Ruka uende katika maudhui ya msingi

Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dubia (DXB)

Iwe unasafiri kuelekea katikati ya jiji kutoka Uwanja wa Ndege wa Dubai au kutoka katikati ya jiji kuelekea Uwanja wa Ndege wa Dubai, iamini Uber kukufikisha unakoenda.

7938+77 Dubai - United Arab Emirates
+971 4-224-5555

Njia bora zaidi ya kusafiri

Itisha usafiri kote ulimwenguni

Bonyeza tu kitufe ili upate usafiri wa angani katika zaidi ya viwanja vikuu 500.

Safiri kama mwenyeji

Acha App na dereva wako ashughulikie masuala ya kina ili usisumbuke kutafuta maelekezo katika jiji ambapo wewe ni mgeni.

Safiri bila wasiwasi kwa kutumia Uber

Pata vipengele unavyovipenda, ikiwa ni pamoja na bei zinazooneshwa moja kwa moja na uwezo wa kulipa bila pesa taslimu, hata ukiwa ugenini.

Aina za usafiri ukiwa eneo husika

 • Black

  1-2

  Premium trips in luxury cars

 • Select

  1-2

  Premium rides in high-end cars

 • UberXL

  1-4

  Affordable rides for groups up to 4

1/3

Jinsi ya kupata usafiri wa Uber kutoka uwanja wa ndege

Fungua App yako ili uitishe usafiri

Ukishakuwa tayari, fungua programu yako na uitishe usafiri. Chagua usafiri unaotoshea idadi ya wasafiri na mizigo mliyo nayo.

Fuata maelekezo katika App

Utapata maelekezo kuhusu eneo la kuchukua wasafiri moja kwa moja katika programu. Pia kunaweza kuwa na alama katika uwanja wa ndege.

Kutana na dereva wako

Nenda katika eneo la kuchukuliwa jinsi ilivyobainishwa katika App. Tafadhali kumbuka, eneo hilo huenda halitakuwa karibu kabisa na lango unaloondokea. Ikiwa humpati dereva wako, wasiliana naye kupitia App.

Vidokezo vya kuzingatia katika Uwanja wa Ndege wa Dubai

WiFi katika Uwanja wa Ndege Dubai

Huduma ya WiFi bora na yenye kasi ya juu inapatikana bila malipo katika maeneo yote ya Uwanja wa Ndege wa Dubai. Ikiwa huna simu, unaweza kupata huduma ya intaneti katika vibanda vilivyounganishwa na Global Link na Connect.

Maegesho katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dubai

Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dubia una chaguo mbalimbali za maegesho ili kukidhi mahitaji ya wasafiri wote. Vituo vya 1 na 2 vina nafasi za maegesho ya Economy na Premium katika umbali tofauti tofauti kutoka kwenye uwanja wa ndege.

Kubadilisha sarafu katika Uwanja wa Ndege wa Dubai

Unaweza kupata vituo vingi vya kubadilisha sarafu katika Uwanja wa Ndege wa DXB. Kila kituo kinabadilisha sarafu mbalimbali ili kuhakikisha kwamba unawasili ukiwa na aina za hela zinazofaa.

Maswali ambayo wasafiri wanauliza sana

 • Uber inapatikana katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dubai, kwa hivyo unaweza kufurahia usafiri wa starehe na uhakika popote unapotaka kwenda.

 • Ili kupata eneo la kuchukuliwa, angalia programu ya Uber baada ya kuitisha usafiri.

 • Hata kama safari si ndefu sana, ada za Uber kutoka na kwenda Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dubai zinaweza kuathiriwa na muda, foleni na masuala mengine. Angalia mfumo wa kukadiria nauli za Uber ili ufahamu makadirio ya nauli ya safari.

 • Muda wa kuchukuliwa unaweza kutofautiana kulingana na wakati, idadi ya madereva wanaopatikana na masuala mengine.

Maelezo zaidi

Je, unaelekea uwanja tofauti wa ndege?

Unaweza kupelekwa na kuchukuliwa kutoka zaidi ya viwanja 600 vya ndege kote duniani.

Taarifa kwa wasafiri kuhusu vituo katika Uwanja wa Ndege wa Dubai

Uber ni chaguo bora kwa wasafiri wanaowasili au kuondoka kwenye Uwanja wa Ndege wa DXB. Uwanja wa Ndege wa Dubai ndio wenye shughuli nyingi zaidi ulimwenguni kote. Una vifaa vya kifahari kwa wageni kutoka kote ulimwenguni. Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dubai unapatikana katika wilaya ya Al Garhoud, takribani kilomita 5 (maili 3) kutoka katikati mwa mji. Kwa kuwa ni uwanja mkuu wa ndege unaohudumia Dubai, ni chaguo bora kwa mtu yeyote anayesafiri mjini Dubai. Pia unafaa wale wanaobadilisha ndege.

Vituo katika Uwanja wa Ndege wa Dubai

Uwanja wa Ndege wa Dubai una vituo 3 vikuu vya wasafiri: Kituo cha 1 , 2 na 3. Kituo cha 1 ndicho chenye shughuli nyingi—kinatumika na mashirika mengi ya ndege—ilhali Kituo cha 2 hutumika sana katika safari za kimaeneo.

