Products

Tulipata maoni yako na tumeamua kuyafanyia kazi: Tumezindua namaba za simu za kuripoti matukio ili kuimarisha usalama wako

July 20, 2018 / Tanzania

Tumepokea maoni kutoka kwa wasafiri wengi wanaotumia Uber jijini Dar es Salaam, na wameeleza umuhimu wa kupewa namba wanazoweza kutumia kuwasiliana na ofisi zetu kunapokuwa na tukio linalohatarisha usalama wao. Ndiyo maana kampuni ya Uber ina furaha kubwa kuwatangazia namba za simu za Timu ya Matukio ya Dharura katika Kusini mwa Jangwa la Sahara. Namba hizi ni mkakati endelevu wa kuimarisha usalama wa wasafiri wanaotumia huduma yetu.

Sasa kuna neema kubwa kupitia namba hizi za Timu ya Matukio ya Dharura ambazo wasafiri wanaweza kupiga taarifa ya tukio lolote linalohatarisha usalama wao au ajali ndani ya app usiku na mchana. Baadaye wasafiri watapigiwa simu na Timu ya Matukio ya Dharura (IRT) haraka iwezekanavyo!

Kutumia namba za simu za Timu ya Matukio ya Dharura (IRT):

  • Fungua menyu ya app ya Uber, na ubonyeze ‘Usaidizi’
  • Bonyeza ‘Safari na Mapitio ya Nauli’
  • Chagua safari husika
  • Chagua ‘kulikuwa na tukio la kiusalama’
  • Tuma tiketi ya tukio hilo ukijumuisha namba zako za simu na maelezo mafupi ya tukio husika
  • Msafiri atapigiwa simu haraka iwezekanavyo!

Bila shaka ni haki ya kila mtu kujisikia salama, iwe wanatumia usafiri wa treni, taksi, daladala, au anatumia Uber. Ingawa hakuna usafiri ambao ni salama 100% au ambao hauna matukio yanayohatarisha usalama wa msafiri, programu za teknolojia kama Uber zinaweza kusaidia kuimarisha usalama, na ndiyo maana namba hizi za Timu ya Matukio ya Dharura zitakuwa na mchango mkubwa katika kuimarisha usalama wa wasafiri.

Ingawa Uber imeweka kipaumbele kwenye usalama wa wasafiri, tunawashauri wasafiri watumie namba za simu za dharura za kitaifa wakati wowote kunapokuwa na tukio linalohatarisha usalama wako.