Ruka uende katika maudhui ya msingi

Uwanja wa Ndege wa Frankfurt am Main (FRA)

Iwe unatoka katika Uwanja wa Ndege wa Frankfurt kuelekea katikati mwa jiji au unatoka Kleinmarkthalle kwenda Uwanja wa Ndege wa Frankfurt, itegemee App ya Uber kufika utakako.

Frankfurt 60547 Germany
+49 180-6-3724636

Njia bora zaidi ya kusafiri

Itisha usafiri kote ulimwenguni

Bonyeza tu kitufe ili upate usafiri wa angani katika zaidi ya viwanja vikuu 500.

Safiri kama mwenyeji

Acha App na dereva wako ashughulikie masuala ya kina ili usisumbuke kutafuta maelekezo katika jiji ambapo wewe ni mgeni.

Safiri bila wasiwasi kwa kutumia Uber

Pata vipengele unavyovipenda, ikiwa ni pamoja na bei zinazooneshwa moja kwa moja na uwezo wa kulipa bila pesa taslimu, hata ukiwa ugenini.

Aina za usafiri ukiwa eneo husika

 • UberX

  1-3

  Affordable everyday trips

 • Premium

  1-3

  High-end trips with professional drivers

 • Green

  1-3

  Emission-free, affordable, everyday rides

 • Taxi

  1-3

  Local taxi-cabs at the tap of a button

1/4

Kupata gari kwenye Uwanja wa Ndege wa Frankfurt

Fungua App yako ili uitishe usafiri

Ukiwa tayari kutoka nje, fungua App yako kisha uitishe usafiri. Chagua aina ya gari linalofaa ukubwa wa kikundi chako na mizigo mnayohitaji kubebewa.

Fuata maelekezo katika App

Utapata maelekezo kuhusu eneo la kuchukua wasafiri moja kwa moja katika App. Pia kunaweza kuwa na mabango katika uwanja wa ndege.

Kutana na dereva wako

Nenda katika eneo la kuchukuliwa jinsi ilivyobainishwa katika App. Tafadhali kumbuka, eneo hilo huenda halitakuwa karibu kabisa na lango unaloondokea. Ikiwa humpati dereva wako, wasiliana naye kupitia App.

Vidokezo kwa ajili ya usafiri salama katika Uwanja wa Ndege wa Frankfurt

WiFi katika Uwanja wa Ndege wa Frankfurt

Wasafiri wamekaribishwa kufurahia WiFi bila malipo wakati wowote katika Uwanja wa Ndege wa Frankfurt. Ili kupata huduma, tafuta mtandao wa Frankfurt-Airport, weka anwani yako ya barua pepe, kisha ukubali vigezo na masharti. Kisha bonyeza Inayofuata halafu Uanze kuperuzi.

Kuhifadhi mizigo katika Uwanja wa Ndege wa Frankfurt

Kuna maeneo matatu ya kuhifadhi mizigo katika Uwanja wa Ndege wa Frankfurt yanayopatikana katika vituo vyote. Maeneo hayo yanaruhusu wasafiri kuhifadhi mizigo kwa muda usiopita miezi 3. Vituo hivyo pia vina huduma za kuminya mizigo mikubwa au iliyotanuka.

Maegesho katika Uwanja wa Ndege wa Frankfurt

Maeneo ya maegesho kadhaa yanapatikana katika Uwanja wa Ndege wa Frankfurt, kwa muda mfupi, muda mrefu, maegesho ya kibiashara na pia eneo la kushukisha.

Maswali ambayo wasafiri wanauliza sana

 • Uber inapatikana katika Uwanja wa Ndege wa Frankfurt, kwa hivyo unaweza kufurahia usafiri wa starehe na uhakika popote unapotaka kwenda.

 • Maeneo ya kuchukua wasafiri wa Uber katika uwanja wa ndege yanaweza kubadilika. Ili kupata eneo la kuchukuliwa, angalia App ya Uber baada ya kuitisha usafiri.

