Ruka uende katika maudhui ya msingi
Uber
Uber

Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Cape Town (CPT)

Iwe unasafiri kuelekea katikati ya jiji kutoka Uwanja wa Ndege wa Cape Town au kutoka katikati ya jiji kuelekea Uwanja wa Ndege wa Cape Town, iamini Uber kukufikisha unakoenda.

Matroosfontein, Cape Town, 7490, South Africa
+27 21-937-1200

Itisha usafiri kote ulimwenguni

Bonyeza tu kitufe ili upate usafiri wa angani katika zaidi ya viwanja vikuu 500.

Safiri kama mwenyeji

Acha programu na dereva wako ashughulikie masuala ya kina ili usisumbuke kutafuta maelekezo katika jiji ambapo wewe ni mgeni.

Safiri bila wasiwasi kwa kutumia Uber

Pata vipengele unavyovipenda, ikiwa ni pamoja na bei zinazooneshwa moja kwa moja na uwezo wa kulipa bila pesa taslimu, hata ukiwa ugenini.

Sampuli za bei za msafiri ni makadirio tu na hazioneshi mabadiliko yanayotokana na mapunguzo, kucheleweshwa kwenye foleni na mambo mengine. Tunaweza kutumia nauli isiyobadilika na bei za chini zaidi. Bei halisi zinaweza kubadilika.

 • UberX1-4

  Affordable, everyday rides

 • UberXL1-6

  Affordable rides for groups up to 6

 • Black1-4

  Premium rides in luxury cars

Fungua programu yako ili kuitisha usafiri

Ukishakuwa tayari, fungua programu yako na uitishe usafiri. Chagua usafiri unaotoshea idadi ya wasafiri na mizigo mliyo nayo.

Fuata maelekezo katika programu

Utapata maelekezo kuhusu eneo la kuchukua wasafiri moja kwa moja katika programu. Pia kunaweza kuwa na alama katika uwanja wa ndege.

Kutana na dereva wako

Nenda katika eneo la kuchukuliwa jinsi ilivyobainishwa katika programu. Tafadhali kumbuka, eneo hilo huenda halitakuwa karibu kabisa na lango unaloondokea. Ikiwa humpati dereva wako, wasiliana naye kupitia programu.

WiFi katika Uwanja wa Ndege wa Cape Town

Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Cape Town hutoa huduma za WiFi bila malipo kwa wasafiri walio katika maeneo ya kuabiri. Utapokea data kwa saa 4 au GB 1 bila malipo, unaweza kuongeza muda au kiasi hicho kwa kulipia kiasi unachotumia.

Maegesho katika Uwanja wa Ndege wa Cape Town

Uwanja wa Ndege wa Cape Town una aina nyingi za maegesho, yakiwemo maegesho ya muda mfupi, maegesho ya muda mrefu, maegesho ya kuchukua na kushukisha wasafiri kwa haraka pamoja na huduma ya kumwachia mhudumu gari ili aliegeshe.

Kuweka mizigo katika Uwanja wa Ndege wa Cape Town

Unaweza kuhifadhi mkoba wako katika sehemu za CPT za kuweka mizigo bila kujali ukubwa wake, sehemu hizo zipo katika Sehemu ya Kuwasili kwa Wasafiri wa Nchini na utatakiwa kulipa ada ndogo.

Uber inapatikana katika Uwanja wa Ndege wa Cape Town, kwa hivyo unaweza kufurahia usafiri wa starehe na uhakika popote unapotaka kwenda.

Ili kupata eneo la kuchukuliwa, angalia programu ya Uber baada ya kuitisha usafiri.

Hata kama safari si ndefu sana, ada za Uber ukitoka na kuenda kwenye Uwanja wa Ndege wa Cape Town zinaweza kuathiriwa na muda, foleni na masuala mengine. Angalia mfumo wa kukadiria nauli wa Uber ili ufahamu makadirio ya nauli ya safari.

Muda wa kuchukuliwa unaweza kutofautiana kulingana na wakati, idadi ya madereva wanaopatikana na masuala mengine.

Unatumia mfumo wa Uber kuendesha gari?

Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kurahisisha huduma unayopokea katika viwanja vya ndege, zikiwemo sheria na kanuni za nchi husika.

Je, unaelekea uwanja tofauti wa ndege?

Unaweza kupelekwa na kuchukuliwa kutoka zaidi ya viwanja 500 vya ndege kote duniani.

