Ruka uende katika maudhui ya msingi
Uber
Uber

Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Geneva (GVA)

Iwe unasafiri kuelekea katikati ya jiji kutoka Uwanja wa Ndege wa Geneva kutoka katikati ya jiji kuelekea Uwanja wa Ndege wa Geneva, iamini Uber kukufikisha unakoenda.

Route de l'Aéroport 21, 1215 Le Grand-Saconnex, Switzerland
+41 22-717-71-11

Njia bora zaidi ya kusafiri

Itisha usafiri kote ulimwenguni

Bonyeza tu kitufe ili upate usafiri wa angani katika zaidi ya viwanja vikuu 500.

Safiri kama mwenyeji

Acha App na dereva wako ashughulikie masuala ya kina ili usisumbuke kutafuta maelekezo katika jiji ambapo wewe ni mgeni.

Safiri bila wasiwasi kwa kutumia Uber

Pata vipengele unavyovipenda, ikiwa ni pamoja na bei zinazooneshwa moja kwa moja na uwezo wa kulipa bila pesa taslimu, hata ukiwa ugenini.

Mfumo wa Uber wa kukadiria nauli

Sampuli za bei za msafiri ni makadirio tu na hazioneshi mabadiliko yanayotokana na mapunguzo, kucheleweshwa kwenye foleni na mambo mengine. Tunaweza kutumia nauli isiyobadilika na bei za chini zaidi. Bei halisi zinaweza kubadilika.

Njia za kusafiri

Jinsi ya kupata usafiri wa Uber kutoka uwanja wa ndege

Fungua App yako ili uitishe usafiri

Ukiwa tayari kutoka nje, fungua programu yako kisha uitishe usafiri. Chagua usafiri unaotoshea idadi ya wasafiri na mizigo mliyo nayo.

Fuata maelekezo katika App

Utapata maelekezo kuhusu eneo la kuchukua wasafiri moja kwa moja katika programu. Pia kunaweza kuwa na alama katika uwanja wa ndege.

Kutana na dereva wako

Nenda katika eneo la kuchukuliwa jinsi ilivyobainishwa katika App. Tafadhali kumbuka, eneo hilo huenda halitakuwa karibu kabisa na lango unaloondokea. Ikiwa humpati dereva wako, wasiliana naye kupitia App.

Vidokezo vya kuzingatia katika Uwanja wa Ndege wa Geneva

WiFi katika Uwanja wa Ndege wa Geneva

Huduma ya WiFi katika Uwanja wa Ndege wa Geneva inapatikana kwa wasafiri wote bila malipo kwa dakika 120. Pata namba ya kuthibitisha kwa SMS au kutoka katika dawati la kujihudumia la WiFi kisha uingie mtandaoni. Unaweza kununua vocha zaidi ikiwa utazidi muda wa dakika 120.

Maegesho katika Uwanja wa Ndege wa Geneva

Kuna maegesho ya aina nyingi katika Uwanja wa Ndege wa GVA, ikiwemo maegesho ya muda mrefu kwa wasafiri wengi na maegesho ya muda mfupi kwa ajili ya kushukisha na kuwachukua wasafiri.

Kuhifadhi mizigo katika Uwanja wa Ndege wa Geneva

Ukiwa GVA, unaweza kuacha mikoba yako katika ofisi ya mizigo, iwe ni katika makabati au kwenye kaunta. Unaweza kuzipata katika kituo cha Swiss Railways kilicho katika uwanja wa ndege, takribani mita 250 kutoka jengo la kituo kikuu, pitia njia yenye paa.

Maswali ambayo wasafiri wanauliza sana

Uber inapatikana katika Uwanja wa Ndege wa Geneva, kwa hivyo unaweza kufurahia usafiri wa starehe na uhakika popote unapotaka kwenda.

Ili kupata eneo la kuchukuliwa, angalia programu ya Uber baada ya kuitisha usafiri.

Hata kama safari si ndefu sana, ada za Uber kutoka na kwenda Uwanja wa Ndege wa Geneva zinaweza kuathiriwa na muda, foleni na masuala mengine. Angalia mfumo wa kukadiria nauli za Uber ili ufahamu makadirio ya nauli ya safari.

Muda wa kuchukuliwa unaweza kutofautiana kulingana na wakati, idadi ya madereva wanaopatikana na masuala mengine.

Maelezo zaidi

Unatumia mfumo wa Uber kuendesha gari?

Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kurahisisha huduma unayopokea katika viwanja vya ndege, zikiwemo sheria na kanuni za nchi husika.

Je, unaelekea uwanja tofauti wa ndege?

