Stories

Mwongozo wa kusaidia safari salama msimu huu wa sikukuu

December 18, 2017 / Tanzania

Msimu wa sikukuu umeshafika, na tunataka kuhakikisha ya kwamba unafurahia sikukuu yako. Katika kipindi hiki ni muhimu sana kuzingatia usalama ili kufika nyumbani salama.

Iwe ni safari za mchana au hata safari za usiku wa manane, ni muhimu sana kuzingatia vipengele vya usalama vya Uber.

 

Kaa ndani mpaka pale unapotaka kuanza safari

Uzuri wa uber mi kwamba unaweza kuomba usafiri hata ukiwa ndani ya nyumba. Hamna shida ya kutoka na kuhangaika barabarani- utapewa taarifa pale dereva wako anapokaribia kufika. Ni vizuri kutoka pale ambapo dereva anakaribia kufika kwenye eneo lako.

Hakikisha taarifa hizi

Upo tayari kuanza safari yako? Hakikisha unaangalia vizuri taarifa za usafiri wako.

  • Hakikisa rangi ya gari inaendana na ile iliyopo kwenye app yako ya Uber
  • Hakikisha namba ya gari ni sawa na ile iliyoonyeshwa kwenye app
  • Hakikisha jina la dereva na picha yake kabla ya kupanda gari

Wajulishe ndugu na jamaa ukiwa safarini

Kwa kubonyeza “Share status” ukiwa safarini unaweza kushiriki taarifa za safari yako na ndugu pamoja na jamaa zako. Unakutana na marafiki zako? Wana weza kuangalia safari yako mwanzo hadi mwisho, pia itawawezesha kujua utafika wakati gani.

Kitu cha kutokusahau ni kufunga mkanda wako


Kuna mambo mengi sana yanatokea barabarani wakati wa kipindi hiki cha sikukuu, ukiingia tu kwenye gari kitu cha kwanza kufanya ni kufunga mkanda.

Kuhakikisha usalama

Sio lazima kutoa taarifa zako binafsi kwa dereva, na hata dereva kukupa wewe taarifa zake binafsi. Kama unahisi kuna hali hatarishi, fuata hisia zako, Kwenye kipindi kama hicho piga 112 kupata msaada wa polisi.

Na kama unakunywa, kwa usalama zaidi agiza Uber yako ikufikishe nyumbani salama