Uber ni chaguo bora kwa wasafiri wanaowasili au kuondoka kwenye Uwanja wa Ndege wa CPT. Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Cape Town ndio wa 3 kwa ukubwa barani Afrika. Unawahudumia takribani wasafiri milioni 10 kila mwaka. Uwanja wa Ndege wa CPT unapatikana umbali wa kilomita 20 (maili 12) kutoka katikati mwa Mji wa Cape Town, jambo linaloufanya kuwa chaguo bora kwa watu wanaowasili na kuondoka Cape Town. Uwanja wa ndege wa CPT ni chaguo bora kwa yeyote anayetembelea Cape Town kwa sababu ndio uwanja wa kipekee unaotoa huduma kwa wasafiri katika eneo hili. Isitoshe, kuna mabasi, magari, teksi na Uber zinazopatikana wakati wowote kusafirisha wasafiri wanaowasili na kuondoka kwenye uwanja wa ndege.

Vituo katika Uwanja wa Ndege wa Cape Town

Uwanja wa Ndege wa Cape Town una kituo kimoja kikuu kilichogawanywa kati ya usafiri wa nchini na wa kimataifa na vina sehemu moja ya kukagua usalama. Kituo cha kimataifa kinapatikana kaskazini mwa jengo na kile cha wasafiri wa nchini kinapatikana kusini. Kituo cha Uwanja wa Kimataifa wa Cape Town kina ghorofa 3: ghorofa ya chini (wanaowasili), ghorofa ya 2 (wanaoondoka) na ghorofa ya 3 ina sehemu ya kuuza vyakula. Mashirika mbalimbali yanahudumu kwenye CPT, yakiwemo:

 • Airlink
 • Austrian
 • CemAir
 • Emirates
 • Ethiopian
 • FlySafair
 • Joon
 • kulula.com
 • Lufthansa
 • Qatar
 • Thomas Cook

Migahawa kwenye Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Cape Town

Kuna aina mbalimbali ya migahawa ya kugundua kwenye Uwanja wa Ndege wa Cape Town. Kuanzia baa na vibanda vya vyakula tayari hadi migahawa na maduka ya vinywaji. Bidhaa kwenye migahawa ya Cape Town zinatosheleza mahitaji yako.

Kusafiri kwenye Uwanja wa Ndege wa CPT

Kwa sababu Uwanja wa Ndege wa Cape Town una jengo moja la kituo kikuu, ni rahisi kutembea mwenyewe.

Mambo ya kufanya kwenye Uwanja wa Ndege wa Cape Town

Iwe unatafuta bidhaa bora za kimataifa au za nchini, unaweza kuzinunua katika maduka kwenye Uwanja wa Ndege wa Cape Town. Uwanja wa Ndege wa CPT, unakupa chaguo za kukufaa, kuanzia vitabu na mizigo hadi mivinyo maarufu ya Afrika Kusini. Isitoshe, maduka ya bidhaa zisizotozwa kodi kwenye Uwanja wa Ndege wa Cape Town yanawafaa watu wanaotaka kuwazawadi wapendwa hedaya za ukumbusho.

Sebule kwenye Uwanja wa Ndege wa Cape Town

Kuna sebule nyingi za kuchagua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Cape Town. Hii inakuwezesha kufanya kazi au kupumzika kabla ya safari. Bidvest Premier Lounges, zinapatikana kwenye vituo vya wasafiri wa nchini na wa kimataifa, zina sehemu nzuri za kukalia, WiFi na vyakula bora. SAA Voyager Platinum Lounge, Baobab Premium Class Lounge, na SLOW Lounge zina maeneo mazuri ya kutulia baada ya shughuli kwenye uwanja wa ndege.

Hoteli karibu na Uwanja wa Ndege wa Cape Town

Kuna hoteli 2 kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Cape Town. Zinawafaa zaidi wasafiri wa alfajiri. Mbali na uwanja huu, kuna hoteli nyingi tofauti katika eneo pana la Cape Town. Utapata vyumba vya bei nafuu, vyumba vya kukodisha au hoteli za kifahari.

Maeneo ya kuzuru karibu na Uwanja wa Ndege wa CPT

Ikiwa unasubiri ndege nyingine katika Uwanja wa Ndege wa Cape Town, unaweza kuzuru maeneo mbalimbali. Kusafiri kuona baadhi ya maeneo asili ya kuvutia, yakiwemo:

 • Boulders Penguin Colony
 • Kisiwa cha Robben
 • Table Mountain
 • Cape of Good Hope

Pata maelezo zaidi kuhusu Uwanja wa Ndege wa Cape Town hapa.

Facebook
Twitter