Ruka uende katika maudhui ya msingi

Uwanja wa Ndege wa Dublin (DUB)

Iwe unasafiri kuelekea katikati ya jiji kutoka Uwanja wa Ndege wa Dublin au kutoka katikati ya jiji kuelekea Uwanja wa Ndege wa Dublin, iamini Uber kukufikisha unakoenda.

CQG2+H2 Collinstown, County Dublin, Ireland
+353 1-814-1111

Njia bora zaidi ya kusafiri

Itisha usafiri kote ulimwenguni

Bonyeza tu kitufe ili upate usafiri wa angani katika zaidi ya viwanja vikuu 500.

Safiri kama mwenyeji

Acha App na dereva wako ashughulikie masuala ya kina ili usisumbuke kutafuta maelekezo katika jiji ambapo wewe ni mgeni.

Safiri bila wasiwasi kwa kutumia Uber

Pata vipengele unavyovipenda, ikiwa ni pamoja na bei zinazooneshwa moja kwa moja na uwezo wa kulipa bila pesa taslimu, hata ukiwa ugenini.

Aina za usafiri ukiwa eneo husika

 • Taxi

  1-3

  Taxi without the hassle

 • Black

  1-3

  Discreet executive quality

1/2

Jinsi ya kupata usafiri wa Uber kutoka uwanja wa ndege

Fungua App yako ili uitishe usafiri

Ukishakuwa tayari, fungua programu yako na uitishe usafiri. Chagua usafiri unaotoshea idadi ya wasafiri na mizigo mliyo nayo.

Fuata maelekezo katika App

Utapata maelekezo kuhusu eneo la kuchukua wasafiri moja kwa moja katika programu. Pia kunaweza kuwa na alama katika uwanja wa ndege.

Kutana na dereva wako

Nenda katika eneo la kuchukuliwa jinsi ilivyobainishwa katika App. Tafadhali kumbuka, eneo hilo huenda halitakuwa karibu kabisa na lango unaloondokea. Ikiwa humpati dereva wako, wasiliana naye kupitia App.

Vidokezo na ushauri wa kuzingatia katika Uwanja wa Ndege wa Dublin

WiFi katika Uwanja wa Ndege wa Dublin

Hutatozwa wala kupimiwa WiFi katika Uwanja wa Ndege wa Dublin. Unachohitaji tu kufanya ni kujiunga na mtandao na kuanza kuvinjari. Hakuna haja ya kujisajili au kuingia katika akaunti.

Maegesho ya uwanja wa ndege wa Dublin

Uwanja wa Ndege wa Dublin una maegesho ya muda mfupi na ya muda mrefu. Maegesho ya muda mfupi katika Uwanja wa Ndege wa Dublin yapo umbali wa dakika chache tu kutoka sehemu ya wanaowasili na wanaoondoka, pia kuna takribani nafasi 18,600 za maegesho ya muda mrefu.

Kuhifadhi mizigo katika Uwanja wa Ndege wa Dublin

Unaweza kuweka mzigo wako katika huduma ya Excess Baggage kwenye ukumbi wa wanaowasili katika Kituo cha 1, ili mzigo uwe salama ukihamishwa katika viwanja vya ndege. Katika sehemu hii unaweza pia kupokea huduma za kufungasha mikoba.

Maswali ambayo wasafiri wanauliza sana

 • Uber inapatikana katika Uwanja wa Ndege wa Dublin, kwa hivyo unaweza kufurahia usafiri wa starehe na uhakika popote unapotaka kwenda.

 • Ili kupata eneo la kuchukuliwa, angalia programu ya Uber baada ya kuitisha usafiri.

 • Hata kama safari si ndefu sana, ada za Uber kutoka na kwenda Uwanja wa Ndege wa Dublin zinaweza kuathiriwa na muda, foleni na masuala mengine. Ada za uwanja wa ndege na maegesho pia zinaweza kuongezwa kwenye nauli yako kamili ya safari.

 • Muda wa kuchukuliwa unaweza kutofautiana kulingana na wakati, idadi ya madereva wanaopatikana na masuala mengine. Mara baada ya kuitisha usafiri, angalia programu ili uone kadirio la muda wa kusubiri.

Maelezo zaidi

Je, unaelekea uwanja tofauti wa ndege?

Unaweza kupelekwa na kuchukuliwa kutoka zaidi ya viwanja 600 vya ndege kote duniani.

Vituo katika Uwanja wa Ndege wa Dublin

Uber ni chaguo bora kwa wasafiri wanaowasili au kuondoka kwenye Uwanja wa Ndege wa DUB. Uwanja wa Ndege wa Dublin ni uwanja wa kimataifa unaohudumia zaidi ya wasafiri milioni 20 kila mwaka, jambo linaloufanya uwe miongoni mwa vituo vya usafiri vyenye shughuli nyingi zaidi barani Ulaya. Uwanja wa Ndege wa Dublin uko umbali wa takribani kilomita 10 (maili 6) kaskazini kutoka katikati mwa mji wa Dublin, karibu na barabara za M1 na M50 na unafikiwa kwa urahisi kwa gari, basi, teksi au Uber.

