Please enable Javascript
Ruka uende katika maudhui ya msingi

Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Incheon (ICN)

Je, unatafuta mbinu mbadala ya usafiri ambayo si basi la kawaida la Uwanja wa Ndege wa Incheon au teksi? Iwe unasafiri kutoka Uwanja wa Ndege wa Incheon hadi Uwanja wa Ndege wa Gimpo au kutoka Kituo cha Seoul hadi Uwanja wa Ndege wa Incheon, fika unakoenda ukitumia programu ya Uber unayoijua tayari. Omba gari la kukupeleka na kukurudisha kutoka ICN kwa kubofya kitufe.

Incheon, 22382
+82 2-1577-2600

search
Where from?
Navigate right up
search
Where to?

Request a ride around the world

Bofya kitufe sasa na upate usafiri wa uwanja wa ndege katika zaidi ya vituo vikuu 700.

Safiri kama mkazi

Acha programu na dereva wako washughulikie maelezo ya kina ili usisumbuke kutafuta maelekezo katika mji usiofahamu.

Safiri bila wasiwasi ukitumia Uber

Pata vipengele unavyovipenda, ikiwemo bei za wakati halisi na malipo ya kielektroniki, hata ukiwa ugenini.

Ways to ride in the area

Pickup at Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Incheon (ICN)

Itisha gari ukiwa tayari kutoka nje.

Chagua aina ya gari linalofaa starehe, idadi ya watu, lugha na mizigo mnayohitaji kubebewa.

Nenda katika eneo la kuchukuliwa

Eneo utakakochukuliwa litategemea gari utakalochagua:

  • Black: Eneo la Kuondoka la 14 la kituo cha 1, na la 6 kwa Kituo cha 2
  • Teksi ya Kimataifa: Eneo la Kuondoka la 4 la Kituo cha 1, na la 1 kwa Kituo cha 2

Kutana na dereva wako

Unaweza kuwasiliana na dereva wako kupitia programu.

Uwanja wa Ndege wa Incheon Map

Tafadhali angalia kituo unachotumia kisha uite gari kulingana na namba ya kituo chako. Unaweza kwenda kwenye kituo kingine kupitia barabara ya reli ya uwanja wa ndege au kwa basi bila malipo.

Ramani ya Uwanja wa Ndege wa Incheon

Top questions from riders

  • Ndiyo. Wasafiri wanaweza kuitisha usafiri kutumia programu ya Uber.

  • Inategemea eneo unakochukuliwa. Uber ina aina nyingi za usafiri wa bei nafuu.

  • Hapana. Hakuna ada tofauti ya uwanja wa ndege kwa safari za Uber kwenye Uwanja wa ndege.

  • Madereva wa UberBlack wanapatikana kwenye Lango la Kuondoka la 14 ukiwa kwenye Kituo cha 1 na Lango la 6 ukiwa kwenye Kituo 2.

    Madereva wa teksi wanaochukua wasafiri wa kimataifa wanasubiri kwenye Lango la Kuondoka la 4 ukiwa katika Kituo cha 1 na kwenye Lango la 1 ukiwa katika Kituo cha 2.

More information

  • Unaendesha gari ukitumia Uber?

    Kuanzia eneo la kuwachukua wasafiri hadi kufuata sheria na kanuni za mahali husika, fahamu jinsi ya kufanya safari zako za uwanja wa ndege ziwe bora zaidi.

  • Unaelekea uwanja tofauti wa ndege?

    Unaweza kushushwa na kuchukuliwa kutoka zaidi ya viwanja 700 vya ndege kote ulimwenguni.

1/2

Maelezo ya wageni katika Uwanja wa Ndege wa Incheon

Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Incheon (ICN) ndio uwanja mkubwa zaidi wa ndege nchini Korea Kusini.

Uwanja huu ulifunguliwa 2001 na sasa ICN unashindana na viwanja vingine vinavyoongoza duniani. ICN ulitangazwa na Shirika la Kukadiria Ubora wa Huduma za Viwanja vya Ndege kuwa uwanja bora wa ndege kwa miaka 12 mfululizo.

Uwanja wa Ndege wa Incheon ndilo lango kuu la kuingia Korea na upo umbali wa dakika 40 kutoka kituo cha Seoul jiji kuu la Korea Kusini.

Vituo katika Uwanja wa Ndege wa Incheon

Uwanja wa ICN una vituo 2 baada ya Kituo cha 2 kufunguliwa 2018. Kwa sababu ndege zimegawanywa katika vituo 2, unaweza kutumia maelezo yaliyo hapa chini kupanga safari yako.

Kituo cha 1 katika Uwanja wa Ndege wa Incheon

  • Air Incheon
  • Air Philip
  • Air Seoul
  • Asiana
  • Eastar Jet
  • Jeju
  • Jin
  • T’way
  • Mashirika mengine ya ndege

Kituo cha 2 katika Uwanja wa Ndege wa Incheon

  • Aeroflot
  • Aeroméxico
  • Air France
  • Alitalia
  • China
  • Czech
  • Delta
  • Garuda Indonesia
  • KLM
  • Korean Air
  • Xiamen

Katika hali ambapo mashirika mawili yanashirikiana kufanikisha safari moja, kituo kinaweza kubadilika kwa kutegemea safari husika. Tafadhali angalia kituo kwenye tiketi yako au kwa kutafuta katika tovuti ya ICN .

Mambo ya kufanya katika Uwanja wa Ndege wa Incheon

Kila mwaka, watu milioni 500 hutembelea ICN ili kuzuru au kupita Korea. Watu hawa wanaweza kufurahia tamaduni, tamasha na maonesho mbalimbali ambayo hufanyika katika uwanja huu wa ndege. ICN huandaa ziara za kuzuru uwanja wenyewe kwa walio katika safari za kutembelea Korea. Kuna zaidi ya maeneo 300 ya kupata chakula katika uwanja wa ndege, zikiwemo baa, maduka ya vitafunio na migahawa. Huduma nyingine kama vile, eneo la kompyuta, sehemu ya kulala, bafu, spaa, hoteli, ukumbi wa mazoezi ya kidijitali, sehemu ya watoto kuchezea, maabadi na ukumbi wa sinema yamefunguliwa kwa wageni wote.

Pata maelezo zaidi kuhusu Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Incheon hapa.

Facebook
Instagram
Twitter

This page contains information from third-party websites that are not under the control of Uber and that may be periodically changed or updated. Any information included on this page that is not directly related to Uber or its operations is for informational purposes only and in no way shall be relied upon, or interpreted or construed to create any warranties of any kind, either express or implied, regarding the information contained herein. Certain requirements and features vary by country, region, and city.