Ruka uende katika maudhui ya msingi
Uber
Uber

Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa McCarran (LAS)

Iwe unasafiri kutoka Uwanja wa Ndege wa McCarran kwenda tamasha iliyo mjini Vegas au kutoka Kiwanja Kidogo cha Ndege kuelekea McCarran, Uber itakuwezesha kufika huko.

5757 Wayne Newton Boulevard, Las Vegas, NV 89119
+1 702-261-5211

Njia bora zaidi ya kusafiri

Itisha usafiri kote ulimwenguni

Bonyeza tu kitufe ili upate usafiri wa angani katika zaidi ya viwanja vikuu 500.

Safiri kama mwenyeji

Acha App na dereva wako ashughulikie masuala ya kina ili usisumbuke kutafuta maelekezo katika jiji ambapo wewe ni mgeni.

Safiri bila wasiwasi kwa kutumia Uber

Pata vipengele unavyovipenda, ikiwa ni pamoja na bei zinazooneshwa moja kwa moja na uwezo wa kulipa bila pesa taslimu, hata ukiwa ugenini.

Mfumo wa Uber wa kukadiria nauli

Sampuli za bei za msafiri ni makadirio tu na hazioneshi mabadiliko yanayotokana na mapunguzo, kucheleweshwa kwenye foleni na mambo mengine. Tunaweza kutumia nauli isiyobadilika na bei za chini zaidi. Bei halisi zinaweza kubadilika.

Njia za kusafiri

 • Pool1-2

  Usafiri wa pamoja, bei nafuu

 • Comfort1-4

  Newer cars with extra legroom

 • UberX1-4

  Usafiri wa bei nafuu unaopatikana kila siku

Jinsi ya kusafiri kutoka Uwanja wa Ndege wa Las Vegas

Ita gari ukiwa tayari kutoka nje

Na uchague gari linalotoshea wasafiri na mizigo mliyo nayo.

Ondoka kupitia ghorofa ya wanaowasili

Ukiwa katika kituo cha 1, elekea kwenye maegesho ya T1 na utumie lifti hadi daraja la 2M ukutane na dereva wako. Ukiwa Kituo cha 3, elekea kwenye maegesho ya T3 na utumie lifti hadi Valet Level (V).

Thibitisha mahali ulipo

Unapodokezwa na programu, weka namba ya kituo ili dereva wako ajue mahali atakukuta. Ikiwa humpati dereva wako, wasiliana naye kupitia programu.

Ada za maegesho katika Uwanja wa Ndege wa Las Vegas

Ikiwa unapanga safari ya kwenda Uwanja wa Ndege wa Las Vegas na unatarajia kuendesha gari, unaweza kupata ada za maegesho hapa.

Aina ya maegesho

Ya Muda Mrefu

Ada

$16 kila siku
Huenda ada za maegesho zikawa zimebadilika; taarifa hii iliwekwa Tarehe 20 Novemba, 2018.

Ramani ya Uwanja wa Ndege wa Las Vegas

Uwanja wa Ndege wa McCarran una vituo 2, Kituo cha 1 na cha 3 na jumla ya kumbi 5 na malango 110.

Maswali ambayo wasafiri wanauliza sana

Ndiyo. Bonyeza hapa ili uone orodha ya viwanja vya ndege kote duniani unakoweza kuitisha usafiri wa Uber.

Nauli ya usafiri wa Uber kuenda (au kutoka) Uwanja wa Ndege wa LAS inategemea hali kama vile aina ya usafiri, kadirio ya umbali na muda wa safari, ada ya vibali barabarani na idadi ya maombi ya usafiri.

Unaweza kuona kadirio la bei kabla ya kuitisha usafiri kwa kuweka eneo la kuchukuliwa na mahali unakoenda katika zana ya kukadiria nauli katika Uber hapo juu. Kisha, unapoitisha usafiri utaona nauli yako halisi kwenye programu kwa kutegemea hali za wakati huo.

Maeneo ya kuchukuliwa yanategemea aina ya usafiri unaoitisha na ukubwa wa uwanja wa ndege. Fuata maagizo kwenye programu kuhusu eneo utakakomkuta dereva wako. Unaweza pia kuangalia mabango yanayoashiria maeneo ya usafiri wa pamoja yaliyobainishwa kwenye uwanja wa ndege.

Ikiwa humpati dereva wako, wasiliana naye kupitia programu.

Maelezo zaidi

Unatumia mfumo wa Uber kuendesha gari?

Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kurahisisha huduma unayopokea katika viwanja vya ndege, zikiwemo sheria na kanuni za nchi husika.

Je, unaelekea uwanja tofauti wa ndege?

Unaweza kupelekwa na kuchukuliwa kutoka zaidi ya viwanja 500 vya ndege kote duniani.

