Ruka uende katika maudhui ya msingi

Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Incheon (ICN)

Tumia Uber kwenda popote, iwe unasafiri kutoka Uwanja wa Ndege wa Incheon kwenda Uwanja wa Ndege wa Gimpo au kutoka Kituo cha Seoul hadi Incheon.

272 Gonghang-ro, Jung-gu, Incheon, Republic of Korea 22382
+82 2-1577-2600

Njia bora zaidi ya kusafiri

Itisha usafiri kote ulimwenguni

Bonyeza tu kitufe ili upate usafiri wa angani katika zaidi ya viwanja vikuu 500.

Safiri kama mwenyeji

Acha App na dereva wako ashughulikie masuala ya kina ili usisumbuke kutafuta maelekezo katika jiji ambapo wewe ni mgeni.

Safiri bila wasiwasi kwa kutumia Uber

Pata vipengele unavyovipenda, ikiwa ni pamoja na bei zinazooneshwa moja kwa moja na uwezo wa kulipa bila pesa taslimu, hata ukiwa ugenini.

Punguzo la ₩20,000

Pata punguzo la ₩10,000 katika safari zako 2 zijazo ukitumia Uber International Taxi. Tumia kuponi KRAIRPORT. Ni sharti safari zianzie OR na kumalizikia ICN au uwanja wa ndege wa GMP. Vigezo na masharti kuzingatiwa.

Aina za usafiri ukiwa eneo husika

 • Uber Black

  1-4

  Large sedan with superb service

 • Intl Taxi

  1-3

  English speaking International taxi drivers, flat fare to and from ICN airport

1/2

Kupata gari kwenye Uwanja wa Ndege wa Incheon

Itisha gari ukiwa tayari kutoka nje.

Chagua aina ya gari linalofaa starehe, idadi ya watu, lugha na mizigo mnayohitaji kubebewa.

Nenda katika eneo la kuchukuliwa

Eneo utakakochukuliwa litategemea gari utakalochagua:

 • Black: Eneo la Kuondoka la 14 la kituo cha 1, na la 6 kwa Kituo cha 2
 • Teksi ya Kimataifa: Eneo la Kuondoka la 4 la Kituo cha 1, na la 1 kwa Kituo cha 2

Kutana na dereva wako

Unaweza kuwasiliana na dereva wako kupitia programu.

Ada za maegesho katika Uwanja wa Ndege wa Incheon

Ikiwa unapanga safari ya kwenda Uwanja wa Ndege wa Incheon na unatarajia kuendesha gari, unaweza kupata ada za maegesho hapa.
Ada za maegesho katika Uwanja wa Ndege wa Incheon

Ada

₩1,200 kwa dakika 30, ₩600 kwa kila dakika 15 za ziada, hadi ₩24,000 kwa siku
₩1,000 kwa saa, hadi ₩9,000 kwa siku (magari makubwa: ₩1,200 kwa dakika 30, hadi ₩12,000 kwa siku)
Haitozwi kwa dakika 45, utatozwa ₩500 kwa kila dakika 15 za ziada, ada ya juu kabisa ni ₩10,000 kwa siku (1.2x kwa magari makubwa)
Nyongeza ya ₩15,000 (magari madogo: ₩10,000) imeongezwa kwenye ada ya maegesho ya muda mrefu
Huenda ada za maegesho zikawa zimebadilika; taarifa hii iliwekwa Tarehe 6 Desemba 2018.

Ramani ya Uwanja wa Ndege wa Incheon

Tafadhali angalia kituo unachotumia kisha uite gari kulingana na namba ya kituo chako. Unaweza kwenda kwenye kituo kingine kupitia barabara ya reli ya uwanja wa ndege au kwa basi bila malipo.

Vidokezo kwa wageni kwenye Uwanja wa Ndege wa Incheon

Pata mtando wa simu wa eneo uliko

Unaweza kukodisha simu au Wi-Fi ya kubeba au ununue kadi ya SIM. Pata maelezo zaidi kwenye kituo cha usaidizi kwa wateja.

Zuru Korea kwa njia ya starehe: jaribu gari letu la kifahari, Uber Black

Uber Black ina dereva mwenye uzoefu wa gari dogo la kifahari, huduma ya maji, chaja ya simu na huduma za mlangoni.

Pata teksi ya wasafiri wa kimataifa

Ikiwa unataka kumpata dereva anayezungumza Kiingereza, itisha teksi ya Kimataifa kupitia mfumo wa Uber. Vituo vya usaidizi vinapatikana katika kila kituo.

Maswali ambayo wasafiri wanauliza sana

 • Ndiyo. Wasafiri wanaweza kuitisha usafiri kutumia programu ya Uber.

 • Inategemea eneo unakochukuliwa. Uber ina aina nyingi za usafiri wa bei nafuu.

 • Hapana. Hakuna ada tofauti ya uwanja wa ndege kwa safari za Uber kwenye Uwanja wa ndege.

 • Madereva wa UberBlack wanapatikana kwenye Lango la Kuondoka la 14 ukiwa kwenye Kituo cha 1 na Lango la 6 ukiwa kwenye Kituo 2.

