Please enable Javascript
Ruka uende katika maudhui ya msingi

Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Daniel K. Inouye (HNL)

Je, unatafuta mbinu mbadala ya usafiri ambayo si basi la kawaida la Uwanja wa Ndege wa Honolulu au teksi? Iwe unasafiri kutoka Uwanja wa Ndege wa Honolulu hadi Waikiki au kutoka Pearl Harbor hadi uwanja wa ndege, fika unakoenda ukitumia programu ya Uber unayoijua tayari. Omba gari la kukupeleka na kukurudisha kutoka HNL kwa kubofya kitufe.

Honolulu, HI 96819
+1 808-836-6411

search
Where from?
Navigate right up
search
Where to?

Request a ride around the world

Bofya kitufe sasa na upate usafiri wa uwanja wa ndege katika zaidi ya vituo vikuu 700.

Safiri kama mkazi

Acha programu na dereva wako washughulikie maelezo ya kina ili usisumbuke kutafuta maelekezo katika mji usiofahamu.

Safiri bila wasiwasi ukitumia Uber

Pata vipengele unavyovipenda, ikiwemo bei za wakati halisi na malipo ya kielektroniki, hata ukiwa ugenini.

Ways to ride in the area

Pickup at Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Daniel K. Inouye (HNL)

Fungua programu yako ili uombe safari

Ukiwa tayari, fungua programu ya Uber ili uombe safari ya kuelekea mahali unakoenda. Chagua chaguo la usafiri wa uwanja wa ndege wa HNL linalokidhi mahitaji ya idadi ya wasafiri na mizigo yenu.

Fuata maelekezo kwenye programu

Utapata maelekezo kuhusu maeneo ya kuchukuliwa katika Uwanja wa Ndege wa Honolulu moja kwa moja kwenye programu.

Kwa wanaowasili kutoka visiwani na mataifa mengine (Kituo cha 1), tumia sehemu ya pili katika ghorofa ya wanaoondoka mkabala na Ukumbi wa 2.

Kwa watu wanaotoka Marekani Bara (Kituo cha 2), tumia sehemu ya pili katika ghorofa ya wanaoondoka mkabala na Ukumbi wa 8.

Kutana na dereva wako

Nenda kwenye eneo lako la kuchukuliwa la HNL kama ilivyobainishwa kwenye programu. Tafadhali kumbuka: eneo hili huenda lisiwe kwenye lango la kutoka lililo karibu zaidi nawe. Jina la dereva wako, nambari ya leseni na rangi ya gari itaonyeshwa kwenye programu. Thibitisha gari lako kabla ya kuingia. Ikiwa humpati dereva wako, wasiliana naye kupitia programu.

Uwanja wa Ndege wa Honolulu Map

Uwanja wa Ndege wa Honolulu una vituo 3 tofauti. Kituo cha 1 awali kilijulikana kama Kituo cha Kisiwani na ndiyo makao ya Shirika la Ndege la Hawaii. Kituo cha 2 zamani kilikuwa kikijulikana kama Kituo cha Kimataifa, huku Kituo cha 3 kikijulikana kama Kituo cha Wasafiri wa Kawaida.

Ramani ya Uwanja wa Ndege wa Honolulu

Top questions from riders

  • Ndiyo. Nenda kwenye orodha hii ya viwanja vya ndege kote ulimwenguni unakoweza kuomba safari ukitumia Uber.

  • The cost of an Uber trip to (or from) HNL depends on factors that include the type of ride you request, the estimated length and duration of the trip, tolls, and current demand for rides.

    You can see an estimate of the price before you request by going here and entering your pickup spot and destination. Then when you request a ride you’ll see your actual price in the app based on real-time factors.

  • Maeneo ya kuchukuliwa yanategemea aina ya safari unayoomba na ukubwa wa uwanja wa ndege. Fuata maelekezo kwenye programu kuhusu mahali pa kukutana na dereva wako. Unaweza pia kutafuta ishara zinazoonyesha maeneo ya kusafiri pamoja yaliyobainishwa kwenye uwanja wa ndege.

    Ikiwa humpati dereva wako, wasiliana naye kupitia programu.

More information

  • Unaendesha gari ukitumia Uber?

    Kuanzia eneo la kuwachukua wasafiri hadi kufuata sheria na kanuni za mahali husika, fahamu jinsi ya kufanya safari zako za uwanja wa ndege ziwe bora zaidi.

  • Unaelekea uwanja tofauti wa ndege?

    Unaweza kushushwa na kuchukuliwa kutoka zaidi ya viwanja 700 vya ndege kote ulimwenguni.

1/2

Maelezo kwa wageni kwenye Uwanja wa Ndege wa Honolulu

Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Daniel K. Inouye (HNL) ni moja kati ya viwanja vya ndege vyenye shughuli nyingi sana Marekani, unawahudumia zaidi ya abiria milioni 20 kwa mwaka. Uwanja wenyewe upo takribani maili 6 (kilomita 10) kaskazini magharibi mwa katikati ya jiji la Honolulu, na unafikika kwa wasafiri wanaoingia na kuondoka jijini. Inachukua dakika 15 kwa kuendesha gari wakati hakuna foleni au vikwazo vingine barabarani kuufikia kutoka katikati ya jiji la Honolulu.

