliyo na huduma ya kulia mezani. Hizi zote zinapatikana katika maeneo mbalimbali ya uwanja wa ndege. Wasafiri wanaweza kupata aina mbalimbali ya vyakula katika ORD vikiwemo sushi, mapishi ya kimediterenia, vitobosha, bisi, vyakula vya mtindo wa California, piza ya mseto wa kisasa na zaidi.

Kusafiri kwenye Uwanja wa Ndege wa ORD

Wasafiri wanaweza kutumia mfumo wa usafiri katika Uwanja wa Ndege wa Chicago unaoitwa Airport Transit System (ATS), kutoka eneo moja kwenda kwingine. Mfumo huu wa kiotomatiki wa kusafirisha watu unakwenda umbali wa maili 2.5 (kilomita 4) na hufanyakazi saa 24 kwa siku, huku ukiunganisha vituo vyote 4 na maegesho yaliyo nje. Stesheni zimeandikwa waziwazi katika kila kituo.

Mambo ya kufanya kwenye Uwanja wa Ndege wa ORD

Uwanja wa ndege wa Chicago ni makao ya vivutio mbalimbali, ukiwemo mradi wa umma wa sanaa unaoonesha vinyago, michoro na mapambo ya ukuta, na maonesho yako katika maeneo mbalimbali ya uwanja wa ndege. Umbo la gofu la dinosau wa aina ya Brachiosaurus lenye urefu wa futi 72 (mita 22), ambalo limeletwa kwa mkopo kutoka Makumbusho ya Chicago Field, lipo katika daraja la juu la Kituo cha 1 katika Ukumbi wa B. Kuna chumba cha yoga kilicho na sakafu iliyoundwa kutokana na mbao ya mwanzi uliokuzwa kwa mbinu endelevu, chumba kina vioo kwenye dari na upande mmoja wa ukuta pamoja na mikeka ya mazoezi, kinapatikana katika Kituo cha 3 karibu na Urban Garden. Maduka katika Uwanja wa Ndege wa Chicago yana rafu za majarida na maduka yanayouza nguo za mitindo ya juu.

Kubadilisha sarafu katika Uwanja wa Ndege wa ORD

Ofisi za kubadilisha sarafu katika uwanja wa ndege wa O’Hare zipo katika maeneo yafuatayo:

 • Kituo cha 1: Malango ya B9 na C18
 • Kituo cha 2: ukumbi mkuu
 • Kituo cha 3: Lango la K11
 • Kituo cha 5: madaraja ya juu na chini

Hoteli zilizo karibu na Uwanja wa Ndege wa ORD

Iwe unasubiri ndege nyingine au ndege imechelewa usiku kucha, au kama unahitaji mahali pa kukaa karibu na ORD, kuna zaidi ya hoteli 30 na maeneo ya kulala karibu, pamoja na hoteli nyingine unazoweza kuchagua ndani na karibu na katikati ya jiji la Chicago.

Maeneo ya kuzuru karibu na Uwanja wa Ndege wa ORD

 • Tangi la samaki la Chicago
 • Makumbusho ya sanaa Chicago
 • The Magnificent Mile
 • Navy Pier
 • Willis Tower

Pata maelezo zaidi kuhusu Uwanja wa Ndege wa ORDhapa.

Facebook
Instagram
Twitter

Ukurasa huu una taarifa kutoka kwenye tovuti za washirika wengine ambazo hazisimamiwi na Uber na zinaweza kugeuzwa au kubadilishwa mara kwa mara. Maelezo yoyote yaliyojumuishwa kwenye ukurasa huu ambayo hayahusiani moja kwa moja na Uber au kazi zake yanatumika kuarifu tu na hayafai kutegemewa, au kuchukuliwa au kufasiliwa kwa namna inayoweka dhamana ya aina yoyote, iwe ya moja kwa moja au inayokisiwa, kuhusu maelezo yaliyo hapa. Baadhi ya masharti na vipengele hutofautiana kutegemea nchi, eneo na jiji. Ofa ya punguzo inawalenga watumiaji wapya pekee. Huwezi kutumia ofa hii pamoja na ofa nyinginezo na haiwezi kutumiwa katika bakshishi. Inapatikana kwa muda mfupi. Vigezo na masharti ya ofa vinaweza kubadilika.