Ruka uende katika maudhui ya msingi

Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Miami (MIA)

Tutumia Uber kusafiri popote, iwe unasafiri kutoka Uwanja wa Ndege wa Miami hadi South Beach au kutoka Ocean Drive hadi MIA.

2100 NW 42nd Avenue, Miami, FL 33126
+1 305-876-7000

Njia bora zaidi ya kusafiri

Itisha usafiri kote ulimwenguni

Bonyeza tu kitufe ili upate usafiri wa angani katika zaidi ya viwanja vikuu 500.

Safiri kama mwenyeji

Acha App na dereva wako ashughulikie masuala ya kina ili usisumbuke kutafuta maelekezo katika jiji ambapo wewe ni mgeni.

Safiri bila wasiwasi kwa kutumia Uber

Pata vipengele unavyovipenda, ikiwa ni pamoja na bei zinazooneshwa moja kwa moja na uwezo wa kulipa bila pesa taslimu, hata ukiwa ugenini.

Punguzo la hadi $15

Pata punguzo la $5 kwenye safari zako tatu za kwanza. Tumia kuponi ya ofa NEWRIDER15. Muda wa kuitumia unakwisha siku 30 baada ya kuweka kuponi ya ofa kwenye akaunti yako ya Uber.

Aina za usafiri ukiwa eneo husika

 • UberX

  1-3

  Affordable rides, all to yourself

 • Comfort

  1-3

  Newer cars with extra legroom

 • UberXL

  1-5

  Affordable rides for groups up to 5

 • Uber Green

  1-3

  Low-emission rides

 • Connect

  1-4

  Send packages to friends & family

 • Pool - Unavailable

  1-2

  Temporarily unavailable

1/6

Kupata gari kwenye Uwanja wa Ndege wa Miami

Ita gari ukiwa tayari kutoka nje

Na uchague gari linalotoshea wasafiri na mizigo mliyo nayo.

Ondoka kupitia ghorofa ya chini ya wanaowasili.

Thibitisha kituo na eneo la malango wako kwenye programu, kisha uondoke nje ya sehemu ya kuchukua mizigo na uvuke hadi kwenye sehemu ya katikati, kando ya barabara.

Kutana na dereva wako sehemu ya katikati, kando ya barabara

Thibitisha kuwa dereva wako ni yule aliye kwenye programu. Ikiwa humpati dereva wako, wasiliana naye kwenye programu.

Ada za maegesho katika Uwanja wa Ndege wa Miami

Ikiwa unapanga safari ya kwenda Uwanja wa Ndege wa Miami na unatarajia kuendesha gari, unaweza kupata ada za maegesho hapa.
Ada za maegesho katika Uwanja wa Ndege wa Miami

Ada

$30 kila siku
$17 kila siku
Huenda ada za maegesho zikawa zimebadilika; taarifa hii iliwekwa Tarehe 20 Novemba, 2018.

Ramani ya Uwanja wa Ndege wa Miami

Uwanja wa Ndege wa Miami una malango 131 yaliyosambaa katika vituo 6. Takribani vituo vyote vinaweza kuwashughulikia wasafiri wanaowasili kutoka safari za kimataifa isipokuwa Kituo cha G.

Maswali ambayo wasafiri wanauliza sana

 • Ndiyo. Bonyeza hapa ili uone orodha ya viwanja vya ndege kote duniani unakoweza kuitisha usafiri wa Uber.

 • Nauli ya usafiri wa Uber kuenda (au kutoka) Uwanja wa Ndege wa MIA inategemea hali kama vile aina ya usafiri, kadirio ya umbali na muda wa safari, ada ya vibali barabarani na idadi ya maombi ya usafiri.

  Unaweza kuona kadirio la bei kabla ya kuitisha usafiri kwa kuweka eneo la kuchukuliwa na mahali unakoenda katika zana ya kukadiria nauli katika Uber hapo juu. Kisha, unapoitisha usafiri utaona nauli yako halisi kwenye app kwa kutegemea hali za wakati huo.

 • Maeneo ya kuchukuliwa yanategemea aina ya usafiri unaoitisha na ukubwa wa uwanja wa ndege. Fuata maagizo kwenye App kuhusu eneo utakakomkuta dereva wako. Unaweza pia kuangalia mabango yanayoashiria maeneo ya usafiri wa pamoja yaliyobainishwa kwenye uwanja wa ndege.

  Ikiwa humpati dereva wako, wasiliana naye kupitia programu.

Maelezo zaidi

Unatumia mfumo wa Uber kuendesha gari?

Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kurahisisha huduma unayopokea katika viwanja vya ndege, zikiwemo sheria na kanuni za nchi husika.

Je, unaelekea uwanja tofauti wa ndege?

Unaweza kupelekwa na kuchukuliwa kutoka zaidi ya viwanja 600 vya ndege kote duniani.

Maelezo kwa wageni kwenye Uwanja wa Ndege wa Miami

Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Miami (MIA) ndio wa 12 kwa shughuli nyingi zaidi nchini Marekani kulingana na idadi ya abiria, unawahudumia zaidi ya wasafiri milioni 44 kila mwaka. Uwanja upo maili 8 (kilomita 13) kutoka katikati ya jiji la Miami, mwendo wa dakika 25 kwa gari wakati hakuna foleni au vikwazo vingine barabarani.

Vituo katika Uwanja wa Ndege wa Miami

Uwanja wa Ndege wa MIA una vituo 3: Kituo cha Kaskazini, Kituo cha Kati na Kituo cha Kusini Kila kituo kina kumbi zilizo na malango ya kuabiri. Kumbi katika Uwanja wa Ndege wa Miami zipo katika vituo mbalimbali. Unaweza kupanga safari yako ukitumia taarifa zilizo hapa chini.

