Ruka uende katika maudhui ya msingi

Uwanja wa Ndege wa London City (LCY)

Iwe unasafiri kuelekea London kutoka Uwanja wa Ndege wa London City au kutoka katikati ya jiji kuelekea Uwanja wa Ndege wa London City, iamini Uber kukufikisha unakoenda.

Hartmann Road, London E16 2PX, United Kingdom
+44 20-7646-0000

Njia bora zaidi ya kusafiri

Itisha usafiri kote ulimwenguni

Bonyeza tu kitufe ili upate usafiri wa angani katika zaidi ya viwanja vikuu 500.

Safiri kama mwenyeji

Acha App na dereva wako ashughulikie masuala ya kina ili usisumbuke kutafuta maelekezo katika jiji ambapo wewe ni mgeni.

Safiri bila wasiwasi kwa kutumia Uber

Pata vipengele unavyovipenda, ikiwa ni pamoja na bei zinazooneshwa moja kwa moja na uwezo wa kulipa bila pesa taslimu, hata ukiwa ugenini.

Aina za usafiri ukiwa eneo husika

 • UberX

  1-3

  Affordable rides, all to yourself

 • Green

  1-3

  Sustainable trips in electric vehicles

 • Comfort

  1-3

  New, spacious cars and top-rated drivers

 • Exec

  1-3

  Premium rides in high-end cars

 • UberXL

  1-5

  Affordable rides for groups up to 5

 • Lux

  1-3

  Ultimate luxury & style

1/6

Jinsi ya kupata usafiri wa Uber kutoka uwanja wa ndege

Fungua App yako ili uitishe usafiri

Ukiwa tayari kutoka nje, fungua programu yako kisha uitishe usafiri. Chagua usafiri unaotoshea idadi ya wasafiri na mizigo mliyo nayo.

Fuata maelekezo katika App

Utapata maelekezo kuhusu eneo la kuchukua wasafiri moja kwa moja katika programu. Pia kunaweza kuwa na alama katika uwanja wa ndege.

Kutana na dereva wako

Nenda katika eneo la kuchukuliwa jinsi ilivyobainishwa katika App. Tafadhali kumbuka, eneo hilo huenda halitakuwa karibu kabisa na lango unaloondokea. Ikiwa humpati dereva wako, wasiliana naye kupitia App.

Vidokezo vya usafiri katika Uwanja wa Ndege wa London City

WiFi katika Uwanja wa Ndege wa London City

Uwanja wa Ndege wa LCY unatoa huduma za WiFi bila malipo kwa wasafiri walio katika jengo la kituo. Unatakiwa tu kuunganisha kwenye mtandao wa LCY wa WiFi bila malipo kisha uthibitishe anwani yako ya barua pepe.

Maegesho katika Uwanja wa Ndege wa London City

Uwanja wa Ndege wa LCY una aina nyingi za maegesho, yakiwemo maegesho ya muda mfupi, maegesho ya muda mrefu, pamoja na huduma ya kumwachia mhudumu gari aliegeshe. Maegesho hayapo mbali sana na jengo kuu la kituo.

Kuhifadhi mizigo katika Uwanja wa Ndege wa London City

Kuna sehemu salama kwa ajili ya kuweka mizigo ya wasafiri. Utatozwa kila baada ya saa 24. Ili iweze kutumia huduma ya kuwekewa mizigo, andikisha bidhaa zako katika Dawati la Taarifa kabla ya kuelekea katika chumba cha kuacha mizigo.

Maswali ambayo wasafiri wanauliza sana

 • Uber inapatikana katika Uwanja wa Ndege wa LCY, kwa hivyo unaweza kufurahia usafiri wa starehe na uhakika popote unapotaka kwenda.

 • Ili kupata eneo la kuchukuliwa, angalia programu ya Uber baada ya kuitisha usafiri.

 • Hata kama safari si ndefu sana, ada za Uber kutoka na kwenda Uwanja wa Ndege wa London City zinaweza kuathiriwa na muda, foleni na masuala mengine. Ada za uwanja wa ndege na maegesho pia zinaweza kuongezwa kwenye nauli yako kamili ya safari.

 • Muda wa kuchukuliwa unaweza kutofautiana kulingana na wakati, idadi ya madereva wanaopatikana na masuala mengine. Mara baada ya kuitisha usafiri, angalia programu ili uone kadirio la muda wa kusubiri.

Maelezo zaidi

Unatumia mfumo wa Uber kuendesha gari?

Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kurahisisha huduma unayopokea katika viwanja vya ndege, zikiwemo sheria na kanuni za nchi husika.

Je, unaelekea uwanja tofauti wa ndege?

Unaweza kupelekwa na kuchukuliwa kutoka zaidi ya viwanja 600 vya ndege kote duniani.

Vituo vya Uwanja wa Ndege wa London City: taarifa kwa wageni

Uber ni chaguo bora kwa wasafiri wanaowasili au kuondoka kwenye Uwanja wa Ndege wa London City (LCY). Uwanja wa Ndege wa LCY unawahudumia takribani wasafiri milioni 5 kila mwaka. Safari nyingi huwa za kikazi za kwenda Ulaya na Mji wa Newyork.

