Ruka uende katika maudhui ya msingi
Uber
Uber

Uwanja wa Ndege wa Amsterdam Schiphol (AMS)

Iwe unasafiri kuelekea jijini Amsterdam kutoka Uwanja wa Ndege wa Schiphol au kutoka jijini Amsterdam kuelekea Uwanja wa Ndege wa Schiphol, iamini Uber kukufikisha unakoenda.

Evert van de Beekstraat 202, 1118 CP Schiphol, Netherlands
+31 20-794-0800

Itisha usafiri kote ulimwenguni

Bonyeza tu kitufe ili upate usafiri wa angani katika zaidi ya viwanja vikuu 500.

Safiri kama mwenyeji

Acha programu na dereva wako ashughulikie masuala ya kina ili usisumbuke kutafuta maelekezo katika jiji ambapo wewe ni mgeni.

Safiri bila wasiwasi kwa kutumia Uber

Pata vipengele unavyovipenda, ikiwa ni pamoja na bei zinazooneshwa moja kwa moja na uwezo wa kulipa bila pesa taslimu, hata ukiwa ugenini.

Sampuli za bei za msafiri ni makadirio tu na hazioneshi mabadiliko yanayotokana na mapunguzo, kucheleweshwa kwenye foleni na mambo mengine. Tunaweza kutumia nauli isiyobadilika na bei za chini zaidi. Bei halisi zinaweza kubadilika.

 • UberX1-4

  Affordable, everyday rides

 • Black1-4

  Premium rides in luxury cars

 • Gari aina ya Van1-7

  Spacious rides for groups up to 7

Fungua programu yako ili kuitisha usafiri

Ukishakuwa tayari, fungua programu yako na uitishe usafiri. Chagua usafiri unaotoshea idadi ya wasafiri na mizigo mliyo nayo.

Fuata maelekezo katika programu

Utapata maelekezo kuhusu maeneo ya kuchukua wasafiri moja kwa moja katika programu. Pia kunaweza kuwa na alama katika uwanja wa ndege.

Kutana na dereva wako

Nenda katika eneo la kuchukuliwa jinsi ilivyobainishwa katika programu. Tafadhali kumbuka, eneo hilo huenda halitakuwa karibu kabisa na lango unaloondokea. Ikiwa humpati dereva wako, wasiliana naye kupitia programu.

WiFi katika AMS

WiFi inapatikana bila malipo katika maeneo yote ya ndani ya Uwanja wa Ndege wa Amsterdam. Ingia katika akaunti ya mtandao wa Schiphol ili uweze kutumia kwa saa 4. Unaweza kuingia tena katika akaunti baada ya saa hizo 4 kuisha ili uweze kuendelea.

Maegesho katika uwanja wa ndege wa Schiphol

Kuna aina nyingi za maegesho katika uwanja wa ndege wa Schiphol. P1, Maegesho ya Muda Mfupi ni kwa ajili ya kuwachukua na kuwashukisha wasafiri, huku P3, Maegesho ya Muda Mrefu kwa wanaokawia.

Kuhifadhi mizigo katika Uwanja wa Ndege wa Schiphol

Unaweza kutumia depo la mizigo katika uwanja wa ndege wa Schiphol kuhifadhi mifuko na mizigo mikubwa kwa hadi siku 30. Depo lipo katika sehemu ya chini kati ya Vituo vya Wanaowasili vya 1 na 2, ada za Schiphol za kuweka mizigo zinategemea aina ya mzigo wala si uzani.

Uber inapatikana katika Uwanja wa Ndege wa Amsterdam, kwa hivyo unaweza kufurahia usafiri wa starehe na uhakika popote unapotaka kwenda.

Ili kupata eneo la kuchukuliwa, angalia programu ya Uber baada ya kuitisha usafiri.

Hata kama safari si ndefu sana, ada za Uber kutoka na kwenda Uwanja wa Ndege wa Schiphol zinaweza kuathiriwa na muda, foleni na masuala mengine. Angalia mfumo wa kukadiria nauli za Uber ili ufahamu makadirio ya nauli ya safari.

Muda wa kuchukuliwa unaweza kutofautiana kulingana na wakati, idadi ya madereva wanaopatikana na masuala mengine.

Unatumia mfumo wa Uber kuendesha gari?

Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kurahisisha huduma unayopokea katika viwanja vya ndege, zikiwemo sheria na kanuni za nchi husika.

Je, unaelekea uwanja tofauti wa ndege?

Unaweza kupelekwa na kuchukuliwa kutoka zaidi ya viwanja 500 vya ndege kote duniani.