Unaweza kupelekwa na kuchukuliwa kutoka zaidi ya viwanja 500 vya ndege kote duniani.

Gundua vitu vya kufanya katika vituo vya Uwanja wa Ndege wa Geneva

Uber ni chaguo bora kwa wasafiri wanaowasili au kuondoka kwenye Uwanja wa Ndege wa Geneva. Uwanja wa Ndege wa Geneva ni mojawapo ya viwanja vya ndege vyenye shughuli nyingi zaidi nchini Uswizi na huhudumia zaidi ya wasafiri milioni 17 kila mwaka.

Unahudumiwa na mojawapo ya wasafirishaji wakuu barani Ulaya na ndio njia rahisi kufika Geneva, maeneo ya karibu na vituo vingi na sehemu nyingi za kupumzika ya Ufaransa, Uswizi na kimataifa. Isitoshe, Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Geneva unapatikana takribani kilomita 4 (maili 2.5) kaskazini mwa mji wa Geneva, jambo linalofanya kuwa rahisi kuufikia kwa usafiri wa umma, magari au hata Uber. Magari huchukua takribani dakika 20, kutegemea hali ya foleni, ilhali safari fupi kwenye treni kwenda uwanja wa ndege kutoka katikati ya mji huchukua dakika 6 tu.

Vituo katika GVA

Uwanja wa Ndege wa Geneva una vituo viwili vikuu vya wasafiri: Kituo cha 1 na Kituo cha 2. Kituo cha 1 hutumika sana, kikilinganishwa na cha 2—ambacho ndicho kituo asili cha uwanja huu—kinatumika tu wakati wa msimu wa baridi. Kwa hivyo, kina huduma chache kikilinganishwa na Kituo cha 1, lakini kina kituo cha treni. Kituo cha 1 kimegawanywa katika vituo 5 vidogo: A, B, C, D na F.

Migahawa kwenye Uwanja wa Ndege wa GVA

Kuna migahawa mingi kwenye Uwanja wa Ndege wa Geneva, kuanzia migahawa midogo hadi hoteli za kifahari, baa na vyumba vya chai. Vyakula kwenye Uwanja wa Ndege wa Geneva vinamfaa kila mtu.

Kusafiri kwenye Uwanja wa Ndege wa GVA

Unaweza kufikia maeneo mbalimbali kwenye uwanja wa ndege kwa miguu, isipokuwa Kituo cha 2, ambacho kiko kando na uwanja mkuu. Unaweza kusafiri kati ya vituo hivi 2 kwa basi.

Mambo ya kufanya kwenye Uwanja wa Ndege wa GVA

Kuna maduka mengi ya kufanya ununuzi kwenye Uwanja wa Ndege wa Geneva, yenye bidhaa zisizolipishwa kodi pamoja na maduka mengi ya nchini na ya kimataifa. Kuna huduma 2 za VIP ambazo zinawawezesha wateja kufikia sebule na kuwaongoza katika sehemu za ukaguzi wa usalama. Huduma za siha bora zinapatikana kwenye uwanja wa ndege, huku kukiwa na vyumba vya kutafakari na vya kuoga. Isitoshe, wasafiri wanaweza kunufaika kwa kutumia maeneo 2 ya watoto kucheza, maeneo yaliyotengewa shughuli za biashara na vyumba vya mikutano.

Kubadilisha sarafu kwenye Uwanja wa Ndege wa GVA

Kuna afisi kadhaa za kubadilisha sarafu katika maeneo ya wanaowasili na wanaoondoka kwenye uwanja wa ndege. Mitambo ya benki pia inapatikana kwenye uwanja wa ndege, mingi ikiwapa wasafiri fursa ya kutoa pesa katika sarafu mbalimbali.

Hoteli karibu na Uwanja wa Ndege wa GVA

Takribani hoteli 10 zinapatikana karibu na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Geneva, jambo linazozifanya kuwa chaguo bora kwa wasafiri walio kwenye mapumziko ya muda mfupi na wanaowasili jioni. Utapata hoteli za gharama aina zote katikati mwa mji wa Geneva. Kuna pia chaguo za usafiri kwenda kwenye vituo vya kuteleza kwenye theluji na vyumba maalum katika eneo hilo, iwe nchini Ufaransa au Uswizi.

Maeneo ya kuzuru karibu na GVA

  • Jet d’Eau (Chemchemi ya Maji)
  • Ziwa la Geneva
  • Mont Salève
  • Old Town
  • Saint Pierre Cathedral (St. Peter’s Cathedral)

Pata maelezo zaidi kuhusu GVA hapa.

Facebook
Instagram
Twitter