Please enable Javascript
Ruka uende katika maudhui ya msingi

Uwanja wa Ndege wa Paris-Charles de Gaulle (CDG)

Je, unatafuta mbinu mbadala ya usafiri ambayo si basi la kawaida la Uwanja wa Ndege wa Charles de Gaulle au teksi? Iwe unasafiri kutoka CDG hadi Paris au kutoka Paris hadi CDG, fika unakoenda ukitumia programu ya Uber unayoijua tayari. Omba gari la kukupeleka na kukurudisha kutoka CDG kwa kubofya kitufe.

Roissy-en-France, 95700
+33 1-70-36-39-50

search
Where from?
Navigate right up
search
Where to?

Request a ride around the world

Bofya kitufe sasa na upate usafiri wa uwanja wa ndege katika zaidi ya vituo vikuu 700.

Safiri kama mkazi

Acha programu na dereva wako washughulikie maelezo ya kina ili usisumbuke kutafuta maelekezo katika mji usiofahamu.

Safiri bila wasiwasi ukitumia Uber

Pata vipengele unavyovipenda, ikiwemo bei za wakati halisi na malipo ya kielektroniki, hata ukiwa ugenini.

Ways to ride in the area

Pickup at Uwanja wa Ndege wa Paris-Charles de Gaulle (CDG)

Fungua programu yako ili uombe safari

Ukiwa tayari, fungua programu ya Uber ili uombe safari ya kuelekea mahali unakoenda. Chagua chaguo la usafiri wa uwanja wa ndege wa CDG linalokidhi mahitaji ya idadi ya wasafiri na mizigo yenu.

Fuata maelekezo kwenye programu

Utapata maelekezo kuhusu maeneo ya kuchukua wasafiri ya Uwanja wa Ndege wa Charles de Gaulle moja kwa moja kwenye programu. Maeneo ya kuchukua wasafiri yanaweza kutofautiana kulingana na kituo. Ishara za maeneo ya kuchukua wasafiri wanaosafiri pamoja zinaweza pia kupatikana katika Uwanja wa Ndege wa Paris-Charles de Gaulle.

Kutana na dereva wako

Nenda kwenye eneo lako la kuchukuliwa la CDG kama ilivyobainishwa kwenye programu. Tafadhali kumbuka: eneo hili huenda lisiwe kwenye lango la kutoka lililo karibu zaidi nawe. Jina la dereva wako, nambari ya leseni na rangi ya gari itaonyeshwa kwenye programu. Thibitisha gari lako kabla ya kuingia. Ikiwa humpati dereva wako, wasiliana naye kupitia programu.

Top questions from riders

  • Uber inapatikana katika Uwanja wa Ndege wa Charles de Gaulle, kwa hivyo unaweza kufurahia usafiri wa starehe na uhakika popote unapotaka kwenda.

  • Ili kupata eneo la kuchukuliwa, angalia programu ya Uber baada ya kuitisha usafiri.

  • Hata kama safari si ndefu sana, ada za Uber kutoka na kwenda Uwanja wa Ndege wa Charles de Gaulle zinaweza kuathiriwa na muda, foleni na masuala mengine. Angalia mfumo wa kukadiria nauli wa Uber ili ufahamu makadirio ya nauli ya safari.

  • Muda wa kuchukuliwa unaweza kutofautiana kulingana na wakati, idadi ya madereva wanaopatikana na masuala mengine.

More information

  • Unaendesha gari ukitumia Uber?

    Kuanzia eneo la kuwachukua wasafiri hadi kufuata sheria na kanuni za mahali husika, fahamu jinsi ya kufanya safari zako za uwanja wa ndege ziwe bora zaidi.

  • Unaelekea uwanja tofauti wa ndege?

    Unaweza kushushwa na kuchukuliwa kutoka zaidi ya viwanja 700 vya ndege kote ulimwenguni.

1/2

Mambo unayofaa kufanya ukiwa katika vituo vya uwanja wa ndege wa Charles de Gaulle

Uber ni chaguo bora kwa wasafiri wanaowasili au kuondoka Uwanja wa Ndege wa CDG. Uwanja wa Ndege wa Charles de Gaulle—unaojulikana pia kama Uwanja wa Ndege wa Roissy—ndio uwanja mkubwa zaidi wa kimataifa nchini Ufaransa. Iwe unaelekea Disneyland au Paris, ni chaguo linalowafaa wasafiri wa nchini na wa kimataifa. Uwanja wa Ndege wa Charles de Gaulle unapatikana takribani kilomita 25 (maili 15) kaskazini mwa Paris, hivyo kuufanya chaguo bora zaidi kwa wageni wanaozuru mji huu mkuu na maarufu wa Ufaransa. Kuna watalii wanaotembelea eneo pana la Paris.

