Ruka uende katika maudhui ya msingi

Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Indira Gandhi (DEL)

Tumia Uber kwenda popote, iwe unasafiri kutoka Uwanja wa Ndege wa Delhi kwenda Qutub Minar au kutoka India Gate kurudi kwenye Uwanja wa Ndege.

H34X+FX Delhi, India
+91 124-337-6000

Njia bora zaidi ya kusafiri

Itisha usafiri kote ulimwenguni

Bonyeza tu kitufe ili upate usafiri wa angani katika zaidi ya viwanja vikuu 500.

Safiri kama mwenyeji

Acha App na dereva wako ashughulikie masuala ya kina ili usisumbuke kutafuta maelekezo katika jiji ambapo wewe ni mgeni.

Safiri bila wasiwasi kwa kutumia Uber

Pata vipengele unavyovipenda, ikiwa ni pamoja na bei zinazooneshwa moja kwa moja na uwezo wa kulipa bila pesa taslimu, hata ukiwa ugenini.

Aina za usafiri ukiwa eneo husika

 • Sedan Intercity

  1-4

  Outstation rides in comfortable sedans

 • XL Intercity

  1-6

  Affordable outstation rides for groups up to 6

1/2

Kupata gari kwenye Uwanja wa Ndege wa DEL

Fahamu unakoweza kuchukuliwa

Katika Uwanja wa Ndege wa Delhi, eneo lako la kuchukuliwa linategemea kituo ulichochagua. Ikiwa umechagua Kituo cha 1 au 3, tembea hadi eneo la kuchukuliwa lilitotengewa Uber. Kwa Kituo cha 2, dereva wako atakupata katika eneo ulilochagua kuchukuliwa.

Angalia App ili upate maelezo

Pindi unapoitisha gari, fuata maelekezo kwenye programu ili ufike eneo lako la kuchukuliwa.

Kituo cha 1: Tembea kuelekea eneo la Uber la kuchukua wasafiri katika maegesho.

Kituo cha 2: Fuata maelekezo kwenye programu ili ufikie eneo ulilochagua kuchukuliwa.

Kituo cha 3: Tembea hadi kwenye Eneo la Kuchukua wasafiri wa Uber katika ghorofa ya chini ya maegesho ya T3, mkabala wa malango ya Wanaowasili ya 1 na 2.

Kutana na dereva wako

Dereva wako atakukuta katika eneo la kuchukulia wasafiri lililooneshwa kwenye programu. Ikiwa humpati dereva wako, wasiliana naye kupitia programu.

Ramani ya Uwanja wa Ndege wa Delhi

Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Indira Gandhi unahudumia mashirika 80 ya ndege katika vituo 2: Kituo cha 1 na Kituo cha 3. Kituo cha 1 kina vituo vidogo 4. Kituo cha 1A, Kituo cha 1B, Kituo cha 1C na Kituo cha 1D. Mashirika yote ya ndege yanayofanya safari za kimataifa yanatumia Kituo cha 3.

Maswali ambayo wasafiri wanauliza sana

 • Ndiyo. Bonyeza hapa ili uone orodha ya viwanja vya ndege kote duniani unakoweza kuitisha usafiri wa Uber.

 • Nauli ya usafiri wa Uber kuenda (au kutoka) Uwanja wa Ndege wa DEL inategemea hali kama vile aina ya usafiri, kadirio ya umbali na muda wa safari, ada ya vibali barabarani na idadi ya maombi ya usafiri.

  Unaweza kuona kadirio la bei kabla ya kuitisha usafiri kwa kuweka eneo la kuchukuliwa na mahali unakoenda katika zana ya kukadiria nauli katika Uber hapo juu. Kisha, unapoitisha usafiri utaona nauli yako halisi kwenye app kwa kutegemea hali za wakati huo.

 • Maeneo ya kuchukuliwa yanategemea aina ya usafiri unaoitisha na ukubwa wa uwanja wa ndege. Fuata maagizo kwenye App kuhusu eneo utakakomkuta dereva wako. Unaweza pia kuangalia mabango yanayoashiria maeneo ya usafiri wa pamoja yaliyobainishwa kwenye uwanja wa ndege.

  Ikiwa humpati dereva wako, wasiliana naye kupitia programu.

Maelezo zaidi

Je, unaelekea uwanja tofauti wa ndege?

Unaweza kupelekwa na kuchukuliwa kutoka zaidi ya viwanja 600 vya ndege kote duniani.

Maelezo kwa wageni kwenye Uwanja wa Ndege wa Delhi

Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Indira Gandhi unashikilia nafasi ya 10 kati ya viwanja vyenye abiria wengi zaidi duniani, huku ukiwahudumia zaidi ya wasafiri milioni 65 kila mwaka. Uwanja upo kilomita 16 (maili 10) kutoka katikati ya jiji la New Delhi, ni mwendo wa dakika 16 kwa gari wakati hakuna foleni au vikwazo vingine barabarani.