Vituo katika Uwanja wa Ndege wa Honolulu

Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Honolulu una vituo 3: Kituo cha 1, Kituo cha 2 na Kituo cha 3. Kituo cha 2 kinatumika sana kwa safari za kimataifa. Kuna malango 43 katika vituo vyote. Unaweza kupanga safari yako ukitumia taarifa zilizo hapa chini.

Kituo cha 1 katika HNL

  • Hawaiian
  • Hawaiian Airlines Premier Club

Kituo cha 2 katika HNL

  • AirAsia X
  • Air Canada
  • Air China
  • Air New Zealand
  • Alaska
  • All Nippon
  • American
  • Asiana
  • Boyd Vacations Hawaii
  • China Airlines
  • China Eastern Airlines
  • Delta
  • Fiji
  • Hawaiian
  • Japan Airlines
  • Jetstar
  • Jin Air
  • Korean Air
  • Philippine
  • Qantas
  • Scoot
  • Sun Country
  • United
  • WestJet

HNL Terminal 3

  • Mokulele

Kituo cha kimataifa katika HNL

Safari za kimataifa kutoka Uwanja wa Ndege wa Honolulu kwa kawaida zipo katika Kituo cha 2. HNL una safari za ndege za moja kwa moja za kimataifa kuelekea maeneo mbalimbali, yakiwemo Japani na Australia. Kituo cha 2 pia ni makao kwa zaidi ya kumbi 5 za Uwanja wa Ndege wa Honolulu, zikiwemo kumbi za Air New Zealand, United Club na ukumbi wa Korean Air.

Kupata chakula katika Uwanja wa Ndege wa Honolulu

Kuna zaidi ya maeneo 20 ya kupata chakula katika uwanja wa ndege, yakiwemo baa, maduka ya kahawa, maduka ya vitafunio na migahawa. Sehemu mahususi kwa ajili ya kula katika Uwanja wa Ndege wa Honolulu ipo kati ya Lango la E2 na Lango la E4 katika Kituo cha 2.

Kusafiri katika Uwanja wa Ndege wa Honolulu

Ili kusafiri kutoka vituo na malango katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Honolulu, wasafiri wanaweza kutumia mabasi ya Uwanja wa Ndege wa Honolulu. Basi lililo katika daraja la 3 kwenye Kituo cha 2 huwapeleka wasafiri wanaoondoka wa safari za kimataifa (ambao tayari wamepitia ukaguzi wa usalama) kwenye malango ya C au G. Abiria wanaowasili katika malango hayo wanaweza kutumia basi hilo kuelekea katika Kituo cha 1 au cha 2. Wasafiri wanaoingia katika Kituo cha 1 kwa ajili ya usafiri wa kuelekea bara kutoka Kituo cha 2 watakuta mabasi katika daraja la 3 ambayo yanaweza kuwapeleka katika malango wanayotaka.

Mambo ya kufanya katika Uwanja wa Ndege wa Honolulu

Uwanja wa Ndege wa HNL una vivutio mbalimbali, vikiwemo bustani zilizo na ushawishi wa tamaduni za Kichina, Kihawaii na Kijapani. Bustani hizo zinazingira ukumbi wa kununua tiketi na lango la E katika uwanja wa ndege. Uwanja huu wa ndege pia una bidhaa mbalimbali za sanaa, zikiwemo vinyago na michoro ya kutundika ukutani, ambayo inapatikana katika vituo vyote.

Kubadilisha sarafu katika Uwanja wa Ndege wa Honolulu

Ofisi za kubadilisha fedha katika Uwanja wa Ndege wa Honolulu zipo katika Kituo cha 2, upande wa pili wa duka la bidhaa zisizotozwa ushuru, katika Kituo cha 2 mkabala na Lango la F2, katika Kituo cha 2 mkabala na Lango la D2 na katika eneo la wanaowasili kutoka safari za kimataifa.

Hoteli zilizo karibu na Uwanja wa Ndege wa Honolulu

Iwe unasubiri ndege nyingine au ndege imechelewa usiku kucha, au kama unahitaji mahali pa kukaa karibu na HNL, kuna hoteli nyingi na maeneo ya kulala karibu.

Vivutio katika Uwanja wa Ndege wa Honolulu

  • Volkano ya Diamond Head
  • Manoa Falls
  • Pearl Harbor
  • Ufukwe wa Waikiki

Pata maelezo zaidi kuhusu Uwanja wa Ndege wa Honolulu hapa.

Facebook
Twitter

This page contains information from third-party websites that are not under the control of Uber and that may be periodically changed or updated. Any information included on this page that is not directly related to Uber or its operations is for informational purposes only and in no way shall be relied upon, or interpreted or construed to create any warranties of any kind, either express or implied, regarding the information contained herein. Certain requirements and features vary by country, region, and city.