Ruka uende katika maudhui ya msingi

Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Nashville (BNA)

Tumia Uber kwenda popote, iwe unasafiri kutoka Uwanja wa Ndege wa BNA kwenda Broadway au kutoka katikati ya mji ya Nashville hadi BNA

1 Terminal Drive, Nashville, TN 37214
+1 615-275-1675

Njia bora zaidi ya kusafiri

Itisha usafiri kote ulimwenguni

Bonyeza tu kitufe ili upate usafiri wa angani katika zaidi ya viwanja vikuu 500.

Safiri kama mwenyeji

Acha App na dereva wako ashughulikie masuala ya kina ili usisumbuke kutafuta maelekezo katika jiji ambapo wewe ni mgeni.

Safiri bila wasiwasi kwa kutumia Uber

Pata vipengele unavyovipenda, ikiwa ni pamoja na bei zinazooneshwa moja kwa moja na uwezo wa kulipa bila pesa taslimu, hata ukiwa ugenini.

Punguzo la hadi $15

Pata punguzo la $5 kwenye safari zako tatu za kwanza. Tumia kuponi ya ofa NEWRIDER15. Muda wa kuitumia unakwisha siku 30 baada ya kuweka kuponi ya ofa kwenye akaunti yako ya Uber.

Aina za usafiri ukiwa eneo husika

 • UberX

  1-3

  Affordable rides, all to yourself

 • Comfort

  1-3

  Newer cars with extra legroom

 • UberXL

  1-5

  Affordable rides for groups up to 5

 • Uber Green

  1-3

  Low-emission rides

 • Uber Pet

  1-4

  Affordable rides for you and your pet

 • Connect

  1-4

  Send packages to friends & family

 • Pool - Unavailable

  1-2

  Temporarily unavailable

1/7

Kupata usafiri katika Uwanja wa Ndege wa Nashville

Ita gari ukiwa tayari kutoka nje

Na uchague gari linalotoshea wasafiri na mizigo mliyo nayo.

Fuata maelekezo hadi kwenye Ground Transportation Center

Eneo la kuchukuliwa kwenye Uwanja wa ndege wa BNA liko katika Ghorofa ya 1 ya Ground Transportation Center. Tafuta mabango yaliyoandikwa “Ride App Pickup.”

Kutana na dereva wako kando ya barabara

Mpate dereva wako katika sehemu ya kwanza kando ya barabara kwenye Maeneo ya A1 hadi B3 ya Ground Transportation Center.

Ramani ya Ramani ya Uwanja wa Ndege wa Nashville

Uwanja wa Ndege wa Nashville una kumbi 4, huku kituo cha kimataifa kikiwa kwenye Ukumbi wa A.

Maswali ambayo wasafiri wanauliza sana

 • Ndiyo. Bonyeza hapa ili uone orodha ya viwanja vya ndege kote duniani unakoweza kuitisha usafiri wa Uber.

 • Nauli ya usafiri wa Uber kuenda (au kutoka) Uwanja wa Ndege wa BNA inategemea hali kama vile aina ya usafiri, kadirio ya umbali na muda wa safari, ada ya vibali barabarani na idadi ya maombi ya usafiri.

  Unaweza kuona kadirio la bei kabla ya kuitisha usafiri kwa kuweka eneo la kuchukuliwa na mahali unakoenda katika zana ya kukadiria nauli katika Uber hapo juu. Kisha, unapoitisha usafiri utaona nauli yako halisi kwenye app kwa kutegemea hali za wakati huo.

 • Maeneo ya kuchukuliwa yanategemea aina ya usafiri unaoitisha na ukubwa wa uwanja wa ndege. Fuata maagizo kwenye App kuhusu eneo utakakomkuta dereva wako. Unaweza pia kuangalia mabango yanayoashiria maeneo ya usafiri wa pamoja yaliyobainishwa kwenye uwanja wa ndege.

  Ikiwa humpati dereva wako, wasiliana naye kupitia programu.

 • Msimbo wa uwanja wa ndege wa BNA ni ufupisho wa Berry Field Nashville.

Maelezo zaidi

Unatumia mfumo wa Uber kuendesha gari?

Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kurahisisha huduma unayopokea katika viwanja vya ndege, zikiwemo sheria na kanuni za nchi husika.

Je, unaelekea uwanja tofauti wa ndege?

Unaweza kupelekwa na kuchukuliwa kutoka zaidi ya viwanja 600 vya ndege kote duniani.

Maelezo kwaa wageni kwenye Uwanja wa Ndege wa Nashville

Kwa sasa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Nashville unahudumia mashirika 20 ya ndege na una safari 575 za kuwasili na kuondoka kila siku. Uwanja wa Ndege wa Nashville, ndio lango la kuingia Tennessee, na ni mwendo wa dakika 15 kwa gari wakati hakuna foleni au vikwazo vingine barabarani kutoka katikati ya jiji la Nashville, ambalo ndilo jiji kuu la jimbo. Jiji lipo maili 9 (kilomita 14) kutoka katika uwanja wa ndege.

