Ruka uende katika maudhui ya msingi
Uber
Uber

Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa OR Tambo (JNB)

Iwe unasafiri kuelekea katikati ya jiji kutoka Uwanja wa Ndege wa Johannesburg kutoka katikati ya jiji kuelekea Uwanja wa Ndege wa Johannesburg, iamini Uber kukufikisha unakoenda.

1 Jones Road, Kempton Park, Johannesburg, 1632, South Africa
+27 11-921-6262

Njia bora zaidi ya kusafiri

Itisha usafiri kote ulimwenguni

Bonyeza tu kitufe ili upate usafiri wa angani katika zaidi ya viwanja vikuu 500.

Safiri kama mwenyeji

Acha App na dereva wako ashughulikie masuala ya kina ili usisumbuke kutafuta maelekezo katika jiji ambapo wewe ni mgeni.

Safiri bila wasiwasi kwa kutumia Uber

Pata vipengele unavyovipenda, ikiwa ni pamoja na bei zinazooneshwa moja kwa moja na uwezo wa kulipa bila pesa taslimu, hata ukiwa ugenini.

Mfumo wa Uber wa kukadiria nauli

Sampuli za bei za msafiri ni makadirio tu na hazioneshi mabadiliko yanayotokana na mapunguzo, kucheleweshwa kwenye foleni na mambo mengine. Tunaweza kutumia nauli isiyobadilika na bei za chini zaidi. Bei halisi zinaweza kubadilika.

Njia za kusafiri

  • UberX1-4

    Affordable, everyday rides

  • Black1-4

    Premium rides in luxury cars

  • Gari aina ya Van1-7

    Rides for groups up to 7

Jinsi ya kupata usafiri wa Uber kutoka uwanja wa ndege

Fungua App yako ili uitishe usafiri

Ukiwa tayari kutoka nje, fungua programu yako kisha uitishe usafiri. Chagua usafiri unaotoshea idadi ya wasafiri na mizigo mliyo nayo.

Fuata maelekezo katika App

Utapata maelekezo kuhusu eneo la kuchukua wasafiri moja kwa moja katika programu. Pia kunaweza kuwa na alama katika uwanja wa ndege.

Kutana na dereva wako

Nenda katika eneo la kuchukuliwa jinsi ilivyobainishwa katika App. Tafadhali kumbuka, eneo hilo huenda halitakuwa karibu kabisa na lango unaloondokea. Ikiwa humpati dereva wako, wasiliana naye kupitia App.

Vidokezo vya kuzingatia katika Uwanja wa Ndege wa OR Tambo

WiFi katika Uwanja wa Ndege wa OR Tambo

Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa OR Tambo hutoa huduma za WiFi bila malipo kwa wasafiri wote, inapatikana kwa muda wa saa 4 au hadi kufikia kikomo cha GB1. Baada ya hapo unaweza kuongezea data yako kwa kulipia kiasi unachotumia.

Maegesho katika Uwanja wa Ndege wa OR Tambo

Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa OR Tambo una maegesho kwenye uwanja kwa muda mfupi na muda mrefu, pia una sehemu za kushukisha na kuchukua wasafiri. Kuna nafasi 11,500 za kuegesha kwa umma katika maegesho 9.

Kubadilisha sarafu katika uwanja wa ndege wa OR Tambo

Madawati ya Travelex ya kubadilisha fedha za kigeni na huduma nyingine yapo katika duka la bidhaa zisizotozwa ushuru na upande wa kuabiri ndege pia. JNB pia ina matawi kadhaa ya benki, yakiwamo Absa, American Express na First National Bank.

Maswali ambayo wasafiri wanauliza sana

Uber inapatikana katika Uwanja wa Ndege wa JNB, kwa hivyo unaweza kufurahia usafiri wa starehe na uhakika popote unapotaka kwenda.

Ili kupata eneo la kuchukuliwa, angalia programu ya Uber baada ya kuitisha usafiri.

Hata kama safari si ndefu sana, ada za Uber kutoka na kwenda Uwanja wa Ndege wa OR Tambo zinaweza kuathiriwa na muda, foleni na masuala mengine. Angalia mfumo wa kukadiria nauli za Uber ili ufahamu makadirio ya nauli ya safari.

Muda wa kuchukuliwa unaweza kutofautiana kulingana na wakati, idadi ya madereva wanaopatikana na masuala mengine.

Maelezo zaidi

Unatumia mfumo wa Uber kuendesha gari?

Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kurahisisha huduma unayopokea katika viwanja vya ndege, zikiwemo sheria na kanuni za nchi husika.

Je, unaelekea uwanja tofauti wa ndege?

Unaweza kupelekwa na kuchukuliwa kutoka zaidi ya viwanja 500 vya ndege kote duniani.

Taarifa kwa wasafiri katika Uwanja wa Ndege wa Johannesburg