Please enable Javascript
Ruka uende katika maudhui ya msingi

Uwanja wa Ndege wa Frankfurt am Main (FRA)

Je, unatafuta mbinu mbadala ya usafiri ambayo si basi la kawaida la Uwanja wa Ndege wa Frankfurt au teksi? Iwe unasafiri kutoka Uwanja wa Ndege wa Frankfurt hadi katikati ya jiji au kutoka Kleinmarkthalle hadi Uwanja wa Ndege wa Frankfurt, fika unakoenda ukitumia programu ya Uber unayoijua tayari. Omba gari la kukupeleka na kukurudisha kutoka FRA kwa kubofya kitufe.

Frankfurt, 60547
+49 180-6-3724636

search
Where from?
Navigate right up
search
Where to?

Request a ride around the world

Bofya kitufe sasa na upate usafiri wa uwanja wa ndege katika zaidi ya vituo vikuu 700.

Safiri kama mkazi

Acha programu na dereva wako washughulikie maelezo ya kina ili usisumbuke kutafuta maelekezo katika mji usiofahamu.

Safiri bila wasiwasi ukitumia Uber

Pata vipengele unavyovipenda, ikiwemo bei za wakati halisi na malipo ya kielektroniki, hata ukiwa ugenini.

Ways to ride in the area

Pickup at Uwanja wa Ndege wa Frankfurt am Main (FRA)

Fungua programu yako ili uombe safari

Ukiwa tayari, fungua programu ya Uber ili uombe safari ya kuelekea mahali unakoenda. Chagua chaguo la usafiri wa uwanja wa ndege wa FRA linalokidhi mahitaji ya idadi ya wasafiri na mizigo yenu.

Fuata maelekezo kwenye programu

Utapata maelekezo kuhusu maeneo ya kuchukua wasafiri ya Uwanja wa Ndege wa Frankfurt moja kwa moja kwenye programu. Maeneo ya kuchukua wasafiri yanaweza kutofautiana kulingana na kituo. Ishara za maeneo ya kuchukua wasafiri wanaosafiri pamoja zinaweza pia kupatikana katika Uwanja wa Ndege wa Frankfurt am Main.

Kutana na dereva wako

Nenda kwenye eneo lako la kuchukuliwa la FRA kama ilivyobainishwa kwenye programu. Tafadhali kumbuka: eneo hili huenda lisiwe kwenye lango la kutoka lililo karibu zaidi nawe. Jina la dereva wako, nambari ya leseni na rangi ya gari itaonyeshwa kwenye programu. Thibitisha gari lako kabla ya kuingia. Ikiwa humpati dereva wako, wasiliana naye kupitia programu.

Top questions from riders

  • Uber inapatikana katika Uwanja wa Ndege wa Frankfurt, kwa hivyo unaweza kufurahia usafiri wa starehe na uhakika popote unapotaka kwenda.

  • Maeneo ya kuchukua wasafiri wa Uber katika uwanja wa ndege yanaweza kubadilika. Ili kupata eneo la kuchukuliwa, angalia App ya Uber baada ya kuitisha usafiri.

  • Ada za safari za kwenda au kutoka katika Uwanja wa Ndege wa Frankfurt zinaweza kuathiriwa na wakati, foleni na masuala mengine. Angalia App ya Uber kwa maelezo yanayohusu nauli ya safari.

  • Unapoitisha usafari, App itakupa makadirio ya muda ambao dereva atachukua kufika katika eneo la kuchukua wasafiri.

More information

  • Unaendesha gari ukitumia Uber?

    Kuanzia eneo la kuwachukua wasafiri hadi kufuata sheria na kanuni za mahali husika, fahamu jinsi ya kufanya safari zako za uwanja wa ndege ziwe bora zaidi.

  • Unaelekea uwanja tofauti wa ndege?

    Unaweza kushushwa na kuchukuliwa kutoka zaidi ya viwanja 700 vya ndege kote ulimwenguni.

1/2

Maelezo kwa wageni kwenye Uwanja wa Ndege wa Frankfurt

Uwanja wa Ndege wa Frankfurt am Main ulifunguliwa 1936 na umeendelea kuwa mojawapo ya viwanja vikuu vya ndege Ujerumani, huku ukiwahudumia takribani wasafiri milioni 70 kila mwaka. Ni kituo muhimu cha usafiri barani Ulaya na ni kitovu kikuu chenye ajira nyingi katika sehemu moja nchini Ujerumani, na kinawaajiri watu 81,000 kwenye kampuni na mashirika 450. Uwanja huu wa ndege upo kilomita 12 (maili 7) upande wa kusini mashariki mwa Frankfurt, kwa hivyo inachukua takribani dakika 15 kutoka katikati ya jiji hadi eneo la kushukishia wasafiri.

Vituo katika Uwanja wa Ndege wa Frankfurt

Uwanja wa Ndege wa Frankfurt una vituo 2, Kituo cha 1 na Kituo cha 2, usafiri kati ya vituo hivyo ni kwa basi au treni ya SkyLine. Safari za kitaifa na za kimataifa hufanyika katika vituo vyote viwili, kwa hivyo ni muhimu kuangalia kituo chako cha kuondoka kwa makini. Uwanja wa Ndege wa Frankfurt ndio una Kituo cha Daraja la Kwanza la Lufthansa, kituo hiki ni mahususi kwa wasafiri wa daraja la kwanza wa shirika la ndege la Lufthansa.