Uber ndiyo chaguo bora ya kusafiri kuenda na kuondoka kwenye Uwanja wa Ndege wa Amsterdam Schiphol (AMS). Itakuchukua dakika 20 kufika Uwanja wa Ndege wa Schiphol kutoka katikati mwa jiji la Amsterdam. Hupatikana kwa urahisi na wasafiri wa kwenda na kuondoka mji wa Amsterdam. Njia za usafiri katika Uwanja wa Ndege wa AMS ni pamoja na treni, basi na teksi huhakikisha kuwa wasafiri na wakaazi wengine wa Uholanzi wanapata huduma bora. Uber pia inapatikana ili kukuwezesha kufika unakoenda kwa urahisi.

Vituo katika Schiphol

Uwanja wa Ndege wa Schiphol una kituo kimoja kikuu cha wasafiri kilichoagawanywa katika ghorofa 3. Katika ghorofa ya chini ya Kituo cha Uwanja wa Ndege wa Schiphol, utapata eneo la wanaowasili, pamoja na migahawa, maduka makuu na huduma nyingine mbalimbali zikiwemo vyumba vya mapumziko na ususi. Ghorofa ya 2 ina maeneo ya kukaguliwa na kuondoka, ilhali daraja ya 3 iina maeneo ya sebule za VIP. Ndege zinazoondoka katika uwanja wa Ndege wa AMS zinajumuisha:

 • Croatia
 • Delta
 • HOP!
 • Jet2.com
 • United

Migahawa ya Uwanja wa Ndege wa Schiphol

Uwanja wa Ndege wa Amsterdam Schiphol una sehemu mbalimbali za kula na kunywa, zikiwemo vibanda vya vyakula, migahawa na baa. Uwanja wa ndege wa Amsterdam una aina nyingi za vyakula kutoka kila bara, vikiwemo vyakula kutoka Mediterania na Vyakula halisi vya Uholanzi. Kwa hivyo, huwezi kukosa mlo unaotaka.

Kusafiri kwenye Uwanja wa Ndege wa AMS

Kwa kuwa kuna kituo kimoja tu cha wasafiri kwenye uwanja wa ndege wa Schiphol, ni rahisi kutembea.

Mambo unayoweza kufanya kwenye Uwanja wa Ndege wa AMS

Utapata bidhaa za kipekee kama vile wanasesere, vidude vya kuchezea, jibini na chokoleti wakati wowote kwenye maduka ya Uwanja wa Ndege wa Schiphol. Kabla ya kuondoka kwa ndege, mbona usimnunulie unayempenda zawadi? Utapata aina ya mapambo na vipodozi kochokocho kwenye maduka ya Uwanja wa Ndege wa Amsterdam. Isitoshe, kutokana na kuwepo kwa maduka mengi yanayouza bidhaa zisizotozwa ushuru kwenye Uwanja wa Ndege wa Amsterdam, AMS ni mahali bora zaidi pa kununua zawadi maridadi kwa ajili ya ndugu na marafiki kwa bei nafuu.

Kubadilisha sarafu kwenye Uwanja wa Ndege wa Schiphol

Kibanda cha kubadilisha sarafu katika ABN AMRO Exchange Schiphol kinakuwezesha kubadilisha aina 60 za sarafu. Kinamfaa mtu yeyote anayetaka kuwa na pesa chache taslimu kabla ya kuzuru Amsterdam. Hutatozwa ukibadilisha kiasi kisichopungua Yuro 200; ikiwa unabadilisha chini ya kiasi hicho, utahitaji kulipa ada ndogo. Kwa hivyo ni bora kubadilisha pesa nyingi ikiwa unapanga kukawia.

Migahawa kwenye Uwanja wa Ndege wa Amsterdam

Migahawa mingi inafikiwa kupitia usafiri wa Uber katika Uwanja wa Ndege wa AMS. Pia kuna migahawa mbalimbali katika Uwanja wa Ndege wa Amsterdam ambako unaweza kwenda kwa miguu. Kwa hivyo wakati wowote unapowasili, iwe unawasili alfajiri au usiku wa manane, una uhakika wa kupumzika. Isitoshe, kuna vituo vya biashara vinavyopatikana katika migahawa mingi. Vituo hivi vinawafaa wafanyabiashara popote walipo.

Sehemu za kuzuru karibu na Schiphol

Wakati unasubiri ndege nyingine katika Uwanja wa Ndege wa Schiphol, kuna mambo mengi unayoweza kufanya, haswa ikiwa unaweza kuzuru mji wa Amsterdermr:

 • Anne Frank House
 • Dam Square
 • Rijksmuseum
 • Royal Palace

Pata maelezo zaidi kuhusu Uwanja wa Ndege wa AMS hapa.