Vituo kwenye Uwanja wa Ndege wa Charles de Gaulle

Uwanja wa Ndege wa Charles de Gaulle una vituo 3 vya wasafiri: T1, T2 na T3.

Kituo cha 1 kwenye CDG

Mashirika yafuatayo,miongoni mwa mengine yanatoa huduma katika Kituo cha 1:

  • Aegean
  • Malaysia
  • Qatar

Kituo cha 2 kwenye CDG

Kituo cha 2 kimegawanywa katika zaidi ya vituo 7 vidogo, 2A hadi 2G na kina kituo cha reli cha TGV-RER kinachojulikana kama Aéroport Charles de Gaulle 2. Mashirika yafuatayo yanahudumia Kituo cha 2:

  • Air France
  • British Airways
  • Cathay Pacific

Kituo cha 3 kwenye CDG

Shirika hili miongoni mwa mengine yanahudumia Kituo cha 3:

  • Jordan Aviation

Vyakula katika Uwanja wa Ndege wa Paris-Charles de Gaulle

Utapata aina nyingi za vyakula na vinywaji katika Uwanja wa Ndege wa CDG. Vyakula hivi ni vya Kifaransa na vya kimataifa. Migahawa kwenye Uwanja wa Ndege wa Charles de Gaul hutoa huduma yoyote ya mapishi unayotaka.

Kusafiri kwenye Charles de Gaulle (CDG)

CDGVAL inaweza kukusafirisha kati ya vituo mbalimbali vya Charles de Gaulle kutoka maegesho yake 2. Pia kuna kituo cha mabasi na magari ya uwanja wa ndege. Unaweza pia kusafiri moja kwa moja hadi Paris kwa kutumia barabara ya RER B kupitia Vituo vya 2 na 3.

Mambo unayoweza kufanya katika Uwanja wa Ndege wa Charles de Gaulle

Maduka kwenye Uwanja wa Ndege wa CDG yana kila unachohitaji, iwe unatafuta mvinyo, vileo, vipodozi au zawadi za ukumbusho kutoka Paris. Elekea Chanel au Swarovski ili kupata vito na saa, au uchague baadhi ya mavazi ya kisasa zaidi kutoka Prada, Dior, Gucci na kwenye maduka mengine mengi ya mavazi yanayotambulika kote ulimwenguni. Uwanja wa Ndege wa Charles de Gaulle pia una sehemu ya watoto kucheza, pamoja na vyumba vya maombi na sebule.

Hoteli kwenye Uwanja wa Ndege wa Charles de Gaulle

Kuna hoteli 2 zinazopatikana ndani ya Kituo cha 2. Hii inawafaa watu wanaowasili jioni au alfajiri. Kando na haya, kuna hoteli mbalimbali za kifahari katika eneo la Roissy, ambapo uwanja wa Ndege wa Charles de Gaulle unapatikana. Mji wa Paris una vyumba mbalimbalii vya kulala vilivyoundwa kufaa kila msafiri kulingana na uwezo wake wa kifedha.

Maeneo ya kuzuru karibu na Uwanja wa Ndege wa Paris-Charles de Gaulle

Ukiwa kwenye kituo katika Uwanja wa Ndege wa Charles de Gaulle na una muda wa kutosha kufika katikati mwa mji wa Paris—utahitaji muda wa angalau saa 6—kuna maeneo mengi ya kihistoria unayoweza kuzuru. Magari mengi yanayounganisha CDG na katikati mwa Paris.

  • Arc de Triomphe
  • Champs-Élysées
  • Eiffel Tower
  • Makavazi ya Louvre
  • Notre-Dame de Paris
  • Kasri ya Versailles

Pata maelezo zaidi kuhusu Uwanja wa Ndege wa Paris-Charles de Gaulle hapa.

This page contains information from third-party websites that are not under the control of Uber and that may be periodically changed or updated. Any information included on this page that is not directly related to Uber or its operations is for informational purposes only and in no way shall be relied upon, or interpreted or construed to create any warranties of any kind, either express or implied, regarding the information contained herein. Certain requirements and features vary by country, region, and city.