Migahawa katika Uwanja wa Ndege wa Frankfurt

Iwe unapenda staftahi ya kujichagulia, chakula cha mchana kwa haraka au kuketi na kufurahia chakula cha jioni, Uwanja wa Ndege wa Frankfurt utakidhi matamanio yako. Maeneo mengi ya vyakula yana aina zote za vyakula, iwe ni kitafunwa cha haraka au mlo kamili kwa walio na muda zaidi. Mbali na vyakula vya kawaida kama vile sandwichi, supu, saladi, vinywaji baridi na moto, smuthi, sharubati na vitobosha, wasafiri wanaweza kufurahia milo kadhaa kutoka duniani kote vikiwemo vya Italia, Asia bila kusahau vyakula vya kienyeji vya Ujerumani. Kuna vyakula vinavyowafaa walamboga na vilevile visivyo na gluteni.

Maduka katika Uwanja wa Ndege wa Frankfurt

Kwa wasafiri ambao hujiliwaza kwa ununuzi, Uwanja wa Ndege wa FRA una sehemu nyingi. Uwanja huu wa ndege una sehemu ya bidhaa zisizotozwa kodi, yenye maduka yanayouza vitu kwa bei nafuu vikiwemo marashi, manukato ya kutumia baada ya kunyoa ndevu, miwani ya jua, mapambo, tamutamu, bia, mvinyo na vileo vinginevyo. Kadhalika kuna maduka yanayouza bidhaa za kifahari za fashoni, viatu, vifaa vya umeme, mapambo, magazeti, majarida, vitabu, vifaa vya tiba na dawa, na vitu vingine unavyoweza kuhitaji katika dakika za mwisho safarini. Vilevile wasafiri wanaweza kujinunulia dafina kama vile mlo wa mayai ya samaki na vyakula vya kienyeji vya Kijerumani.

Kumbi katika Uwanja wa Ndege wa Frankfurt

Frankfurt ina kumbi kadhaa kubwa, baadhi ya kumbi hizo ni maalum kwa wanaosafiri mara kwa mara au wanaosafiri katika daraja la biashara. Hata hivyo, kuna kumbi ambazo ni wazi kwa wasafiri wote ilimradi walipie. Katika kumbi hizo, unaweza kutulia kabla ya safari na ufurahie viti vya kujimwaya, vinywaji baridi au moto, WiFi, televisheni na magazeti.

Huduma katika FRA

Kuna huduma mbalimbali katika Uwanja wa Ndege wa Frankfurt ili kuhakikisha kwamba wasafiri wote wanafurahia usafiri. Kuna madawati ya kufanyia kazi kwa ajili ya wanaosafiri kikazi au wanaotaka kutumia muda wao katika uwanja wa ndege wakiperuzi mtandao. Familia zinazosafiri pamoja na watoto wachanga zinaweza kufurahia sehemu za watoto kuchezea katika vituo vyote viwili, pia kuna vyumba mahususi kwa ajili ya kuwanyonyesha na kuwabadilisha watoto nepi. Kwa wasafiri wanaosubiri kwa muda mrefu, kuna kumbi kadhaa za sinema za Movie Worlds katika Kituo cha 1, ambapo wanaweza kutazama filamu, filamu za hali halisi na misimu pendwa ya vipindi vya TV.

Hoteli katika Uwanja wa Ndege wa Frankfurt

Kuna hoteli kadhaa katika Uwanja wa Ndege wa Frankfurt zinazotoa makazi kwa gharama zinazokidhi bajeti mbalimbali. Baadhi yazo zina njia za kutembea moja kwa moja kuelekea katika vituo vya wasafiri. Katika maeneo yaliyo karibu na uwanja wa ndege, hasa Rüsselsheim na Langen, kuna chaguo nyingi za makazi pia. Kwa sababu kituo cha Frankfurt hakipo mbali sana, wasafiri ambao hawana haraka ya kuwahi ndege wanaweza kuchagua aina nyingi za hoteli na vyumba vinavyopatikana katika maeneo hayo.

Maeneo ya kuzuru karibu na Uwanja wa Ndege wa Frankfurt

Frankfurt ni kitovu cha kifedha, kwa hivyo ni maarufu miongoni mwa wanaosafiri kibiashara, pia ina vivutio kadhaa vya kuona kama vile sanaa, mijengo na makumbusho. Baadhi ya vivutio vya Frankfurt ni:

  • Kaiserdom (Kanisa Kuu la Kifalme)
  • Soko la Kleinmarkthalle
  • Makavazi ya historia asili
  • Mbuga ya Römerberg
  • Makavazi ya sanaa ya Städel

Pata maelezo zaidi kuhusu FRA hapa.

Facebook
Instagram
Twitter
YouTube

This page contains information from third-party websites that are not under the control of Uber and that may be periodically changed or updated. Any information included on this page that is not directly related to Uber or its operations is for informational purposes only and in no way shall be relied upon, or interpreted or construed to create any warranties of any kind, either express or implied, regarding the information contained herein. Certain requirements and features vary by country, region, and city.