Please enable Javascript
Ruka uende katika maudhui ya msingi

Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (DAR)

Safiri kwenda na kutoka Uwanja wa Ndege wa Dar es Salaam ukitumia Uber. Badala ya kusubiri basi la DAR au teksi, unaweza kuomba safari moja kwa moja kwenye programu na utakuwa safarini.

Dar es Salaam,
+255 22-284-4371

search
Where from?
Navigate right up
search
Where to?

Request a ride around the world

Bofya kitufe sasa na upate usafiri wa uwanja wa ndege katika zaidi ya vituo vikuu 700.

Safiri kama mkazi

Acha programu na dereva wako washughulikie maelezo ya kina ili usisumbuke kutafuta maelekezo katika mji usiofahamu.

Safiri bila wasiwasi ukitumia Uber

Pata vipengele unavyovipenda, ikiwemo bei za wakati halisi na malipo ya kielektroniki, hata ukiwa ugenini.

Ways to ride in the area

Pickup at Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (DAR)

Fungua programu yako ili uombe safari

Chagua gari linalotoshea idadi ya wasafiri na mizigo mliyo nayo.

Fuata maelekezo kwenye programu

Utapata maelekezo kuhusu maeneo ya kuchukua wasafiri moja kwa moja katika programu. Pia kunaweza kuwa na mabango katika uwanja wa ndege.

Kutana na dereva wako

Nenda katika eneo la kuchukuliwa jinsi ilivyobainishwa katika App. Tafadhali kumbuka, eneo hilo huenda halitakuwa karibu kabisa na lango unaloondokea. Ikiwa humpati dereva wako, wasiliana naye kupitia App.

Top questions from riders

  • Iwe umewasili au unajiandaa kuondoka Dar es Salaam, Uber iko tayari kukufikisha unapotaka kwenda.

  • Nauli hutegemea wakati, upatikanaji na masuala mengine. Angalia mfumo wa Uber wa kukadiria nauli ili ufahamu itakugharimu hela ngapi kusafiri.

  • Maeneo ya kuchukuliwa yanaweza kubadilika, kwa hivyo hakikisha kwamba umeangalia programu ya Uber mara kwa mara baada ya kuitisha usafiri.

  • Hubadilika kutegemea wakati, foleni na idadi ya madereva walio kazini.

More information

  • Unaendesha gari ukitumia Uber?

    Kuanzia eneo la kuwachukua wasafiri hadi kufuata sheria na kanuni za mahali husika, fahamu jinsi ya kufanya safari zako za uwanja wa ndege ziwe bora zaidi.

  • Unaelekea uwanja tofauti wa ndege?

    Unaweza kushushwa na kuchukuliwa kutoka zaidi ya viwanja 700 vya ndege kote ulimwenguni.

1/2

Taarifa kwa wageni jijini Dar es Salaam

Uber ndio usafiri bora zaidi unaposafiri kati ya Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere hadi katikati mwa jiji la Dar es Salaam. Uwanja huu wa kimataifa upo takriban kilomita 13 (maili 8) kutoka katikati mwa jiji la Dar es Salaam; na jina lake linatokana na Rais wa kwanza wa Tanzania, Mwalimu Julius Nyerere. Uwanja wa Ndege wa DAR huhudumia takriban wasafiri milioni 3.5 kila mwaka sambamba na safari hizi kuelekea nchi nyingine za Afrika, Ulaya na Mashariki ya Kati. Uber itakusaidia kurahisisha safari yako kwa kukusafirisha kutoka kwenye uwanja wa ndege hadi unakoenda na kukurudisha kwenye uwanja uda wa safari yako ya ndege ukifika.

Vituo vya Uwanja wa Ndege wa Dar es Salaam

Kuna vituo 2 vinavyohudumia wasafiri wa ndani ya nchii na wa kimataifa. Ujenzi wa kituo cha 3 utakamilika mwaka wa 2019. Kituo cha 1 kinahudumia wasafiri wa ndani ya na ndege ndogo. Kituo cha 2 kwenye Uwanja wa Ndege wa DAR kinahudumia wasafiri wa kimataifa na ndege kubwa za safari za ndani ya nchi.

Kusafiri katika Uwanja wa Ndege wa Dar es Salaam

Hakuna huduma za mabasi kati ya vituo. Kwa safari za kwenda katikati ya mji, unaweza kuabiri basi wakati wowote kutoka kwenye vituo vilivyo takribani mita 500 (theluthi moja ya maili) kutoka Kituo cha 1 na umbali wa mita 100 kutoka Kituo cha 2. Hoteli nyingi pia hutoa huduma za usafiri kutoka na kwenda kwenye uwanja wa ndege ni nzuri kwa safari za kuunganisha haraka.

Migahawa katika Uwanja wa Ndege wa Dar es Salaam

Uwanja wa Ndege wa Dar es Salaam una vyakula vingi. Uwanja huu wa ndege una migahawa mbalimbali na aina nyingi za vyakula.

Maduka katika Uwanja wa Ndege wa Dar es Salaam

Uwanja wa Ndege wa DAR una maduka ya bidhaa zisizotozwa kodi ambako unaweza kupata bidhaa ikiwa ni pamoja na vitafunwa na sabuni kwa bei nafuu. Kuna uwezekano wa kupata unachohitaji, iwe unachukua hedaya au kitu cha kukumbuka safari

.

Hoteli katika Uwanja wa Ndege wa Dar es Salaam

Ikiwa unasafiri alfajiri au unahitaji mahali panapokufaa kutulia kabla au baada ya safari, hoteli karibu na Uwanja wa Ndege wa Dar es Salaam zina vyumba vya kulala. Kuna hoteli za mbali na za karibu na uwanja wa ndege kwa bei mbalimbali. Hutakosa inayokufaa. Angalia hoteli yako ili uone ikiwa ina huduma ya kupelekwa kwenye uwanja wa ndege, au uitishe usafiri wa Uber ili upelekwe kwa urahisi kwenye uwanja wa ndege.

Sehemu za kuvutia karibu na Uwanja wa Ndege wa DAR

Unaweza kufanya mambo mbalimbali mjini Dar es Salaam, yakiwemo kutembelea:

  • Askari Monument
  • Bongoyo Island
  • Coco Beach
  • Dar es Salaam Zoo
  • Kariakoo Market
  • The National Museum of Tanzania
  • Oyster Bay

Pata maelezo zaidi kuhusu Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere hapa.

This page contains information from third-party websites that are not under the control of Uber and that may be periodically changed or updated. Any information included on this page that is not directly related to Uber or its operations is for informational purposes only and in no way shall be relied upon, or interpreted or construed to create any warranties of any kind, either express or implied, regarding the information contained herein. Certain requirements and features vary by country, region, and city.