Kituo cha LYC

Uwanja wa Ndege wa London City ni mdogo ukilinganishwa na viwanja vingine maarufu mjini London, kama vile Heathrow, Gatwick na Stansted. Una kituo kimoja tu cha wasafiri, ambacho kimegawanya katika ghorofa 2. Ghorofa ya chini ina kibanda cha kukaguliwa na huduma mbalimbali. Ghorofa ya juu ina maduka, maeneo ya kusubiri, sebule na migahawa mingi. Mashirika ya ndege yafuatayo hutoa huduma katika Uwanja wa Ndege wa LYC:

 • Alitalia
 • British Airways
 • British Airways inayosimamiwa na SUN-AIR
 • CityJet
 • Flybe
 • KLM
 • Lufthansa
 • Luxair
 • SWISS
 • TAP Air Portugal

Migahawa kwenye LCY

Kuna migahawa na baa mbalimbali kwenye Uwanja wa Ndege wa London City kabla na baada ya sehemu ya kukaguliwa. Iwe unatafuta vyakula freshi au vya kubeba, ni rahisi kuvipata kabla ya safari.

Kwenda kwenye LCY

Uwanja wa Ndege wa LCY unapatikana umbali wa kilomita 10 (maili 6) mashariki mwa Central London. Utasafiri kwa kilomita 5 (maili 3) kutoka Canary Wharf ili uufikie. Hivyo basi ni mojawapo ya viwanja vya ndege vinavyofikiwa kwa urahisi zaidi. Kuna njia mbalimbali za usafiri kwa watu wanaokwenda na kuondoka kwenye Uwanja wa Ndege wa LCY. Utatumia dakika 30 tu kufika Central London. Docklands Light Railway (DLR) ndiyo mbinu kuu ya usafiri, lakini kuna mabasi mengi yanayohudumia uwanja huu. Kwa wale wanaosafiri kwenda London LCY kwa gari, kuna maegesho ya kutosha na Uber itawafaa zaidi. Unahitajika kuweka nafasi mapema ikiwa unapanga kuegesha gari lako kwenye uwanja wa ndege.

Maduka kwenye LCY

LCY ina bidhaa mbalimbali kama vile vitu unavyohitaji kwa dharura kabla ya safari na zawadi za kifahari. Isitoshe, maduka ya bidhaa zisizotozwa ushuru kwenye Uwanja wa Ndege wa London City—yanayopatikana kwenye eneo la Wanaoondoka baada ya kukaguliwa—ni bora kwa kwa ununuzi kabla ya safari, iwe unatafuta saa za kifahari au vipodozi murua.

Kubadilisha sarafu kwenye LCY

Vibanda vya kubadilisha sarafu vinapatikana LCY na unaweza kuagiza sarafu au kadi za kulipa mapema, hata saa 4 kabla kuchukuliwa.

Hoteli za LCY

Zaidi ya hoteli 10 zinapatikana karibu na Uwanja wa Ndege wa LCY. Zina aina mbalimbali za vyumba vya kulala kwa wale wanaotaka hoteli ya karibu. Kwa vile uko karibu na Central London, kuna hoteli nyingi za kifahari na nafuu. Zinazowafaa wageni wenye shughuli za kitaalamu na hoteli hizi zina vyumba vya mikutano na vituo vya biashara kwa ajili ya wataalamu wenye shughuli nyingi.

Sehemu za kuvutia karibu na LCY

Uwanja wa Ndege wa LCY unapatikana karibu na Canary Wharf. Uko karibu na unaweza kufikiwa kwa urahisi na wakaazi wengine wa London—ikiwa una muda wa kutosha kuzuru maeneo mbalimbali kabla ya kusafiri. Kwa kuwa Greenwich iko karibu sana, baadhi ya vivutio bora ni pamoja na:

 • The Cutty Sark
 • Greenwich Park
 • The National Maritime Museum
 • The Royal Observatory

Pata maelezo zaidi kuhusu Uwanja wa Ndege wa LCY hapa.

Facebook
Instagram
Twitter

Ukurasa huu una taarifa kutoka kwenye tovuti za washirika wengine ambazo hazisimamiwi na Uber na zinaweza kugeuzwa au kubadilishwa mara kwa mara. Maelezo yoyote yaliyojumuishwa kwenye ukurasa huu ambayo hayahusiani moja kwa moja na Uber au kazi zake yanatumika kuarifu tu na hayafai kutegemewa, au kuchukuliwa au kufasiliwa kwa namna inayoweka dhamana ya aina yoyote, iwe ya moja kwa moja au inayokisiwa, kuhusu maelezo yaliyo hapa. Baadhi ya masharti na vipengele hutofautiana kutegemea nchi, eneo na jiji. Ofa ya punguzo inawalenga watumiaji wapya pekee. Huwezi kutumia ofa hii pamoja na ofa nyinginezo na haiwezi kutumiwa katika bakshishi. Inapatikana kwa muda mfupi. Vigezo na masharti ya ofa vinaweza kubadilika.