Please enable Javascript
Ruka uende katika maudhui ya msingi

Uwanja wa Ndege wa London City (LCY)

Je, unatafuta mbinu mbadala ya usafiri ambayo si basi la kawaida la Uwanja wa Ndege wa London City au teksi? Iwe unasafiri kutoka Uwanja wa Ndege wa London City hadi London au kutoka katikati ya jiji hadi uwanja wa ndege, fika unakoenda ukitumia programu ya Uber unayoijua tayari. Omba gari la kukupeleka na kukurudisha kutoka LCY kwa kubofya kitufe.

London, E16 2PX
+44 20-7646-0000

search
Where from?
Navigate right up
search
Where to?

Request a ride around the world

Bofya kitufe sasa na upate usafiri wa uwanja wa ndege katika zaidi ya vituo vikuu 700.

Safiri kama mkazi

Acha programu na dereva wako washughulikie maelezo ya kina ili usisumbuke kutafuta maelekezo katika mji usiofahamu.

Safiri bila wasiwasi ukitumia Uber

Pata vipengele unavyovipenda, ikiwemo bei za wakati halisi na malipo ya kielektroniki, hata ukiwa ugenini.

Ways to ride in the area

Pickup at Uwanja wa Ndege wa London City (LCY)

Fungua programu yako ili uombe safari

Ukiwa tayari, fungua programu ya Uber ili uombe safari ya kuelekea mahali unakoenda. Chagua chaguo la usafiri wa uwanja wa ndege wa LCY linalokidhi mahitaji ya idadi ya wasafiri na mizigo yenu.

Fuata maelekezo kwenye programu

Utapata maelekezo kuhusu maeneo ya kuchukua wasafiri ya Uwanja wa Ndege wa London City moja kwa moja kwenye programu. Maeneo ya kuchukua wasafiri yanaweza kutofautiana kulingana na kituo. Ishara za maeneo ya kuchukua wasafiri wanaosafiri pamoja zinaweza pia kupatikana katika Uwanja wa Ndege wa London City.

Kutana na dereva wako

Nenda kwenye eneo lako la kuchukuliwa la LCY kama ilivyobainishwa kwenye programu. Tafadhali kumbuka: eneo hili huenda lisiwe kwenye lango la kutoka lililo karibu zaidi nawe. Jina la dereva wako, nambari ya leseni na rangi ya gari itaonyeshwa kwenye programu. Thibitisha gari lako kabla ya kuingia. Ikiwa humpati dereva wako, wasiliana naye kupitia programu.

Top questions from riders

  • Uber inapatikana katika Uwanja wa Ndege wa LCY, kwa hivyo unaweza kufurahia usafiri wa starehe na uhakika popote unapotaka kwenda.

  • Ili kupata eneo la kuchukuliwa, angalia programu ya Uber baada ya kuitisha usafiri.

  • Hata kama safari si ndefu sana, ada za Uber kutoka na kwenda Uwanja wa Ndege wa London City zinaweza kuathiriwa na muda, foleni na masuala mengine. Ada za uwanja wa ndege na maegesho pia zinaweza kuongezwa kwenye nauli yako kamili ya safari.

  • Muda wa kuchukuliwa unaweza kutofautiana kulingana na wakati, idadi ya madereva wanaopatikana na masuala mengine. Mara baada ya kuitisha usafiri, angalia programu ili uone kadirio la muda wa kusubiri.

More information

  • Unaendesha gari ukitumia Uber?

    Kuanzia eneo la kuwachukua wasafiri hadi kufuata sheria na kanuni za mahali husika, fahamu jinsi ya kufanya safari zako za uwanja wa ndege ziwe bora zaidi.

  • Unaelekea uwanja tofauti wa ndege?

    Unaweza kushushwa na kuchukuliwa kutoka zaidi ya viwanja 700 vya ndege kote ulimwenguni.

1/2

Vituo vya Uwanja wa Ndege wa London City: taarifa kwa wageni

Uber ni chaguo bora kwa wasafiri wanaowasili au kuondoka kwenye Uwanja wa Ndege wa London City (LCY). Uwanja wa Ndege wa LCY unawahudumia takribani wasafiri milioni 5 kila mwaka. Safari nyingi huwa za kikazi za kwenda Ulaya na Mji wa Newyork.

