Huenda ukatatizika wakati wa kujisajili au kupokea taarifa kutoka kwa mwanatimu wa mauzo. Tafadhali angalia tena kwani upatikanaji wa bidhaa unaweza kubadilika.
Chunguza machaguo ya usafiri katika eneo lako kwenye programu ya Uber
Majiji yanaendeshwa kwenye mitandao ya usafiri. Sasa unaweza kupata yako kwenye Uber. Punguza kiwango cha hewa ya ukaa unayozalisha na upambane na msongamano wa magari. Tutakusaidia ufike mahali unakoenda, bila kujali jinsi utakavyofika huko.
Safiri ukitumia usafiri wa umma bila usumbufu
Achana na ratiba tata za wakati, uhamisho wenye shughuli nyingi na kusubiri kusikotarajiwa huku ukipunguza uzalishaji wa hewa ya ukaa kwenye safari yako. Pata taarifa za barabara za wakati halisi katika kila hatua.
Chunguza jumuiya yako
Angalia mtandao wa usafiri wa eneo lako kwa kutupia jicho, bila kutumia ramani zinazochosha, ratiba zinazokanganya na ucheleweshaji wa kushtukiza.
Punguza kiwango cha hewa ya ukaa unayozalisha
Fika mahali unakoenda huku ukipunguza matumizi ya mafuta. Sasa ni rahisi kuchagua usafiri usiochafua mazingira.
Punguza msongamano wa magari
Punguza idadi ya magari barabarani kwa kuchagua barabara ya basi, treni ya chini ya ardhi au treni katika eneo lako.
Jinsi Mipango ya Safari inavyofanya kazi
Iwe unasafiri kwenda kazini au unaelekea kupata chakula cha saa tano asubuhi, tovuti yetu inafanya usafiri katika eneo lako uwe rahisi kama vile kutumia usafiri wa pamoja. Panga barabara yako, nunua tiketi na upate taarifa za usafiri za wakati halisi. Hayo yote kwenye programu ya Uber.
Angalia chaguo la usafiri linalopatikana katika mahali pamoja
Pata taarifa yote unayohitaji kwenye skrini moja. Weka mahali unakoenda na programu ya Uber itakutafutia barabara, miunganisho, bei na nyakati za kuwasili.
Tambua barabara zinazofaa zaidi kwa ajili ya safari yako
Pata taarifa ya usafiri ya wakati halisi na uchague barabara ya haraka zaidi ya kukufikisha mahali unakoenda.
Pata maelekezo ya kina kuhusu mahali unakoenda
Pata maelekezo ya hatua kwa hatua kutoka mwanzo hadi mwisho, ikiwemo uhamishaji kati ya magari ya usafiri na sehemu za kuvukia barabara.
Nunua tiketi za usafiri kwa urahisi kwenye programu
Hakuna haja tena ya kuwa na wasiwasi kuhusu foleni kwenye kioski cha usafiri au kushikilia tiketi za karatasi. Nunua na uhifadhi tiketi za usafiri moja kwa moja kwenye programu ya Uber.
Fika mahali unakoenda kwa kutumia Uber Transit
Kuhusu