Ruka uende katika maudhui ya msingi
Uber
Uber

Uwanja wa Ndege wa Istanbul Atatürk (IST)

Iwe unasafiri kuelekea Istanbul kutoka Uwanja wa Ndege wa Atatürk au kutoka katikati ya jiji kuelekea Uwanja wa Ndege wa Atatürk, iamini Uber kukufikisha unakoenda.

Yeşilköy, 34149 Bakırköy/Istanbul, Turkey
+90 212-463-30-00

Njia bora zaidi ya kusafiri

Itisha usafiri kote ulimwenguni

Bonyeza tu kitufe ili upate usafiri wa angani katika zaidi ya viwanja vikuu 500.

Safiri kama mwenyeji

Acha App na dereva wako ashughulikie masuala ya kina ili usisumbuke kutafuta maelekezo katika jiji ambapo wewe ni mgeni.

Safiri bila wasiwasi kwa kutumia Uber

Pata vipengele unavyovipenda, ikiwa ni pamoja na bei zinazooneshwa moja kwa moja na uwezo wa kulipa bila pesa taslimu, hata ukiwa ugenini.

Mfumo wa Uber wa kukadiria nauli

Sampuli za bei za msafiri ni makadirio tu na hazioneshi mabadiliko yanayotokana na mapunguzo, kucheleweshwa kwenye foleni na mambo mengine. Tunaweza kutumia nauli isiyobadilika na bei za chini zaidi. Bei halisi zinaweza kubadilika.

Njia za kusafiri

 • Taxi Yellow1-4

  Taxi rides made easy

 • Taxi Turquoise1-4

  Premium taxi ride with comfortable vehicle

Jinsi ya kupata usafiri wa Uber kutoka uwanja wa ndege

Fungua App yako ili uitishe usafiri

Ukiwa tayari kutoka nje, fungua programu yako kisha uitishe usafiri. Chagua usafiri unaotoshea idadi ya wasafiri na mizigo mliyo nayo.

Fuata maelekezo katika App

Utapata maelekezo kuhusu eneo la kuchukua wasafiri moja kwa moja katika programu. Pia kunaweza kuwa na alama katika uwanja wa ndege.

Kutana na dereva wako

Nenda katika eneo la kuchukuliwa jinsi ilivyobainishwa katika App. Tafadhali kumbuka, eneo hilo huenda halitakuwa karibu kabisa na lango unaloondokea. Ikiwa humpati dereva wako, wasiliana naye kupitia App.

Vidokezo vya kuzingatia katika Uwanja wa Ndege wa Istanbul Atatürk

WiFi ukiwa Atatürk

Unaweza kupata huduma ya WiFi bila malipo katika Uwanja wa Ndege wa Atatürk kwa saa 2. Unahitaji kuwa na namba ya simu inayoweza kupokea SMS nchini Uturuki ili kuitumia, au unaweza kutumia huduma ya WiFi ya kulipia katika uwanja wa ndege.

Maegesho katika Uwanja wa Ndege wa Istanbul Atatürk

Uwanja wa Ndege wa Istanbul Atatürk una aina mbalimbali za maegesho, unaweza kupata sehemu ya kushukishia kwa haraka au maegesho ya muda mrefu. Baada ya gari kuegeshwa, tumia basi la uwanja wa ndege kwenda Istanbul Atatürk.

Kuhifadhi mizigo katika uwanja wa ndege wa Atatürk

Kuna ofisi za kuweka mizigo katika Kituo cha Kimataifa na Kituo cha Wasafiri wa Ndani, ofisi hizi zinawasaidia wasafiri wanaosubiri muda mrefu kuhifadhi mikoba yao na kusafiri kwenda Istanbul.

Maswali ambayo wasafiri wanauliza sana

Uber inapatikana katika Uwanja wa Ndege wa Atatürk, kwa hivyo unaweza kufurahia usafiri wa starehe na uhakika popote unapotaka kwenda.

Ili kupata eneo la kuchukuliwa, angalia programu ya Uber baada ya kuitisha usafiri.

Hata kama safari si ndefu sana, ada za Uber kutoka na kwenda Uwanja wa Ndege wa Atatürk zinaweza kuathiriwa na muda, foleni na masuala mengine. Angalia mfumo wa kukadiria nauli za Uber ili ufahamu makadirio ya nauli ya safari.

Muda wa kuchukuliwa unaweza kutofautiana kulingana na wakati, idadi ya madereva wanaopatikana na masuala mengine.

Maelezo zaidi

Je, unaelekea uwanja tofauti wa ndege?