Vituo katika Uwanja wa Ndege wa Nashville

Uwanja wa Ndege wa BNA una kituo kikuu kinachoitwa Robert C.H. Mathews Jr. Kituo. Kituo kina kumbi 4, A mpaka D zikiwa na malango 44 kote. Unaweza kupanga safari yako ukitumia taarifa zilizo hapa chini.

Ukumbi wa A

 • Air Canada
 • Frontier
 • United

Ukumbi wa B

 • Alaska
 • Boutique Air
 • British Airways
 • Contour
 • Delta
 • JetBlue
 • Sun Country
 • WestJet

Ukumbi wa C

 • American
 • Kusini magharibi

Kituo cha Kimataifa katika BNA

Uwanja wa Ndege wa BNA una safari za moja kwa moja kuelekea Bahamas, Kanada, Jamhuri ya Dominika, Jamaika na Meksiko, pamoja na safari ya moja kwa moja kwenda Heathrow, London. Maeneo ya kuondoka katika Uwanja wa Ndege wa Nashville yanapatikana katika Kumbi za A na B.

Kupata chakula katika Uwanja wa Ndege wa Nashville

Kuna zaidi ya maeneo 24 ya kupata mlo katika Kituo cha Mathews yanayouza vyakula na vinywaji mbalimbali, vikiwemo kahawa, sushi, vyakula vya kufungashiwa na sandwichi. Ukumbi wa maakuli katika Uwanja wa Ndege wa Nashville upo katika Ukumbi wa C, lakini kuna sehemu nyingine za kula katika kumbi zote.

Kusafiri katika Uwanja wa Ndege wa Nashville

Uwanja wa Ndege wa BNA una kituo kimoja kikuu cha wasafiri: Ikiwa unahitaji usaidizi wa ziada katika uwanja wa ndege, unaweza kuupata kwa kuwasiliana na shirika la ndege unalotumia.

Mambo ya kufanya katika Uwanja wa Ndege wa Nashville

Uwanja wa ndege wa BNA una maonesho ya sanaa ambayo huandaliwa na mpango wa sanaa katika Uwanja wa Ndege, na kuwashirikisha wasanii wa karibu, wa kikanda na wa kitaifa hivyo kuongeza uzuri katika uwanja wa ndege na kwa wageni wake. Hata hivyo sanaa katika BNA si maonesho ya kuona pekee. Kuna muziki ambao ni sehemu ya sanaa katika Nashville, na huandaliwa kila siku katika uwanja wa ndege.

Katika kumbi za B na C unaweza kupata sehemu ya kukandwa. Ukumbi wa C una saluni inayotoa huduma za kutunza kucha na nywele. Kuna maeneo 2 kwa ajili ya watoto kuchezea katika Ukumbi wa A na B.

Kubadilisha sarafu katika Uwanja wa Ndege wa Nashville

Huduma za kubadilisha fedha katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Nashville zinapatikana kati ya Ukumbi wa A na wa B na pia katika Kituo cha Wasafiri kilicho kati ya Ukumbi wa C na D.

Hoteli zilizo karibu na Uwanja wa Ndege wa Nashville

Iwe unasubiri ndege nyingine au ndege imechelewa usiku kucha, au kama unahitaji mahali pa kukaa karibu na BNA, kuna zaidi ya hoteli kadhaa na maeneo ya kukaa karibu.

Sehemu za kuvutia karibu na Uwanja wa Ndege wa Nashville

 • Bustani ya Cumberland
 • Maeneo ya muziki wa moja kwa moja karibu na Music Row na Lower Broadway
 • Jumba la makumbusho ya sanaa na historia katika Nashville

Pata maelezo zaidi kuhusu Uwanja wa Ndege wa Nashville hapa.

Facebook
Instagram
Twitter

Ukurasa huu una taarifa kutoka kwenye tovuti za washirika wengine ambazo hazisimamiwi na Uber na zinaweza kugeuzwa au kubadilishwa mara kwa mara. Maelezo yoyote yaliyojumuishwa kwenye ukurasa huu ambayo hayahusiani moja kwa moja na Uber au kazi zake yanatumika kuarifu tu na hayafai kutegemewa, au kuchukuliwa au kufasiliwa kwa namna inayoweka dhamana ya aina yoyote, iwe ya moja kwa moja au inayokisiwa, kuhusu maelezo yaliyo hapa. Baadhi ya masharti na vipengele hutofautiana kutegemea nchi, eneo na jiji. Ofa ya punguzo inawalenga watumiaji wapya pekee. Huwezi kutumia ofa hii pamoja na ofa nyinginezo na haiwezi kutumiwa katika bakshishi. Inapatikana kwa muda mfupi. Vigezo na masharti ya ofa vinaweza kubadilika.