Ruka uende katika maudhui ya msingi
Uber
Uber

Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Orlando (MCO)

Tumia Uber kwenda popote, iwe unasafiri kutoka Uwanja wa Ndege wa Orlando kwenda kwenye bustani ya burudani au kutoka International Drive hadi kwenye uwanja wa ndege.

1 Jeff Fuqua Boulevard, Orlando, FL 32827
+1 407-825-2001

Njia bora zaidi ya kusafiri

Itisha usafiri kote ulimwenguni

Bonyeza tu kitufe ili upate usafiri wa angani katika zaidi ya viwanja vikuu 500.

Safiri kama mwenyeji

Acha App na dereva wako ashughulikie masuala ya kina ili usisumbuke kutafuta maelekezo katika jiji ambapo wewe ni mgeni.

Safiri bila wasiwasi kwa kutumia Uber

Pata vipengele unavyovipenda, ikiwa ni pamoja na bei zinazooneshwa moja kwa moja na uwezo wa kulipa bila pesa taslimu, hata ukiwa ugenini.

Mfumo wa Uber wa kukadiria nauli

Sampuli za bei za msafiri ni makadirio tu na hazioneshi mabadiliko yanayotokana na mapunguzo, kucheleweshwa kwenye foleni na mambo mengine. Tunaweza kutumia nauli isiyobadilika na bei za chini zaidi. Bei halisi zinaweza kubadilika.

Njia za kusafiri

 • UberX1-4

  Affordable, everyday rides

 • UberXL1-6

  Affordable rides for groups up to 6

 • Black1-4

  Luxury rides with professional drivers

Kupata gari kwenye Uwanja wa Ndege wa Orlando

Itisha usafiri ukiwa tayari kutoka nje.

Baada ya kuchukua mizigo yako, chagua aina ya gari linaloweza kuwabeba nyote, kulingana na bei na nafasi unayotaka ya mizigo.

Ondoka kupitia ghorofa ya wanaowasili

Ondoka katika Daraja la 2—sehemu ya Wanaowasili, kisha umsubiri dereva kando ya barabara.

Kutana na dereva wako kando ya barabara

Hakikisha kila wakati kwamba namba pleti ya gari inalingana na ile unayoona kwenye programu. Ikiwa humpati dereva wako, wasiliana naye kupitia programu.

Ada za maegesho katika Uwanja wa Ndege wa Orlando

Ikiwa unapanga safari ya kwenda Uwanja wa Ndege wa Orlando na unatarajia kuendesha gari, unaweza kupata ada za maegesho hapa.

Aina ya maegesho

Mhudumu wa Kuegesha

Maegesho ya Kituo cha Juu

Majumba ya Maegesho ya A na B

Garage C

Ada

$28.76 per day
$19 kila siku
$19 kila siku
$17 kila siku
Huenda ada za maegesho zikawa zimebadilika; taarifa hii iliwekwa Tarehe 20 Novemba, 2018.

Ramani ya Uwanja wa Ndege wa Orlando

Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Orlando una vituo viwili: Kituo cha A na Kituo cha B. Vituo hivi 2 vina kumbi 4 za kando ya uwanja zilizo na malango 129.

Maswali ambayo wasafiri wanauliza sana

Ndiyo. Bonyeza hapa ili uone orodha ya viwanja vya ndege kote duniani unakoweza kuitisha usafiri wa Uber.

Nauli ya usafiri wa Uber kuenda (au kutoka) Uwanja wa Ndege wa MCO inategemea hali kama vile aina ya usafiri, kadirio ya umbali na muda wa safari, ada ya vibali barabarani na idadi ya maombi ya usafiri.

Unaweza kuona kadirio la bei kabla ya kuitisha usafiri kwa kuweka eneo la kuchukuliwa na mahali unakoenda katika zana ya kukadiria nauli katika Uber hapo juu. Kisha, unapoitisha usafiri utaona nauli yako halisi kwenye programu kwa kutegemea hali za wakati huo.

Maeneo ya kuchukuliwa yanategemea aina ya usafiri unaoitisha na ukubwa wa uwanja wa ndege. Fuata maagizo kwenye programu kuhusu eneo utakakomkuta dereva wako. Unaweza pia kuangalia mabango yanayoashiria maeneo ya usafiri wa pamoja yaliyobainishwa kwenye uwanja wa ndege.

Ikiwa humpati dereva wako, wasiliana naye kupitia programu.

Msimbo wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Orlando MCO unatokana na jina la awali, McCoy Air Force Base. Ingawa wenyeji wengi hivi leo wanasema kuwa MCO inasimamia Mickey’s Corporate Office.

Maelezo zaidi

Unatumia mfumo wa Uber kuendesha gari?

Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kurahisisha huduma unayopokea katika viwanja vya ndege, zikiwemo sheria na kanuni za nchi husika.

Je, unaelekea uwanja tofauti wa ndege?

Unaweza kupelekwa na kuchukuliwa kutoka zaidi ya viwanja 500 vya ndege kote duniani.