Kituo cha 1 kwenye Uwanja wa Ndege wa DXB

 • Mashirika yote ya kimataifa ya ndege

Kituo cha 2 kwenye Uwanja wa Ndege wa DXB

 • flydubai
 • Mashirika mengine ya maeneo na ya kimataifa ya ndege

Kituo cha 3 kwenye Uwanja wa Ndege wa DXB

 • Emirates
 • flydubai
 • Qantas

Migahawa kwenye Uwanja wa Ndege wa Dubai

Migahawa kwenye Uwanja wa Ndege wa Dubai ina kila unachohitaji, vyakula na vinywaji bora. Ina zaidi ya maduka 80 ya vyakula na vinywaji. Unaweza kufurahia vyakula kutoka kote ulimwenguni. Mgahawa wa Butler’s Chocolate unawafaa wanaotaka vyakula vya sukari, ilhali Mgahawa wa Chowking Orient unawafaa wanaotaka vyakula vya bara la Asia.

Kusafiri kwenye Uwanja wa Ndege wa DXB

Kuna basi linalosafirisha wasafiri saa yoyote kati ya Kituo cha 1 na 3. Unaweza pia kutumia treni kusafiri kutoka kituo kimoja hadi kingine.

.

Mambo ya kufanya DXB

Maduka ya bidhaa zisizotozwa kodi kwenye Uwanja wa Ndege wa Dubai, ni bora kwa ununuzi rejareja. Yana bidhaa mbalimbali kwenye Uwanja wa Ndege wa Dubai, zikiwemo bidhaa maarufu, vifaa vya kisanaa na vitu unavyohitaji katika safari. Utapata unachotaka kama vile vito, hedaya, vipodozi, mavazi na zaidi.

Mabafu katika Uwanja wa Ndege wa Dubai

Mabafu zaidi yanapatikana kati ya Milango ya C18 na C22 na Milango ya B13 na B19 katika Kituo cha 3 kwa yeyote anayetaka kuoga kabla ya safari. Ni muhimu kuondoa uchafu na kuwa freshi katika safari inayofuata.

Uhifadhi wa mizigo katika Uwanja wa Ndege wa Dubai

Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dubai una chaguo mbalimbali za kuhifadhi mizigo kwa muda mfupi katika Vituo vya 1 na 3. Kwa kulipia ada ndogo, unaweza kuhifadhi mikoba yako kwa muda wa saa 12. Huduma ya kuhifadhi mizigo haipatikani kwenye Kituo cha 2. Huduma ya kufunga mzigo na ya uchukuzi pia inapatikana, ili kukuwezesha kudhibiti mizigo mizito.

Kubadilisha sarafu kwenye DXB

Kwa kuwa ni uwanja wa ndege wenye shughuli nyingi kote ulimwenguni, kuna mashirika mbalimbali ya kubadilisha sarafu kwenye Uwanja wa Ndege wa DXB. Kila kituo kina vibanda vya kubadilisha sarafu mbalimbali ili kuhakikisha una sarafu inayofaa kokote unakoenda.

Hoteli karibu na Uwanja wa Ndege wa Dubai

Hoteli mbalimbali zinapatikana kwenye Vituo vya 1 na 3 katika Uwanja wa Ndege wa Dubai, jambo linalozifanya ziwe bora kwa mapumziko katikati mwa safari. Kuna Hoteli nyingi karibu na uwanja huu wa ndege na wasafiri wanaweza kuweka nafasi ya vyumba vya kulala mjini, ambako kunafikiwa kwa urahisi kupitia Uber.

Maeneo ya kuzuru karibu na Uwanja wa Ndege wa Dubai

Ikiwa unasubiri ndege nyingine katika Uwanja wa Ndege wa DXB na una muda wa zaidi ya saa 6, kuna maeneo mengi ya kuzuru karibu na Uwanja wa Ndege wa Dubai, yakiwemo:

 • Burj Khalifa
 • Fuo za Dubai
 • Chemichemi ya Dubai
 • The Dubai Mall

Pata maelezo zaidi kuhusu Uwanja wa Ndege wa Dubaihapa.

Facebook
Instagram
Twitter

Ukurasa huu una taarifa kutoka kwenye tovuti za washirika wengine ambazo hazisimamiwi na Uber na zinaweza kugeuzwa au kubadilishwa mara kwa mara. Maelezo yoyote yaliyojumuishwa kwenye ukurasa huu ambayo hayahusiani moja kwa moja na Uber au kazi zake yanatumika kuarifu tu na hayafai kutegemewa, au kuchukuliwa au kufasiliwa kwa namna inayoweka dhamana ya aina yoyote, iwe ya moja kwa moja au inayokisiwa, kuhusu maelezo yaliyo hapa. Baadhi ya masharti na vipengele hutofautiana kutegemea nchi, eneo na jiji. Ofa ya punguzo inawalenga watumiaji wapya pekee. Huwezi kutumia ofa hii pamoja na ofa nyinginezo na haiwezi kutumiwa katika bakshishi. Inapatikana kwa muda mfupi. Vigezo na masharti ya ofa vinaweza kubadilika.