Vituo katika Uwanja wa Ndege wa Delhi

Uwanja wa Ndege wa DEL una vituo 3 vikuu vya wasafiri: Kituo cha 1, Kituo cha 2 na Kituo cha 3. Kumbi za Uwanja wa Ndege wa DEL zipo katika maeneo mbalimbali uwanjani. Unaweza kupanga safari yako ukitumia taarifa zilizo hapa chini.

Kituo cha 1 katika DEL

 • IndiGo
 • SpiceJet

Kituo cha 2 katika DEL

 • GoAir
 • IndiGo
 • SpiceJet

Kituo cha 3 (Kimataifa) katika DEL

Uwanja wa Ndege wa New Delhi una safari za kimataifa katika Kituo cha 3. DEL una safari za moja kwa moja za kimataifa kuelekea maeneo 70 zinazofanywa na mashirika ya ndege ya American, British Airways na Emirates. Kumbi za Uwanja wa Ndege wa Indira Gandhi zipo kwenye maeneo 5 ya Kituo cha 3.

Kupata chakula katika Uwanja wa Ndege wa Delhi

Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Indira Gandhi una sehemu nyingi za kupata mlo katika vituo vyote. Kuna zaidi ya maeneo 80, ambapo wasafiri wanaweza kupata vinywaji na vyakula, yakiwemo maduka ya kahawa, migahawa ya kuuza vyakula vya kufungashiwa na maduka yanayouza vitafunio. Wasafiri ambao wanapendelea huduma za kulia mezani wanaweza kuchagua migahawa iliyo katika uwanja wa ndege wa DEL.

Kusafiri kwenye Uwanja wa Ndege wa Delhi

Kuna mabasi ya usafiri bila malipo katika Uwanja wa Ndege wa New Delhi yanayounganisha Kituo cha 1 na Kituo cha 3 kila baada ya dakika 20. Abiria wanaoelekea katika mashirika tofauti ya ndege kutoka kituo kimoja hadi kingine wanafaa kuenda katika kaunta ya kuhamishiwa katika kituo tofauti (ipo karibu na Nguzo ya 10 katika Kituo cha 3 na chini ya barabara ya juu kwa juu katika Kituo cha 1). Kituo cha 2 na Kituo 3 vinakaribiana, kwa hivyo inachukua dakika 5 kutembea kutoka kituo kimoja kwenda kingine.

Mambo ya kufanya katika Uwanja wa Ndege wa Delhi

Kuna vitu vingi vya kuvutia katika Uwanja wa Ndege wa DEL ambavyo wasafiri wanaweza kufanya, zikiwemo spaa katika sehemu za kuondoka katika Kituo cha 3 na Kituo cha 1. Isitoshe kuna maduka mengi katika Uwanja wa Ndege wa New Delhi yanayouza vifaa vya kielektroniki, zawadi, pipi na mapambo. Katika eneo la kuondoka kwa ajili ya safari za kimataifa kwenye Kituo cha 3, kuna mfumo wa kuiga namna ya kurusha ndege unaowapa wasafiri fursa ya kuendesha Boeing 737.

Kubadilisha sarafu katika Uwanja wa Ndege wa Delhi

Ofisi za kubadilisha fedha katika Uwanja wa Ndege wa New Delhi zipo katika eneo la Wanaowasili na Kuondoka katika Kituo cha 3, Kituo cha 3 kwa ajili ya safari za wasafiri wa nchini wanaoingia na kuondoka, na Kituo cha 1 kwa ajili ya wanaondoka .

Hoteli zilizo karibu na Uwanja wa Ndege wa Delhi

Iwe unasubiri ndege nyingine au ndege imechelewa usiku kucha, au kama unahitaji mahali pa kukaa karibu na DEL, kuna zaidi ya hoteli 40 na maeneo ya kulala karibu.

Sehemu za kuvutia karibu na Uwanja wa Ndege wa Delhi

 • Kaburi la Humayun
 • Khari Baoli
 • Red Fort
 • Sunder Nursery

Pata maelezo zaidi kuhusu DEL hapa.

Facebook
Instagram
Twitter

Ukurasa huu una taarifa kutoka kwenye tovuti za washirika wengine ambazo hazisimamiwi na Uber na zinaweza kugeuzwa au kubadilishwa mara kwa mara. Maelezo yoyote yaliyojumuishwa kwenye ukurasa huu ambayo hayahusiani moja kwa moja na Uber au kazi zake yanatumika kuarifu tu na hayafai kutegemewa, au kuchukuliwa au kufasiliwa kwa namna inayoweka dhamana ya aina yoyote, iwe ya moja kwa moja au inayokisiwa, kuhusu maelezo yaliyo hapa. Baadhi ya masharti na vipengele hutofautiana kutegemea nchi, eneo na jiji. Ofa ya punguzo inawalenga watumiaji wapya pekee. Huwezi kutumia ofa hii pamoja na ofa nyinginezo na haiwezi kutumiwa katika bakshishi. Inapatikana kwa muda mfupi. Vigezo na masharti ya ofa vinaweza kubadilika.