Stories

Tunaadhimisha miaka 5, Afrika! #5Years5Stars

September 11, 2018 / Tanzania

Tulianza kwa kutumia simu kuita usafiri, na miaka michache baadaye tumepanua wigo wetu – kuanza kutoa huduma katika miji mbalimbali, kuwasili kwa muda pale unapohitaji usafiri wetu na kutengeneza nafasi za ajira kwa maelfu ya watu.

Tulifungua milango yetu barani Afrika miaka mitano iliyopita na tungependa kuku shukuru kwa kutukaribisha na kushirikiana nasi katika safari hii ambayo imeleta mabadiliko makubwa katika mfumo wa usafiri. Tumewasaidia watu mbalimbali kwenda kukutana na marafiki baada ya siku ndefu, kwenda sokoni na hata kufika hospitali kwa wakati kwa wale mama zetu walio karibu kujifungua,hii ni furaha kubwa kwa familia – ufanisi huu umepatikana kupitia ushirikiano mkubwa tuliopata kutoka kwa wadau wote, na bila shaka wewe umekuwa nguzo muhimu katika safari hii!

Mwaka huu tunaadhimisha miaka mitano ya huduma zetu na bara la Afrika ni maarufu kwa maeneo 5 ambayo tumepiga hatua kubwa yanayojulikana kama Big 5, tumeona kuna haja ya kukufahamisha kuhusu haya maeneo matano muhimu, maarufu kama BIG 5 yanayoainisha jinsi Uber ilivyoleta mabadiliko chanya katika sekta ya usafiri:

Ujio wa Uber umeleta mabadiliko gani katika maisha ya watu? Mabadiliko mengi! Uber imekuwa mbadala wa kumiliki gari kwa wasafiri zaidi ya milioni 1.3 kusini mwa Jangwa la Sahara, tumerahisisha safari zako na sasa unaweza kusafiri mjini bila ugumu wowote. Isitoshe, tumeanzisha huduma za bei nafuu kama UberCHAPCHAP, UberPOA na uberBODA, kwa hiyo, kila mtu sasa anaweza kufurahia huduma zetu.

Tumetengeneza nafasi za ajira zaidi ya 36 000 ndani ya hiki kipindi kifupi ambacho tumekuwa katika bara la Afrika! Madereva wanaokuchukua usiku wa manane ukiwa umechelewa kurudi nyumbani, wanaokupeleka kwenye mtoko na marafiki zako, na wale wanaohakikisha kwamba unawahi kuhudhuria vikao na mikutano mbalimbali. Hawa ndio mashujaa wa UberHEROES.

Tuna mpango endelevu wa kuimarisha vipengele vyetu vya usalama, ili ujisikie salama zaidi kabla ya safari kuanza, unapokuwa safarini au hata baada ya safari kukamilika.  Aidha, unaweza kumwonesha ndugu au rafiki safari yako mahali ulipofikia ukiwa safarini na zaidi ya yote unaweza kupata usaidizi usiku na mchana mwaka mzima.

Magari yanayotumiwa na mtu mmoja ndio chanzo kikubwa cha foleni ya magari katika miji mingi kusini mwa Jangwa la Sahara, sambamba na kuongeza uchafuzi wa mazingira. Kampuni ya Uber, imedhamiria kupunguza makali ya hali hii kwa kujaribu kupunguza idadi ya magari barabarani, hasa kupitia mpango wa watu wengi kujichanga na kutumia gari moja-mpango huu umepokelewa vizuri na watu wanazidi kuuchangamkia.

Uber ni zaidi ya magari, tumepiga hatua kubwa katika bara la Afrika na sasa Uber inatoa huduma nyingine ya Uber EATS kwa kushirikiana na migahawa maarufu nchini Afrika Kusini na Kenya. Tuna mpango endelevu wa kupanua wigo wa huduma zetu ili kutosheleza mahitaji yako. Pakua app ya UberEATS hapa.

Tumeingia awamu muhimu ya huduma zetu katika bara la Afrika #UBERMOVESAFRICA #5YEARS5STARS