 • Ada za safari za kwenda au kutoka katika Uwanja wa Ndege wa Frankfurt zinaweza kuathiriwa na wakati, foleni na masuala mengine. Angalia App ya Uber kwa maelezo yanayohusu nauli ya safari.

 • Unapoitisha usafari, App itakupa makadirio ya muda ambao dereva atachukua kufika katika eneo la kuchukua wasafiri.

Maelezo zaidi

Je, unaelekea uwanja tofauti wa ndege?

Unaweza kupelekwa na kuchukuliwa kutoka zaidi ya viwanja 600 vya ndege kote duniani.

Maelezo kwa wageni kwenye Uwanja wa Ndege wa Frankfurt

Uwanja wa Ndege wa Frankfurt am Main ulifunguliwa 1936 na umeendelea kuwa mojawapo ya viwanja vikuu vya ndege Ujerumani, huku ukiwahudumia takribani wasafiri milioni 70 kila mwaka. Ni kituo muhimu cha usafiri barani Ulaya na ni kitovu kikuu chenye ajira nyingi katika sehemu moja nchini Ujerumani, na kinawaajiri watu 81,000 kwenye kampuni na mashirika 450. Uwanja huu wa ndege upo kilomita 12 (maili 7) upande wa kusini mashariki mwa Frankfurt, kwa hivyo inachukua takribani dakika 15 kutoka katikati ya jiji hadi eneo la kushukishia wasafiri.

Vituo katika Uwanja wa Ndege wa Frankfurt

Uwanja wa Ndege wa Frankfurt una vituo 2, Kituo cha 1 na Kituo cha 2, usafiri kati ya vituo hivyo ni kwa basi au treni ya SkyLine. Safari za kitaifa na za kimataifa hufanyika katika vituo vyote viwili, kwa hivyo ni muhimu kuangalia kituo chako cha kuondoka kwa makini. Uwanja wa Ndege wa Frankfurt ndio una Kituo cha Daraja la Kwanza la Lufthansa, kituo hiki ni mahususi kwa wasafiri wa daraja la kwanza wa shirika la ndege la Lufthansa.

Migahawa katika Uwanja wa Ndege wa Frankfurt

Iwe unapenda staftahi ya kujichagulia, chakula cha mchana kwa haraka au kuketi na kufurahia chakula cha jioni, Uwanja wa Ndege wa Frankfurt utakidhi matamanio yako. Maeneo mengi ya vyakula yana aina zote za vyakula, iwe ni kitafunwa cha haraka au mlo kamili kwa walio na muda zaidi. Mbali na vyakula vya kawaida kama vile sandwichi, supu, saladi, vinywaji baridi na moto, smuthi, sharubati na vitobosha, wasafiri wanaweza kufurahia milo kadhaa kutoka duniani kote vikiwemo vya Italia, Asia bila kusahau vyakula vya kienyeji vya Ujerumani. Kuna vyakula vinavyowafaa walamboga na vilevile visivyo na gluteni.

Maduka katika Uwanja wa Ndege wa Frankfurt

Kwa wasafiri ambao hujiliwaza kwa ununuzi, Uwanja wa Ndege wa FRA una sehemu nyingi. Uwanja huu wa ndege una sehemu ya bidhaa zisizotozwa kodi, yenye maduka yanayouza vitu kwa bei nafuu vikiwemo marashi, manukato ya kutumia baada ya kunyoa ndevu, miwani ya jua, mapambo, tamutamu, bia, mvinyo na vileo vinginevyo. Kadhalika kuna maduka yanayouza bidhaa za kifahari za fashoni, viatu, vifaa vya umeme, mapambo, magazeti, majarida, vitabu, vifaa vya tiba na dawa, na vitu vingine unavyoweza kuhitaji katika dakika za mwisho safarini. Vilevile wasafiri wanaweza kujinunulia dafina kama vile mlo wa mayai ya samaki na vyakula vya kienyeji vya Kijerumani.