Unaweza kupelekwa na kuchukuliwa kutoka zaidi ya viwanja 500 vya ndege kote duniani.
Pata uwanja wa ndege

Taarifa kwa wageni katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Atatürk

Uber ni bora kwa wasafiri wanaowasili au kuondoka kwenye Uwanja wa Ndege wa Istanbul Atatürk. Uwanja wa ndege wa Istanbul Atatürk ndio mkubwa zaidi nchini Uturuki kwa kuzingatia idadi ya wasafiri, Ndio uwanja wa pili kote ulimwenguni wenye safari nyingi zaidi za moja kwa moja. Kuendesha gari kutoka mji wa Istanbul hadi Uwanja wa Ndege wa Atatürk kunachukua takribani dakika 40. Hali hii inafanya uwanja huu kuwa chaguo bora kwa yeyote anayesafiri kuingia au kuondoka Istanbul. Msafiri ambaye hana gari anaweza kufika kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Atatürk kwa treni, basi au Uber.

Vituo vya Istanbul Atatürk

Uwanja wa Ndege wa Atatürk una vituo 2 vya wasafiri: Kituo cha Nchini na cha Kimataifa. Kama unavyotarajia, Kituo cha Usafiri wa Nchini kinashughulikia safari ndani ya nchi ya Uturuki. Kituo cha Kimataifa kinashughulikia safari za kimataifa na kimabara. Vituo hivi 2 vimeunganishwa, hivyo basi kurahisisha usafiri kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Atatürk ikilinganishwa na viwanja vingine vya kiwango kama hiki. Wi-Fi inapatikana katika vituo vyote viwili na unaweza kupata sehemu za kuchaji simu popote kwenye uwanja huu wa ndege.

Kituo cha Safari za Nchini

 • Turkish Airlines
 • Primeclass Lounge

Kituo cha Kimataifa

 • Air France
 • Emirates
 • Safari nyingine za kimabara na kimataifa
 • HSBC Premier Lounge

Vyakula katika Uwanja wa Ndege wa Istanbul Atatürk

Utapata vyakula freshi, vya kienyeji, vitafunio na zaidi katika migahawa mingi tofauti kwenye Uwanja wa Ndege wa Atatürk. Utafurahia njia nyingi za kupata chakula kama vile kujipakulia au kununua vyakula vya kubeba.

Kusafiri kwenye Uwanja wa Ndege wa Istanbul Atatürk

Vituo vya nchini na vya kimataifa vimekaribiana sana, kwa hivyo unaweza kutoka kwenye kituo kimoja kwenda kingine kwa miguu au traveleta—ambayo ni bora zaidi ikiwa una haraka.

Mambo unayoweza kufanya kwenye Uwanja wa ndege wa Atatürk

Kivutio kikuu katika Uwanja wa Ndege wa Atatürk ni maeneo ya ununuzi. Kuna duka kubwa la bidhaa zisizotozwa ushuru na Old Bazaar, mahali unapoweza kupata bidhaa halisi za Uturuki kama viungo, vifaa vya glasi na vito. Maduka ya bidhaa zisizotozwa ushuru kwenye Uwanja wa Ndege wa Atatürk ni sehemu bora ya kununulia marafiki na familia hedaya, na bidhaa mbalimbali kama vile pombe, mapambo, marashi na hata peremende. Huduma nyingine inajumuisha ukandaji wa mwili—ambayo ni huduma bora ya kujituliza kabla ya safari—na sebule nyingine zina mabafu.

Migahawa karibu na Uwanja wa Ndege wa Atatürk

Kuna hoteli mmoja kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Atatürk na zingine karibu nayo, ambazo ni bora kwa watu wanaowasili kwenye uwanja huu alfajiri. Sehemu za biashara, vyumba vya mikutano, migahawa na vyumba vya mazoezi vinapatikana kwenye hoteli hizi. Ni vyema kuangalia kwenye tovuti ya hoteli ili kuhakikisha ina kila kitu unachohitaji.

Maeneo ya kuvutia karibu na Atatürk

Kuna sehemu mbalimbali za kihistoria karibu na Atatürk, kama ilivyo kwenye uwanja wowote wa ndege mjini Istanbul. maeneo haya ni pamoja na:

 • The Blue Mosque
 • Mnara wa Galata
 • Grand Bazaar
 • The Hagia Sophia
 • Kasri ya Topkapi

Pata maelezo zaidi kuhusu Uwanja wa Ndege wa Istanbul Atatürk hapa.