Kituo cha LYC

Uwanja wa Ndege wa London City ni mdogo ukilinganishwa na viwanja vingine maarufu mjini London, kama vile Heathrow, Gatwick na Stansted. Una kituo kimoja tu cha wasafiri, ambacho kimegawanya katika ghorofa 2. Ghorofa ya chini ina kibanda cha kukaguliwa na huduma mbalimbali. Ghorofa ya juu ina maduka, maeneo ya kusubiri, sebule na migahawa mingi. Mashirika ya ndege yafuatayo hutoa huduma katika Uwanja wa Ndege wa LYC:

  • Alitalia
  • British Airways
  • British Airways inayosimamiwa na SUN-AIR
  • CityJet
  • Flybe
  • KLM
  • Lufthansa
  • Luxair
  • SWISS
  • TAP Air Portugal

Migahawa kwenye LCY

Kuna migahawa na baa mbalimbali kwenye Uwanja wa Ndege wa London City kabla na baada ya sehemu ya kukaguliwa. Iwe unatafuta vyakula freshi au vya kubeba, ni rahisi kuvipata kabla ya safari.

Kwenda kwenye LCY

Uwanja wa Ndege wa LCY unapatikana umbali wa kilomita 10 (maili 6) mashariki mwa Central London. Utasafiri kwa kilomita 5 (maili 3) kutoka Canary Wharf ili uufikie. Hivyo basi ni mojawapo ya viwanja vya ndege vinavyofikiwa kwa urahisi zaidi. Kuna njia mbalimbali za usafiri kwa watu wanaokwenda na kuondoka kwenye Uwanja wa Ndege wa LCY. Utatumia dakika 30 tu kufika Central London. Docklands Light Railway (DLR) ndiyo mbinu kuu ya usafiri, lakini kuna mabasi mengi yanayohudumia uwanja huu. Kwa wale wanaosafiri kwenda London LCY kwa gari, kuna maegesho ya kutosha na Uber itawafaa zaidi. Unahitajika kuweka nafasi mapema ikiwa unapanga kuegesha gari lako kwenye uwanja wa ndege.

Maduka kwenye LCY

LCY ina bidhaa mbalimbali kama vile vitu unavyohitaji kwa dharura kabla ya safari na zawadi za kifahari. Isitoshe, maduka ya bidhaa zisizotozwa ushuru kwenye Uwanja wa Ndege wa London City—yanayopatikana kwenye eneo la Wanaoondoka baada ya kukaguliwa—ni bora kwa kwa ununuzi kabla ya safari, iwe unatafuta saa za kifahari au vipodozi murua.

Kubadilisha sarafu kwenye LCY

Vibanda vya kubadilisha sarafu vinapatikana LCY na unaweza kuagiza sarafu au kadi za kulipa mapema, hata saa 4 kabla kuchukuliwa.

Hoteli za LCY

Zaidi ya hoteli 10 zinapatikana karibu na Uwanja wa Ndege wa LCY. Zina aina mbalimbali za vyumba vya kulala kwa wale wanaotaka hoteli ya karibu. Kwa vile uko karibu na Central London, kuna hoteli nyingi za kifahari na nafuu. Zinazowafaa wageni wenye shughuli za kitaalamu na hoteli hizi zina vyumba vya mikutano na vituo vya biashara kwa ajili ya wataalamu wenye shughuli nyingi.

Sehemu za kuvutia karibu na LCY

Uwanja wa Ndege wa LCY unapatikana karibu na Canary Wharf. Uko karibu na unaweza kufikiwa kwa urahisi na wakaazi wengine wa London—ikiwa una muda wa kutosha kuzuru maeneo mbalimbali kabla ya kusafiri. Kwa kuwa Greenwich iko karibu sana, baadhi ya vivutio bora ni pamoja na:

  • The Cutty Sark
  • Greenwich Park
  • The National Maritime Museum
  • The Royal Observatory

Pata maelezo zaidi kuhusu Uwanja wa Ndege wa LCY hapa.

Facebook
Instagram
Twitter

This page contains information from third-party websites that are not under the control of Uber and that may be periodically changed or updated. Any information included on this page that is not directly related to Uber or its operations is for informational purposes only and in no way shall be relied upon, or interpreted or construed to create any warranties of any kind, either express or implied, regarding the information contained herein. Certain requirements and features vary by country, region, and city.