Kituo cha Kaskazini katika MIA North (Ukumbi wa D)

 • American
 • British Airways
 • Centurion Lounge
 • American Airlines Admirals Club

Kituo cha Kati katika MIA (Kumbi za E, F, na G)

 • Aer Lingus
 • Aeroflot
 • Air Europa
 • Air Italy
 • Aruba
 • Avior
 • BoA
 • Cayman
 • Finnair
 • Flair
 • Frontier
 • Iberia
 • Interjet
 • Qatar
 • Sun Country
 • Surinam Airways
 • Swift Air
 • TAP Air Portugal
 • TUI fly
 • United
 • Volaris
 • WestJet
 • World Atlantic
 • XL Airways France
 • Club America

Kituo cha Kusini katika MIA (Kumbi za H na J)

 • Aerolíneas Argentinas
 • Aeroméxico
 • Air Canada
 • Air France
 • Alitalia
 • Austrian
 • Avianca
 • Bahamasair
 • Caribbean Airlines
 • Copa
 • Delta
 • El Al
 • GOL
 • KLM
 • LATAM
 • Lufthansa
 • Miami Air
 • SAS
 • Sunwing
 • SWISS
 • Turkish
 • Virgin Atlantic
 • Viva Air
 • Avianca VIP Lounge
 • Delta Sky Club
 • VIP Lounge Miami

Kituo cha Kimataifa katika MIA

Safari za ndege za kimataifa katika Uwanja wa Ndege wa Miami hutokea katika vituo vyote 3. Uwanja wa Ndege wa MIA husafiri moja kwa moja kuelekea maeneo 107 ya kimataifa.

Kupata mlo katika Uwanja wa Ndege wa Miami

Kuna zaidi ya maeneo 130 ya kupata vinywaji na vyakula katika Uwanja wa Miami yanayopatikana katika vituo na kumbi zote za MIA. Kuna migahawa inayouza vyakula vya kufungashiwa na inayouza vyakula vya mapishi ya kimataifa, hivyo, wasafiri wanaweza kuchagua watakacho. Pia kuna migahawa iliyo na chaguo la kulia mezani katika maeneo mbalimbali ya vituo.

Kusafiri kwenye Uwanja wa Ndege wa Miami

Mfumo wa kiotomatiki wa kusafirisha watu unaoitwa MIA Mover, hufanya shughuli ya uchukuzi wa wasafiri katika Uwanja wa Ndege wa Miami na kuwapeleka abiria kutoka jengo la kituo kikuu cha Uwanja wa Ndege wa Miami na Kituo cha Kukutanisha Njia za Usafiri Miami (MIC). MIA Mover ni mojawapo ya mifumo ya usafiri katika Uwanja wa Ndege wa Miami. Mfumo mwingine ni Skytrain ambao hufanya kazi katika Ukumbi wa D.

Mambo ya kufanya kwenye Uwanja wa Ndege wa Miami

Uwanja wa Ndege wa Miami una sehemu kadhaa za kuhifadhi na kuonesha sanaa katika vituo vya uwanja wa ndege, ikiwa ni pamoja na maonesho na matunzio kadhaa ya sanaa. Uwanja wa ndege pia una sehemu inayosisimua ya watoto kuchezea inayoitwa Plane Fun, katika Ukumbi wa E karibu na Lango E5, inaweza kufikika kutoka Ukumbi wa D. Kwa watu wazima, kuna spaa zilizo katika daraja la 2 kusini mwa Kituo cha H na katika daraja la 2 kusini wa Kituo cha J, zinazotoa huduma za mapambo ya makucha, uso na kusingwa.

Kubadilisha sarafu katika Uwanja wa Ndege wa Miami

Ofisi za kubadilisha fedha katika Uwanja wa Ndege wa Miami zinapatikana katika Ukumbi wa D (Mashariki), Ukumbi wa E, Ukumbi wa F, Ukumbi wa G na Ukumbi wa H.

Hoteli karibu na Uwanja wa Ndege wa Miami

Iwe unasubiri ndege nyingine au ndege imechelewa usiku kucha, au kama unahitaji mahali pa kukaa karibu na MIA, kuna zaidi ya hoteli 40 na maeneo ya kulala karibu.

Maeneo ya kuzuru karibu na Uwanja wa Ndege wa Miami

 • Collins Avenue
 • Key Biscayne
 • Miami Design District
 • South Beach
 • South Pointe Pier
 • Virginia Key

Pata maelezo zaidi kuhusu Uwanja wa Ndege wa Miamihapa.

Facebook
Instagram
Twitter

Ukurasa huu una taarifa kutoka kwenye tovuti za washirika wengine ambazo hazisimamiwi na Uber na zinaweza kugeuzwa au kubadilishwa mara kwa mara. Maelezo yoyote yaliyojumuishwa kwenye ukurasa huu ambayo hayahusiani moja kwa moja na Uber au kazi zake yanatumika kuarifu tu na hayafai kutegemewa, au kuchukuliwa au kufasiliwa kwa namna inayoweka dhamana ya aina yoyote, iwe ya moja kwa moja au inayokisiwa, kuhusu maelezo yaliyo hapa. Baadhi ya masharti na vipengele hutofautiana kutegemea nchi, eneo na jiji. Ofa ya punguzo inawalenga watumiaji wapya pekee. Huwezi kutumia ofa hii pamoja na ofa nyinginezo na haiwezi kutumiwa katika bakshishi. Inapatikana kwa muda mfupi. Vigezo na masharti ya ofa vinaweza kubadilika.