Vituo katika Uwanja wa Ndege wa Dublin

Uwanja wa Ndege wa Dublin unahudumiwa na vituo 2 vikuu: Kituo cha 1 na Kituo cha 2. Kituo cha 2 kinaonekana kwa urahisi, kwa maana kina vifaa vya ukaguzi wa Marekani, ambavyo vinakuwezesha kupitia ukaguzi wa forodha na wa pasipoti ukiwa Dublin. Kwa hivyo, ukiwasili Marekani itakuwa kana kwamba umesafiri nchini mwako, hivyo utaokoa muda na kusubiri kwa muda mrefu katika kukaguliwa.

Kituo cha 1

 • Air Canada
 • Cathay Pacific
 • KLM
 • Ryanair
 • Swiss

Kituo cha 2

 • Aer Lingus
 • American
 • Delta
 • Emirates

Migahawa ya Uwanja wa Ndege wa Dublin

Iwe unataka kupata eneo la kupumzika kabla ya kusafiri au eneo la kupata kahawa kila siku, kuna migahawa mingi unayoweza kuchagua kwenye Uwanja wa Ndege wa Dublin. Katika Kituo cha 1, unaweza kuchukua chakula cha Ayalandi katika Wrights of Howth, ilhali Gourmet Burger Kitchen katika Kituo cha 2 ni bora kwa mlo kabla ya kusafiri. Kuna pia aina mbalimbali za baa katika Uwanja wa Ndege wa Dublin.

Kusafiri kwenye Uwanja wa Ndege wa DUB

Ni rahisi kutembea katika Uwanja wa Ndege wa Dublin. Kuna basi linalosafiri kati ya Kituo cha 1 na Kituo cha 2.

Mambo ya kufanya kwenye Uwanja wa Ndege wa Dublin

Kutokana na zaidi ya aina 100 za bidhaa zinazopatikana kwenye maduka ya Uwanja wa Ndege wa Dublin, mteja ana fursa ya kuchagua bidhaa inayompendeza. Eneo la Biashara kwenye Vituo vya 1 na 2 lina aina nyingi za maduka yanayojulikana kote ulimwenguni ikiwa ni pamoja na Jo Malone, Chanel, Dior na MAC. Na kwa sababu hutozwi ushuru kwenye uwanja huu, wanunuzi wanapata mapunguzo makubwa ya bei> Bei bidhaa nyingine hupungua kwa hadi 40% ikilinganishwa na maduka yaliyo nje ya uwanja huu wa ndege.

Mabafu kwenye Uwanja wa Ndege wa Dublin

Ingawa mabafu hayapatikani kwa wasafiri wengi, mojawapo ya sebule za uwanja wa ndege ina mabafu, yanayokuwezesha kuoga kabla na baada ya safari.

Hoteli karibu na Uwanja wa Ndege wa Dublin

Wageni wanaweza kupata hoteli kadhaa kwa urahisi kwenye uwanja wa ndege. Hii inawafaa zaidi wasafiri wanaowasili Ireland alfajiri. Kwa wale wanaoweza kukaa zaidi kwenye uwanja huu wa Dublin, kuna vyumba vya mapumziko vya bei nafuu na vya kifahari.

Sehemu za kuvutia karibu na Uwanja wa Ndege wa Dublin

Ukiwa katika eneo la kushukishwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Dublin, kuna vitu vingi vya kuona na kufanya. Ni vyema kukumbuka kuwa unapaswa kuanza mchakato wa kuabiri ndege mapema (dakika 40 hadi saa moja). Katika mji wa Dublin, kuna maeneo mengi ya kihistoria na kitamaduni ambayo unaweza kuzuru, yakiwemo:

 • Dublin Castle
 • Guinness Storehouse
 • Irish Whiskey Museum
 • Kilmainham Gaol
 • Richmond Barracks

Pata maelezo zaidi kuhusu Uwanja wa Ndege wa Dublin hapa.

Facebook
Instagram
Twitter

Ukurasa huu una taarifa kutoka kwenye tovuti za washirika wengine ambazo hazisimamiwi na Uber na zinaweza kugeuzwa au kubadilishwa mara kwa mara. Maelezo yoyote yaliyojumuishwa kwenye ukurasa huu ambayo hayahusiani moja kwa moja na Uber au kazi zake yanatumika kuarifu tu na hayafai kutegemewa, au kuchukuliwa au kufasiliwa kwa namna inayoweka dhamana ya aina yoyote, iwe ya moja kwa moja au inayokisiwa, kuhusu maelezo yaliyo hapa. Baadhi ya masharti na vipengele hutofautiana kutegemea nchi, eneo na jiji. Ofa ya punguzo inawalenga watumiaji wapya pekee. Huwezi kutumia ofa hii pamoja na ofa nyinginezo na haiwezi kutumiwa katika bakshishi. Inapatikana kwa muda mfupi. Vigezo na masharti ya ofa vinaweza kubadilika.