Products

Usalama wako ni muhimu sana kwetu

October 11, 2018 / Tanzania

Usalama wako ni muhimu sana kwetu – kabla, kipindi cha, na hata baada ya safari. Ndio maana tuna-jitahidi kutengeneza teknolojia itakayo kupa amani pindi unaposafiri na Uber.

Malipo yanafanyikaje?

Malipo yanafanyika kupitia njia uliyochagua kwenye akaunti yako ya Uber. Kama ulichagua kulipia pesa tasilimu, basi mwisho wa safari utampa dereva-mshirika pesa tasilimu.

Naweza kumuani dereva?

Dereva- mshirika lazima afanyiwe ukaguzi pamoja na gari lake. Hii inamaanisha una safirishwa na gari lenye hadhi nzuri, na pia dereva mzuri, Hivyo kuwa na amani!

Dereva-mshirika anaweza kuona taarifa zangu binafsi?

Dereva-mshirika hawezi kuona taarifa zako binafsi – hii ikijumuisha email yako, njia yako ya malipo na namba yako ya simu. Tunatumia teknolojia amabayo inaweza kuficha taarifa zako pindi unawasiliana na dereva-mshirika.