Ruka uende katika maudhui ya msingi

Uwanja wa Ndege wa Heathrow (LHR)

Iwe unasafiri kuelekea London kutoka Uwanja wa Ndege wa Heathrow au kutoka London kuelekea Uwanja wa Ndege wa Heathrow, iamini Uber kukufikisha unakoenda.

Longford TW6, United Kingdom
+44 20-7360-1250

Njia bora zaidi ya kusafiri

Itisha usafiri kote ulimwenguni

Bonyeza tu kitufe ili upate usafiri wa angani katika zaidi ya viwanja vikuu 500.

Safiri kama mwenyeji

Acha App na dereva wako ashughulikie masuala ya kina ili usisumbuke kutafuta maelekezo katika jiji ambapo wewe ni mgeni.

Safiri bila wasiwasi kwa kutumia Uber

Pata vipengele unavyovipenda, ikiwa ni pamoja na bei zinazooneshwa moja kwa moja na uwezo wa kulipa bila pesa taslimu, hata ukiwa ugenini.

Aina za usafiri ukiwa eneo husika

 • UberX

  1-3

  Affordable rides, all to yourself

 • Green

  1-3

  Sustainable trips in electric vehicles

 • Comfort

  1-3

  New, spacious cars and top-rated drivers

 • Exec

  1-3

  Premium rides in high-end cars

 • UberXL

  1-5

  Affordable rides for groups up to 5

 • Lux

  1-3

  Ultimate luxury & style

1/6

Jinsi ya kupata usafiri wa Uber kutoka uwanja wa ndege

Fungua App yako ili uitishe usafiri

Ukiwa tayari kutoka nje, fungua programu yako kisha uitishe usafiri. Chagua usafiri unaotoshea idadi ya wasafiri na mizigo mliyo nayo.

Fuata maelekezo katika App

Utapata maelekezo kuhusu eneo la kuchukua wasafiri moja kwa moja katika programu. Pia kunaweza kuwa na alama katika uwanja wa ndege.

Kutana na dereva wako

Nenda katika eneo la kuchukuliwa jinsi ilivyobainishwa katika App. Tafadhali kumbuka, eneo hilo huenda halitakuwa karibu kabisa na lango unaloondokea. Ikiwa humpati dereva wako, wasiliana naye kupitia App.

Vidokezo vya kuzingatia katika Uwanja wa Ndege wa Heathrow

WiFi katika Uwanja wa Ndege wa Heathrow

Kuna WiFi bila malipo katika Uwanja wa Ndege wa Heathrow—chagua tu mtandao wa WiFi wa Heathrow kisha ufuate maelekezo kwenye skrini. Pia unaweza kupata mtandao wenye kasi zaidi kwa kutumia kifurushi cha kulipia kiasi unachotumia.

Maegesho katika Uwanja wa Ndege wa Heathrow

Heathrow ina aina nyingi za maegesho, yakiwemo maegesho ya muda mfupi, maegesho ya muda mrefu, maegesho ya daraja la biashara na ya Pod. Pia kuna maegesho ya kuchukua na kushukisha wasafiri kwa haraka na huduma ya kuwaachia wahudumu magari ili wayaegeshe.

Kuweka mizigo katika Uwanja wa Ndege wa Heathrow

Huduma ya kuhifadhi mizigo inapatikana katika kila kituo cha Uwanja wa Ndege wa Heathrow. Ada zinategemea muda unaotaka kuhifadhi mzigo wako. Unaweza kuhifadhi mizigo yako kwa hadi siku 90.

Maswali ambayo wasafiri wanauliza sana

 • Uber inapatikana katika Uwanja wa Ndege wa Heathrow, kwa hivyo unaweza kufurahia usafiri wa starehe na uhakika popote unapotaka kwenda.

 • Ili kupata eneo la kuchukuliwa, angalia programu ya Uber baada ya kuitisha usafiri.

 • Hata kama safari si ndefu sana, ada za Uber kutoka na kwenda Uwanja wa Ndege wa Heathrow zinaweza kuathiriwa na muda, foleni na masuala mengine. Ada za uwanja wa ndege na maegesho pia zinaweza kuongezwa kwenye nauli yako kamili ya safari.

 • Muda wa kuchukuliwa unaweza kuwa tofauti kulingana na wakati, idadi ya madereva wanaopatikana na masuala mengine. Mara baada ya kuitisha usafiri, angalia programu ili uone kadirio la muda wa kusubiri.

Maelezo zaidi

Unatumia mfumo wa Uber kuendesha gari?

Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kurahisisha huduma unayopokea katika viwanja vya ndege, zikiwemo sheria na kanuni za nchi husika.

Je, unaelekea uwanja tofauti wa ndege?

Unaweza kupelekwa na kuchukuliwa kutoka zaidi ya viwanja 600 vya ndege kote duniani.