Kumbi katika Uwanja wa Ndege wa Frankfurt

Frankfurt ina kumbi kadhaa kubwa, baadhi ya kumbi hizo ni maalum kwa wanaosafiri mara kwa mara au wanaosafiri katika daraja la biashara. Hata hivyo, kuna kumbi ambazo ni wazi kwa wasafiri wote ilimradi walipie. Katika kumbi hizo, unaweza kutulia kabla ya safari na ufurahie viti vya kujimwaya, vinywaji baridi au moto, WiFi, televisheni na magazeti.

Huduma katika FRA

Kuna huduma mbalimbali katika Uwanja wa Ndege wa Frankfurt ili kuhakikisha kwamba wasafiri wote wanafurahia usafiri. Kuna madawati ya kufanyia kazi kwa ajili ya wanaosafiri kikazi au wanaotaka kutumia muda wao katika uwanja wa ndege wakiperuzi mtandao. Familia zinazosafiri pamoja na watoto wachanga zinaweza kufurahia sehemu za watoto kuchezea katika vituo vyote viwili, pia kuna vyumba mahususi kwa ajili ya kuwanyonyesha na kuwabadilisha watoto nepi. Kwa wasafiri wanaosubiri kwa muda mrefu, kuna kumbi kadhaa za sinema za Movie Worlds katika Kituo cha 1, ambapo wanaweza kutazama filamu, filamu za hali halisi na misimu pendwa ya vipindi vya TV.

Hoteli katika Uwanja wa Ndege wa Frankfurt

Kuna hoteli kadhaa katika Uwanja wa Ndege wa Frankfurt zinazotoa makazi kwa gharama zinazokidhi bajeti mbalimbali. Baadhi yazo zina njia za kutembea moja kwa moja kuelekea katika vituo vya wasafiri. Katika maeneo yaliyo karibu na uwanja wa ndege, hasa Rüsselsheim na Langen, kuna chaguo nyingi za makazi pia. Kwa sababu kituo cha Frankfurt hakipo mbali sana, wasafiri ambao hawana haraka ya kuwahi ndege wanaweza kuchagua aina nyingi za hoteli na vyumba vinavyopatikana katika maeneo hayo.

Maeneo ya kuzuru karibu na Uwanja wa Ndege wa Frankfurt

Frankfurt ni kitovu cha kifedha, kwa hivyo ni maarufu miongoni mwa wanaosafiri kibiashara, pia ina vivutio kadhaa vya kuona kama vile sanaa, mijengo na makumbusho. Baadhi ya vivutio vya Frankfurt ni:

 • Kaiserdom (Kanisa Kuu la Kifalme)
 • Soko la Kleinmarkthalle
 • Makavazi ya historia asili
 • Mbuga ya Römerberg
 • Makavazi ya sanaa ya Städel

Pata maelezo zaidi kuhusu FRA hapa.

Facebook
Instagram
Twitter
YouTube

Ukurasa huu una taarifa kutoka kwenye tovuti za washirika wengine ambazo hazisimamiwi na Uber na zinaweza kugeuzwa au kubadilishwa mara kwa mara. Maelezo yoyote yaliyojumuishwa kwenye ukurasa huu ambayo hayahusiani moja kwa moja na Uber au kazi zake yanatumika kuarifu tu na hayafai kutegemewa, au kuchukuliwa au kufasiliwa kwa namna inayoweka dhamana ya aina yoyote, iwe ya moja kwa moja au inayokisiwa, kuhusu maelezo yaliyo hapa. Baadhi ya masharti na vipengele hutofautiana kutegemea nchi, eneo na jiji. Ofa ya punguzo inawalenga watumiaji wapya pekee. Huwezi kutumia ofa hii pamoja na ofa nyinginezo na haiwezi kutumiwa katika bakshishi. Inapatikana kwa muda mfupi. Vigezo na masharti ya ofa vinaweza kubadilika.

Viungo kwa tovuti za nje vimeandaliwa kipekee kwa wageni kutumia wanavyotaka. Kupeleka viungo kwa tovuti nyingine itakuwa kwa hiari yako na Uber haitakubali dhima kwa tovuti zilizounganishwa au maudhui yazo.