  Madereva wa teksi wanaochukua wasafiri wa kimataifa wanasubiri kwenye Lango la Kuondoka la 4 ukiwa katika Kituo cha 1 na kwenye Lango la 1 ukiwa katika Kituo cha 2.

 • Sehemu za mizigo iliyopotea na kupatikana ziko katika Kituo cha 1 na 2. Nenda kwenye kituo au piga simu kwa +82 32-741-3110.

 • Unaweza kwenda kwenye benki au afisi ya kubadilisha sarafu inayofanya kazi wakati wowote katika uwanja wa ndege.

 • Kwenye Kituo cha Maelezo, tafuta eneo la karibu la PC, la kulala kwa muda mfupi, duka la dawa, chumba cha kuogea, spa, hoteli, chumba cha kufulia nguo, jumba la mazoezi la kisasa, uwanja wa kuchezea watoto, chumba cha kutunzia watoto, ofisi ya posta, chumba cha maombi na ukumbi wa sanaa.

 • Tafuta kibanda chenye nembo ya Uber karibu na Lango la kuondoka la 4 katika Kituo cha 1 au karibu na Lango la kuondoka la 3 katika Kituo cha 2.

Maelezo zaidi

Unatumia mfumo wa Uber kuendesha gari?

Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kurahisisha huduma unayopokea katika viwanja vya ndege, zikiwemo sheria na kanuni za nchi husika.

Je, unaelekea uwanja tofauti wa ndege?

Unaweza kupelekwa na kuchukuliwa kutoka zaidi ya viwanja 600 vya ndege kote duniani.

Maelezo ya wageni katika Uwanja wa Ndege wa Incheon

Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Incheon (ICN) ndio uwanja mkubwa zaidi wa ndege nchini Korea Kusini.

Uwanja huu ulifunguliwa 2001 na sasa ICN unashindana na viwanja vingine vinavyoongoza duniani. ICN ulitangazwa na Shirika la Kukadiria Ubora wa Huduma za Viwanja vya Ndege kuwa uwanja bora wa ndege kwa miaka 12 mfululizo.

Uwanja wa Ndege wa Incheon ndilo lango kuu la kuingia Korea na upo umbali wa dakika 40 kutoka kituo cha Seoul jiji kuu la Korea Kusini.

Vituo katika Uwanja wa Ndege wa Incheon

Uwanja wa ICN una vituo 2 baada ya Kituo cha 2 kufunguliwa 2018. Kwa sababu ndege zimegawanywa katika vituo 2, unaweza kutumia maelezo yaliyo hapa chini kupanga safari yako.

Kituo cha 1 katika Uwanja wa Ndege wa Incheon

 • Air Incheon
 • Air Philip
 • Air Seoul
 • Asiana
 • Eastar Jet
 • Jeju
 • Jin
 • T’way
 • Mashirika mengine ya ndege

Kituo cha 2 katika Uwanja wa Ndege wa Incheon

 • Aeroflot
 • Aeroméxico
 • Air France
 • Alitalia
 • China
 • Czech
 • Delta
 • Garuda Indonesia
 • KLM
 • Korean Air
 • Xiamen

Katika hali ambapo mashirika mawili yanashirikiana kufanikisha safari moja, kituo kinaweza kubadilika kwa kutegemea safari husika. Tafadhali angalia kituo kwenye tiketi yako au kwa kutafuta katika tovuti ya ICN .

Mambo ya kufanya katika Uwanja wa Ndege wa Incheon

Kila mwaka, watu milioni 500 hutembelea ICN ili kuzuru au kupita Korea. Watu hawa wanaweza kufurahia tamaduni, tamasha na maonesho mbalimbali ambayo hufanyika katika uwanja huu wa ndege. ICN huandaa ziara za kuzuru uwanja wenyewe kwa walio katika safari za kutembelea Korea. Kuna zaidi ya maeneo 300 ya kupata chakula katika uwanja wa ndege, zikiwemo baa, maduka ya vitafunio na migahawa. Huduma nyingine kama vile, eneo la kompyuta, sehemu ya kulala, bafu, spaa, hoteli, ukumbi wa mazoezi ya kidijitali, sehemu ya watoto kuchezea, maabadi na ukumbi wa sinema yamefunguliwa kwa wageni wote.

Pata maelezo zaidi kuhusu Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Incheon hapa.

Facebook
Instagram
Twitter

Ukurasa huu una taarifa kutoka kwenye tovuti za washirika wengine ambazo hazisimamiwi na Uber na zinaweza kugeuzwa au kubadilishwa mara kwa mara. Maelezo yoyote yaliyojumuishwa kwenye ukurasa huu ambayo hayahusiani moja kwa moja na Uber au kazi zake yanatumika kuarifu tu na hayafai kutegemewa, au kuchukuliwa au kufasiliwa kwa namna inayoweka dhamana ya aina yoyote, iwe ya moja kwa moja au inayokisiwa, kuhusu maelezo yaliyo hapa. Baadhi ya masharti na vipengele hutofautiana kutegemea nchi, eneo na jiji. Ofa ya punguzo inawalenga watumiaji wapya pekee. Huwezi kutumia ofa hii pamoja na ofa nyinginezo na haiwezi kutumiwa katika bakshishi. Inapatikana kwa muda mfupi. Vigezo na masharti ya ofa vinaweza kubadilika.