Ruka uende katika maudhui ya msingi
Uber
Uber

Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Hong Kong (HKG)

Tumia Uber kwenda popote, iwe unasafiri kutoka Uwanja wa Ndege wa Hong Kong kwenda Mji wa Kowloon au kutoka Disneyland hadi Uwanja wa Ndege wa Hong Kong.

1 Sky Plaza Rd, Chek Lap Kok, Hong Kong
+852 2181-8888

Njia bora zaidi ya kusafiri

Itisha usafiri kote ulimwenguni

Bonyeza tu kitufe ili upate usafiri wa angani katika zaidi ya viwanja vikuu 500.

Safiri kama mwenyeji

Acha App na dereva wako ashughulikie masuala ya kina ili usisumbuke kutafuta maelekezo katika jiji ambapo wewe ni mgeni.

Safiri bila wasiwasi kwa kutumia Uber

Pata vipengele unavyovipenda, ikiwa ni pamoja na bei zinazooneshwa moja kwa moja na uwezo wa kulipa bila pesa taslimu, hata ukiwa ugenini.

Mfumo wa Uber wa kukadiria nauli

Sampuli za bei za msafiri ni makadirio tu na hazioneshi mabadiliko yanayotokana na mapunguzo, kucheleweshwa kwenye foleni na mambo mengine. Tunaweza kutumia nauli isiyobadilika na bei za chini zaidi. Bei halisi zinaweza kubadilika.

Utapata punguzo la hadi HK$75 kwenye safari yako ya kwanza

Je, ni mara yako ya kwanza kutumia Uber? Pata punguzo la HK$75 kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa HK. Tumia kuponi ya ofa HKAIRPORT. Vigezo na masharti kuzingatiwa.

Jisajili ili usafiri

Njia za kusafiri

 • Flash1-4

  Match with the closest Taxi or UberX

 • UberX1-4

  Affordable, everyday rides

 • Black1-4

  Premium rides in luxury cars

Kupata gari kwenye Uwanja wa Ndege wa Hong Kong

Ada za maegesho katika Uwanja wa Ndege wa Hong Kong

Ikiwa unapanga safari ya kwenda Uwanja wa Ndege wa Hong Kong na unatarajia kuendesha gari, unaweza kupata ada za maegesho hapa.

Aina ya maegesho

Maegesho ya 1

Car Park 4 Indoor Zone G/F - 3/F

Car Park 4 Outdoor Zone 5/F

Maegesho ya 5

SkyCity Car Park

Ada

Gari la binafsi kwa $24 kila saa
Ada ya magari ya kibinafsi ni $24 kwa saa au haipiti $192 kwa siku
Ada ya gari la kibinafsi ni $20 kila saa au ada zisizozidi $160 kila siku
Ada ya gari la kibinafsi ni $20 kila saa au ada zisizozidi $160 kila siku
Ada ya gari la kibinafsi ni $20 kila saa au ada zisizozidi $160 kila siku
Huenda ada za maegesho zikawa zimebadilika; taarifa hii iliwekwa Tarehe 17 Desemba, 2018.

Ramani ya Uwanja wa Ndege wa Hong Kong

Uwanja wa Ndege wa Hong Kong umegawanywa katika Kituo cha 1 na 2.

Kupata intaneti katika Uwanja wa Ndege wa Hong Kong

Jinsi ya kuunganisha kwenye wi-fi

Unaweza kupata muunganisho kwa WiFi bila malipo wakati wowote ukiwa kwenye vituo vya wasafiri. Chagua tu HKAirport Free Wifi kwenye mitandao ya Wi-Fi, kisha uwashe kivinjari cha intaneti na ufuate maagizo.

Kadi za SIM na WiFi ya kubeba

Nunua kadi za SIM za eneo lako au ukodishe Wi-Fi ya kubeba katika maduka na vibanda vifuatavyo:

 • Counter A01, Crazyegg
 • Counter A05, SONGWIFI
 • Counter A08, Uroaming
 • Counter A09, Banana Wifi
 • Counter A12a, VisonData
 • Counter A16, WiFiBB

Maelezo zaidi

Unatumia mfumo wa Uber kuendesha gari?

Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kurahisisha huduma unayopokea katika viwanja vya ndege, zikiwemo sheria na kanuni za nchi husika.

Je, unaelekea uwanja tofauti wa ndege?

Unaweza kupelekwa na kuchukuliwa kutoka zaidi ya viwanja 500 vya ndege kote duniani.

Maelezo kwa wageni kwenye Uwanja wa Ndege wa Hong Kong

Uwanja wa Ndege wa Hong Kong Airport, ambao pia huitwa Uwanja wa Ndege wa Chek Lap Kok, ni moja kati ya viwanja vya ndege vyenye shughuli nyingi zaidi duniani, huwa unawahudumia zaidi ya wasafiri milioni 72 wanaopitia Hong Kong kila mwaka.

Vituo vya Uwanja wa Ndege wa Hong Kong

Uwanja huu una vituo 2 vilivyotenganishwa na stesheni ya MTR. Kituo cha 1 ni makao ya mashirika mengi ya ndege, huku Kituo cha 2 kikihudumia sana mashirika ya usafiri nafuu wa ndege. Unaweza kupanga safari yako ukitumia taarifa zilizo hapa chini.

Kituo cha 1

Kituo cha 1 ndicho sehemu ya kuondoka na kuwasili.

Kituo cha 2

Kituo cha 2 ni kwa ajili ya kuingia na huduma za michakato ya kuwaandaa abiria kuondoka, hakina malango au huduma za kupokea wanaowasili. Wasafiri wote walioingia kupitia Kituo cha 2 husafirishwa kuelekea katika malango ya kuondoka katika Kituo cha 1 kupitia mfumo wa chini ya ardhi.

Mambo ya kufanya katika Uwanja wa Ndege wa Hong Kong

Uwanja wa Ndege wa Hong Kong una mambo mengi ya kufanya. Wasafiri wanaotafuta kitu cha kuchangamkia wanaweza kutembelea Kituo cha Aviation Discovery, klabu ya gofu ya ndani ya Greenlive, UA IMAX @ Airport na njia ya I-Sports. Ili kupata vyakula na vinywaji katika Uwanja wa Ndege wa Hong Kong, kuna chaguo tele, ipo migahawa ya vyakula vya kufungashiwa, mapishi ya Kifaransa, Kiasia na mengine mengi.

Kubadilisha sarafu katika Uwanja wa Ndege wa Hong Kong

Ukiwa katika Uwanja wa Ndege wa Hong Kong, unaweza kupata vituo vingi vya Global Exchange kwa ajili ya kubadilisha hela zako.

Hoteli zilizo karibu na Uwanja wa Ndege wa Hong Kong

Kuna hoteli kadhaa zilizo hatua ya kutembea au usafiri wa muda mfupi kwa basi kutoka katika uwanja wa ndege. Ukiamua kuvinjari jijini, unaweza kupata hoteli na sehemu za kulala mwendo wa karibu kwa gari.

Maeneo ya kuvutia karibu na Uwanja wa Ndege wa Hong Kong

 • Bustani ya Lantau Country
 • Lantau Trail
 • Gari la kamba la Ngong Ping 360
 • Tian Tan Buddha
 • Wisdom Path

Pata maelezo zaidi kuhusu Uwanja wa Ndege wa Hong Kong (HKG) hapa.

Facebook
Instagram
Twitter