Products

Marekebisho kwa ajili ya kuboresha usalama wako.

September 18, 2018 / Tanzania

Zinapatikana kwa urahisi

Zana mpya kwenye programu ya Uber husaidia katika kuhakikisha kwamba uko salama unaposhirikiana na Uber. Pata maelezo kuhusu jinsi zana mpya kwenye programu yako zinasaidia kuhakikisha kwamba umeunganishwa na uko salama. Ikiwa hujaanza kutumia programu mpya bado, jipatie tolea jipya kwenye duka la app/play store.

Kuna dharura? Pata usaidizi haraka

Sasa usaidizi wa dharura sasa unapatikana ndani ya programu. Ikiwa kuna tukio la dharura unapokuwa safarini, unaweza kupiga simu kwa [112] kupitia programu. Na ikiwa unatumia Uber unaposafiri nje ya nchi yako, programu hupiga simu kwa huduma za dharura katika eneo ulipo. Mahali ulipo na maelezo ya safari yataonekana vyema ili uyatume kwa mhudumu wa kituo cha usaidizi wa dharura.

Mahali unapoweza kupata majibu

Tembelea Kituo cha Usalama kwenye programu ili upate usaidizi wakati wa safari yako. Bonyeza aikoni ya ngao ili ufikie zana muhimu mahali moja. Pia unaweza kupata maelezo kuhusu mambo tunayofanya ili kuhakikisha uko salama unaposafiri ukitumia mfumo wa Uber.