Maelezo kwa wageni kwenye Uwanja wa Ndege wa Orlando

Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Orlando (MCO) ndio uwanja wa ndege wa 11 kwa shughuli nyingi zaidi nchini Marekani, huku ukiwahudumia zaidi ya wasafiri milioni 44 kila mwaka. Uwanja upo maili 6 (kilomita 10 ) kutoka katikati ya jiji la Orlando, ni mwendo wa dakika 20 hivi kwa gari wakati hakuna foleni au vikwazo vingine barabarani.

Vituo katika Uwanja wa Ndege wa Orlando

Uwanja wa Ndege wa Orlando una jengo moja kuu lililogawanywa kuwa vituo 2: Kituo cha A na Kituo cha B. Vituo vyote viwili vya Uwanja wa Ndege wa Orlando hushughulikia safari za kimataifa, na kuna malango 129 katika vituo hivyo 2. Kumbi za Uwanja wa Ndege wa Orlando zinapatikana katika vituo vyote viwili. Unaweza kupanga safari yako ukitumia taarifa zilizo hapa chini.

Kituo cha A katika MCO

 • Aeroméxico
 • Alaska
 • Avianca
 • Azul
 • Copa
 • Frontier
 • JetBlue
 • Magnicharters
 • Miami Air International
 • Silver
 • Kusini magharibi
 • World Atlantic
 • Ukumbi wa USO

Kituo cha B katika MCO

 • Aer Lingus
 • Air Canada
 • Air Canada Rouge
 • Air Transat
 • American
 • Bahamasair
 • British Airways
 • Caribbean
 • Delta
 • Edelweiss
 • Emirates
 • Eurowings
 • Icelandair
 • LATAM
 • Lufthansa
 • Norwegian Long Haul
 • Spirit
 • Sun Country
 • Sunwing
 • Thomas Cook
 • United
 • Virgin Atlantic
 • Volaris
 • WestJet
 • American Airlines Admirals Club
 • Delta Sky Club
 • The Club at MCO
 • United Club

Kituo cha Kimataifa cha uwanja wa ndege wa MCO

Safari za kimataifa kutoka Uwanja wa Ndege wa Orlando hutoka katika Kituo cha A na Kituo cha B. MCO una usafiri wa moja kwa moja wa kuelekea maeneo 61 ya kimataifa.

Kupata mlo katika Uwanja wa Ndege wa Orlando

Kuna zaidi ya maeneo 60 za kupata mlo katika Uwanja wa Ndege wa Orlando, yakiwemo yanayouza vyakula vya kufungashiwa, maduka ya kahawa na migahawa. Wasafiri wanaweza kununua vinywaji na vyakula katika vituo vyote viwili. Ukumbi mkuu wa maakuli katika Uwanja wa Ndege wa Orlando upo katika jumba kuu la kituo. Maeneo ya kula yanaweza kupatikana karibu na malango yote.

Kusafiri katika Uwanja wa Ndege wa Orlando

Wasafiri katika MCO wanaweza kutumia mfumo wa kiotomatiki wa kusafirisha watu (APM) kutoka katika jengo kuu la kituo hadi katika kumbi za upande wa kuabiri ndege. APM hufanya kazi katika mfumo wa kupandisha na kushusha, na abiria wanaweza kuipanda baada ya ukaguzi wa usalama. Vilevile, usafiri katika Uwanja wa Ndege wa Orlando hutolewa kupitia kambarau, eskaleta na mikanda ya kutembelea inayojivuta, ili kupunguza umbali wa kutembea katika uwanja wa ndege.

Mambo ya kufanya kwenye Uwanja wa Ndege wa Orlando

Uwanja wa Ndege wa MCO una sehemu ya kudumu ya sanaa inayoangazia mitindo na maudhui mbalimbali. Sanaa hizo zinapatikana katika vituo vyote na kwenye ukumbi upande wa kuabiri ndege. Uwanja wa ndege wa MCO una maduka kadhaa yakiwemo ya rafu za majarida na maduka yanayouza nguzo za mitindo ya juu. Kuna spaa katika maeneo 5 kwenye uwanja wote wa ndege.

Kubadilisha sarafu katika Uwanja wa Ndege wa Orlando

Ofisi za kubadilisha fedha katika Uwanja wa Ndege wa Orlando zinapatikana katika Kituo Kikuu (kumbi za Mashariki na Magharibi) na Upande wa Kuabiri Ndege 4 (Malango ya 70 hadi 99).

Hoteli zilizo karibu na Uwanja wa Ndege wa Orlando

Iwe unasubiri ndege nyingine au ndege imechelewa usiku kucha, au kama unahitaji mahali pa kukaa karibu na MCO, kuna zaidi ya hoteli 24 na maeneo ya kukaa karibu.

Maeneo ya kuzuru karibu na Uwanja wa Ndege wa Orlando

 • The Florida Mall
 • ICON Orlando
 • Lake Nona Medical City
 • Jumba la makumbusho ya Orlando
 • Bustani la maonyesho na burudani Orlando

Pata maelezo zaidi kuhusu Uwanja wa Ndege wa Orlando hapa.

Facebook
Instagram
Twitter