Maelezo ya wageni kwenye Uwanja wa Ndege wa Las Vegas

Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa McCarran (LAS) ndiyo uwanja mkuu kwa maeneo ya Las Vegas, Nevada na mpaka wa Las Vegas Valley. Ndio uwanja wa 8 wenye shughuli nyingi duniani kwa kuzingatia idadi ya ndege zinazohudumu. Uwanja upo Paradise, takribani maili 5 (kilomita 8) kusini mwa katikati ya jiji la Las Vegas na unafikiwa kwa urahisi na abiria wanaoingia na kutoka jijini. Uwanja wa ndege uko umbali wa takribani dakika 15 kutoka katikati ya jiji kwa kuendesha gari wakati hakuna foleni au vikwazo vingine barabarani.

Vituo katika Uwanja wa Ndege wa LAS

Uwanja wa Ndege wa LAS umegawanywa katika vituo 2: Kituo cha 1 na Kituo cha 3. Kituo cha 1 kina njia 4 (A, B, C na D) na Kituo cha 3 kina njia moja (E). Kumbi zinaweza kupatikana katika vituo vyote viwili vya McCarran. Unaweza kupanga safari yako ukitumia taarifa zilizo hapa chini.

Kituo cha 1 katika LAS

 • Allegiant
 • American
 • Delta
 • Kusini magharibi
 • Spirit
 • Ukumbi wa Centurion
 • The Club at LAS
 • United Club

Kituo cha 3 katika LAS

 • Aeroméxico
 • Air Canada
 • British Airways
 • Condor
 • Copa
 • Edelweiss
 • Eurowings
 • Hainan
 • InterJet
 • Korean Air
 • LATAM
 • Norwegian
 • Thomas Cook
 • Virgin Atlantic
 • Viva
 • Volaris
 • WestJet
 • The Club at LAS

Kituo cha kimataifa katika LAS

Wanaoelekea safari za kimataifa kutoka Uwanja wa Ndege wa McCarran hutokea Kituo cha 3, Malango ya E1 hadi E7. Uwanja wa Las Vegas una usafiri wa moja kwa moja kuelekea zaidi ya miji 150 kote duniani. Kituo cha 3 ni makao ya Club at LAS, ukumbi ulio wazi kwa abiria wote.

Kupata chakula katika uwanja wa LAS

Kuna zaidi ya maeneo 80 ya kula na kuburudika katika maeneo mbalimbali ya uwanja wa ndege. Chaguo hizi ni pamoja na vyakula vya kufungashiwa, mapishi ya kimataifa, baa, migahawa na maduka ya kahawa. Ikiwa unataka kula kabla ya kupita sehemu ya ukaguzi wa usalama, kuna sehemu kadhaa katika eneo la madukani na eneo la tiketi kwenye Kituo cha 1. Baada ya kupita eneo la usalama, kuna maeneo mengine ya kupata chakula katika Uwanja wa Ndege wa McCarran.

Kusafiri katika uwanja wa ndege wa LAS

Wasafiri katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa McCarran wanaweza kutumia mfumo wa People Movers ambayo ni treni otomatiki ya umeme iliyo na laini 3: Green Line inayounganisha Kituo cha 1 na Njia ya Lango la C, Blue Line inayounganisha Kituo cha 1 na Njia ya Lango la D, na Red Line inayounganisha Lango la D na Njia ya Kituo cha 3.

Mambo ya kufanya LAS

Uwanja wa Ndege wa McCarran una vivutio kadhaa, yakiwemo maonesho ya sanaa katika majengo 2 ya vituo. Maonesho hayo yanajumuisha vinyago, picha zilizochorwa ukutani na picha za nakshi. Watoto wanaweza kutumia eneo la kucheza katika Lango la D kwenye Daraja 2, watu wazima wanaweza kucheza katika zaidi ya mashine 1,000 za bahati nasibu zilizo kwenye maeneo mbalimbali ya uwanja wa ndege. Vilevile, wasafiri wanaweza kuvinjari sehemu ya makumbusho ya uwanja wa ndege iliyo na historia ya usafiri wa hewani katika eneo la kusini mwa Nevada. Hautozwi kuingia katika jumba hilo la makumbusho, lililo karibu na njia ya sehemu ya kuchukua mizigo. .

Kubadilisha sarafu kwenye LAS

Maeneo ya kubadilisha fedha katika Uwanja wa Ndege wa McCarran yapo katika sehemu za kuchukua mizigo katika Kituo cha 1 na Kituo cha 3.

Hoteli zilizo karibu na LAS

Iwe unasubiri ndege nyingine au ndege imechelewa usiku kucha, au kama unahitaji mahali pa kukaa karibu na LAS, kuna zaidi ya hoteli 60 na maeneo ya kulala karibu.

Sehemu za kuvutia karibu na LAS

 • Hoover Dam
 • Las Vegas Strip
 • Korongo ya Red Rock

Pata Maelezo zaidi kuhusu LAS hapa.

Facebook
Instagram
Twitter