Vituo katika Uwanja wa Ndege wa London Heathrow: taarifa kwa wageni

Uber ni chaguo bora kwa wasafiri wanaowasili au kuondoka kwenye Uwanja wa Ndege wa London Heathrow. Uwanja wa Ndege wa London Heathrow ni wa pili wenye shughuli nyingi kote ulimwengu. Unahudumia eneo pana la London na pia kusini mwa Uingereza. Uwanja wa Ndege wa Heathrow unapatikana takribani kilomita 25 (maili 16) magharibi mwa London ya Kati, hivyo kufikiwa kwa urahisi kwa gari, usafiri wa umma au Uber. Kusafiri kutoka Heathrow kwenda katikati mwa mji wa London huchukua saa moja, kwa hivyo mtu yeyote anayesafiri kwenda na kuondoka mji mkuu wa Uingereza, amefanya chaguo bora.

.

Vituo katika Uwanja wa Ndege wa Heathrow

London Heathrow una vituo 4 vinavyotumika: Vituo vya 2, 3, 4 na 5. Vituo vya 2 na 3 vinapatikana upande wa mashariki mwa Uwanja wa Ndege wa Heathrow, Kituo cha 4 Kusini na cha 5 upande wa Magharibi. Miongoni mwa mashirika mengi yanayohudumu, kuna:

Kituo cha 2

 • Aer Lingus
 • Singapore
 • United

Kituo cha 3

 • British Airways
 • Delta
 • Emirates

Kituo cha 4

 • Malaysia
 • Qatar

Kituo cha 5

 • British Airways

Vyakula kwenye Uwanja wa Ndege wa Heathrow

Heathrow ina migahawa na mabaa zaidi ya 30 unayoweza kuchagua, kwa hivyo iwe unataka kula kabla ya kuondoka au baada ya kuwasili, utapata migahawa mingi Heathrow.

Kusafiri kwenye LHR

Ni rahisi kutoka katika kituo kimoja hadi kingine kwenye Uwanja wa Ndege wa Heathrow. Unaweza kutoka kituo 2 hadi 3 kwa miguu, huku magari ya mara kwa mara yakiunganisha Kituo 4 na 5. Heathrow Express pia inapatikana, kusafiri kutoka Kituo cha 5 hadi vya 2 na 3, kisha kuelekea London ya Kati.

Mambo ya kufanya LHR

Iwe unatafuta makoti ya miundo ya kisasa au saa za kifahari, kuna maduka mengi ya kugundua kwenye Uwanja wa Ndege wa Heathrow. Kuna maduka mengi ya bidhaa zisizotozwa kodi kwenye Uwanja wa Ndege wa Heathrow, kwa watu wanaotaka kuwapelekea marafiki na ndugu zao hedaya. Maduka haya yanakusaidia kuhakikisha kuwa uko tayari kusafiri. Kuna sebule za kifahari pia kwenye uwanja wa ndege, zikiwemo No1 Lounge na Club Aspire Lounge, kwenye Kituo cha 3.

Mabafu kwenye Uwanja wa Ndege wa Heathrow

Sebule kwenye Uwanja wa Ndege wa Heathrow zina vyumba mbalimbali vya kuoga—zikiwemo Plaza Premium, No1, Club Aspire na Spa. Isitoshe, mabafu yanaweza kupatikana kwenye sebule za mashirika ya ndege husika.

Hoteli karibu na Uwanja wa Ndege wa Heathrow

Takriban hoteli 20 zinapatikana karibu na Uwanja wa Ndege wa Heathrow, jambo linalozifanya kuwa chaguo bora kwa wageni kwenye kituo au watu wanaowasili alfajiri. Kuna vyumba vingi vya bei nafuu na vya kifahari kwenye hoteli, kutokana na Mji wa London kuwa karibu.

Maeneo ya kuzuru karibu na Uwanja wa Ndege wa Heathrow

Ikiwa una muda wa kutosha unaposubiri ndege nyingine, unaweza kuzuru katikati mwa mji wa London. Kuna mambo mengi ya kufanya na kuona karibu na Uwanja wa Ndege wa LHR, ikiwa ni pamoja na:

 • Ham House
 • Legoland Windsor Resort
 • London Motor Museum
 • Royal Botanic Gardens, Kew
 • Windsor Castle

Pata maelezo zaidi kuhusu Uwanja wa Ndege wa LHR hapa.

Facebook
Twitter

Ukurasa huu una taarifa kutoka kwenye tovuti za washirika wengine ambazo hazisimamiwi na Uber na zinaweza kugeuzwa au kubadilishwa mara kwa mara. Maelezo yoyote yaliyojumuishwa kwenye ukurasa huu ambayo hayahusiani moja kwa moja na Uber au kazi zake yanatumika kuarifu tu na hayafai kutegemewa, au kuchukuliwa au kufasiliwa kwa namna inayoweka dhamana ya aina yoyote, iwe ya moja kwa moja au inayokisiwa, kuhusu maelezo yaliyo hapa. Baadhi ya masharti na vipengele hutofautiana kutegemea nchi, eneo na jiji. Ofa ya punguzo inawalenga watumiaji wapya pekee. Huwezi kutumia ofa hii pamoja na ofa nyinginezo na haiwezi kutumiwa katika bakshishi. Inapatikana kwa muda mfupi. Vigezo na masharti ya ofa vinaweza kubadilika.