Driver Announcements

Jiandae kwa ajili ya usiku wa mwaka mpya

December 21, 2017 / Tanzania

Anza 2018 na kipato cha ziada

 

Ufanye usiku wa mwaka mpya huu kuwamzuri kwako na kwa wasafiri wako. Tupo hapa kukusaidia kupangilia ratiba yako siku hiyo

Jiandae na safari za mwaka Mpya Dar Es Salaam itawaka siku ya mwaka mpya. Kwahiyo tegemea safari nyingi kuanzia tarehe 31 saa 10 jioni.

Muda mzuri kuwa online

Jipange mapema kuongeza kipato chako, jua ni mida gani ambayo ina maombi mengi ya safari.Tunategemea siku ya mwaka mpya kuwa na maombi mengi sana.

Maombi yataongezeka kuanzia saa 10 jioni - saa 4 usiku, na baada ya mwaka mpya kuingia saa 6.30 usiku mpaka saa 9 usiku wasafiri watakuhitaji zaidi

Vidokezo kwa ajili ya Mwaka mpya

Mjue msafiri wako

Utaona taarifa za msafiri kabla ya kumchukua. Hakikisha jina lake kabla hajapanda kwenye gari.

Liache gari lako likiwa safi

Kama msafiri amachafua gari unaweza ukamdai ada ya kusafisha gari kupitia app yako ya Uber.

Shirikisha ndugu kwenye safri yako

Kuwa na amani. Sasa unaweza kuwashirikisha uwapendao kwenye safari yako kupitia app yako, na wakajua uko wapi muda huo.

Malipo wakati unasubiria kuanzisha safari

Ukifika kwenye eneo la kumchukua msafiri, utaanza kulipwa kwa dakika, kuanzia dakika mbili toka ulipo fika kwenye eneo la kumchukua msafiri.