Driver Announcements

Furahia kazi yako

November 3, 2017 / Tanzania

Tuna nia ya kufanya kazi yako iwe inalipa na kukupunguzia adha za kila siku. Muda wako ni wa thamani na mabadiliko haya yatakusaidia kuokoa muda.

Malipo unapomsubiria msafiri

Sasa abiria wanatakiwa kurequest usafiri pale tu wanapo taka kuondoka, tuna jua kama kuna muda mko tayari kusubiria lakini pale muda unapokua mwingi msafiri itabidi alipie.

Malipo ya kumsubiria msafiri yataanza dakika 5 baada ya wewe kufika eneo la kumchukua msafiri. Inafanyaje kazi? Utaona kisaa kwanye app kinachokuambia kwamba umeanza kulipwa kwa kumsubiria msafiri. Hii itaongezeka baada ya safari kumalizika na utaonywesha kwenye risiti yako.

Ulinzi wa nyota zako

Kuna wakati msafiri anaweza kutoa nyota chache kwa vitu ambavyo vipo nje ya uwezo wako wewe kama dereva-mshirika, vitu kama app na foleni, zamani nyota hizi zilikuwa zinauwezo wa kushusha nyota zako, lakini sasa hii haitaweza kubadilisha tathmini ya nyota zako.

Kuchat ndani ya app

Sasa tumerahisisha mawasiliano yako na msafiri, unaweza kumtumia message moja kwa moja kupitia app yako ya Uber, pale ambapo unataka kuwasiliana na msafiri unaeenda kumchukua utaona option ya kupiga simu au kutuma message. Unaweza ukajibu message kwa haraka kwa kubonyeza kitufe cha dole gumba. Ujumbe ukija unaweza kusomewa kama umeweka sauti kwenye rambaza yako.